Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Waziri mwenye dhamana wa mambo ya ndani. Wewe una dhamana juu ya usalama wa raia na mali zao. Hakuna raia anayependa kutetea watu wanaojihusisha na uhalifu. Ila nchi yetu inatawaliwa na kuongoza kwa misingi ya sheria na haki.
Tarehe 26/10/2019 watuhumiwa wapatao watano walikamatwa na Migambo ambao walitumwa na mtendaji wa Kata ya kahama Wilaya ya Ilemela mkoani mwanza kwa tuhuma ya wizi wa Milango. Kuna Mwanajeshi ambae anadai kuwa alikuwa ameibiwa Tv flat screen alianza kuwapiga watuhiwa na kuwatesa akidai hawa ndio wezi wa Tv yake. Mmoja wa watuhumiwa hao maarufu Omela alipigwa sana na alifariki. Mmoja wa watuhumiwa alipigwa na kug'olewa jino. Raia mwema mmoja alijaribu kusaidia ili watuhumiwa wapelekwe polisi nae alipigwa.
Ndugu za marehemu wanaogopa hata kufuatilia kesi hii. Polisi Kirumba wamedanganya kuwa walipigwa na wananchi wenye hasira kali. Katiba ya jamhuri ibara ya 13(6)(b) ipo wazi juu ya watu kutojichukulia sheria mikononi.
Tukio hili la watuhumiwa kupigwa na kuteswa mpaka mmoja akafa limefanyika ndani ya ofisi ya mtendaji wa kata ya kahama wilaya ya Ilemela na mtendaji na mwenyekiti walikuwepo. Sasa kwa nini wapotoshe kuwa walipigwa na wananchi wenye hasira kali!