Mwanajeshi awatesa vijana na mmoja kufariki akiwatuhumu kumwibia tv yake. Je, hii ni haki?

Mwanajeshi awatesa vijana na mmoja kufariki akiwatuhumu kumwibia tv yake. Je, hii ni haki?

Is
Huyu jiwe mnampa promo sana. Yaani hata nasuala ya mahakamani mnataka akayaamue yeye? Yeye ndiye muweza wa yote Tqnzania (mungu wa Tanzsnia)??

Tunazidi kunjengea udikteta zaidi
Ishu hii sio ya kimahakama.tukio.limetokea ofisi ya mtendaji wa kata.
 
Is
Ishu hii sio ya kimahakama.tukio.limetokea ofisi ya mtendaji wa kata.
Kwaiyo kama siyo ya kimahakama ni ya nani kwamba raisi anatoa hukumu kama mtu alifia ofisini sababu ya kipigo kuna njia za kuwasilisha maombi ata mahakamani kikubwe kuwe na ripoti ya hispitali na mashahidi mtafute wakili ambaye atawasilisha maombi yenu mahakamani siyo kila kitu kumpa shida Raisi wakati nyie hamjachukua hatua yoyote
 
Una maana mtu akiuliwa ndani ya ofisi ya mtendaji sio jinai?
Ni jinai ila hapa kuna ishu kama tatu tambua kuna kuwawajibisha watumishi wa umma na kuna ishu ya jinai pia halafu kumbuka watumishi wote wanamuwakilisha Rais.
 
Sawa tukiwa hapo kwa ajili ya sherehe za Uhuru tutajaribu kupenyeza kimemo
 
Hivi kila anayepigwa akimpelekea mashtaka huyo rais wenu, ataanzia wapi kusikiliza yote?

Huko chini hakuna mabaraza na mahakama?

Hakuna rufaa?

Hakyna vyombo vya kushitaki?

Hakuna TAKUKURU mkoa?

Umemtafuta Mkuu wa TAKUKURU Mwanza?
 
Kiranga,
Yule mama kahama ambae mume wake aligongwa na trafiki mlevi asingemuona rais angepata haki yake?
 
Kwaiyo kama siyo ya kimahakama ni ya nani kwamba raisi anatoa hukumu kama mtu alifia ofisini sababu ya kipigo kuna njia za kuwasilisha maombi ata mahakamani kikubwe kuwe na ripoti ya hispitali na mashahidi mtafute wakili ambaye atawasilisha maombi yenu mahakamani siyo kila kitu kumpa shida Raisi wakati nyie hamjachukua hatua yoyote
Hii ishu inahusu sehemu nyingi.utawala bora ,mahakama nk.usikariri sana .
 
Yule mama kahama ambae mume wake aligongwa na trafiki mlevi asingemuona rais angepata haki yake?
Watanzania wote wenye vikesi vyao wakimpelekea raisi huyo rais atafanya kazi gani ya urais na hizo kesi ataziamulia lini?

Moja ya matatizo makubwa ya Afrika ni haya.

1. Watu wengi wanapenda shortcuts. Kuna mifumo imeoza, badala ya kujikita tubadili mifumo kila mtu afaidike, tynakimbikia kwa mtu mmoja aliye juu ambaye hawezi kusaidia kila mtu.

2.Watu wengi hawana long term planning for long term solution. Wanaoenda kuangalia inapoishia oua tu. Mama hiyu ana tatizo? Mpelekee rais alitatue. Hatuangalii kesho yatatokea matatizo ishirini kama hayo kika wilaya, na keshokutwa ishirini mengine. Rais atataua yote hayo? Kwa nini tusiangakie tatizo la kimfumo?

3. Watu engi wana ubinafsi. Mtu anataka kutatua tatizo lake yeye tu, hajali wengine watatauaje matatizo yao.

4. Wengi wanatumia hisia badala ya mantiki. Mtu akija na story yenye kutia huruma, tunashindwa kuangalia tatizo kwa ujumla wake na kutoa mpango wa kuwajibisha watu wa chini wasiofanya kazi zao vizuri. Tunataka kwenda kwa rais tu kwa kutumia hisia.

5. Watu wengi wanaoenda kuangalia watu badala ya mifumo, kua zia juu badala ya chini.

Kwa kufikiri hivi, nchi haiwezi kuendelea.

Mtampelekea rais vikesi vya kuibiana nguo, hata huyo rais mwenyewe atawadharau na kuona hawa watu hawafai kuheshimiwa nami.

Ndiyo maana li Magufuli linatukana tukana ovyo live nila aibu.

Lishaona watu wenyeee hawa wengi wana syndrome ya hewala hewala.

Wengi wao wanamuona Magufuli kama demigod.
 
Makosa yapi?
Aliyeachiwa kwa rushwa ni mwanajeshi au mtuhumiwa wa wizi wa vifaa vya mwanajeshi?

Je wewe upo upande gani katika utetezi?

Kujichukulia sheria mkonini ni kosa na kumuibia mwanajeshi nalo ni kosa.

Sema sasa upo upande gani wa shilingi,maana pyepyepye nyiiiiingi!
 
Ni jinai.ila hapa kuna ishu kama tatu tambua.kuna kuwawajibisha watumishi wa umma na kuna ishu ya jinai pia.Alafu kumbuka watumishi wote wanamuwakilisha rais.
Aliyeachiwa kwa rushwa ni mwanajeshi au mtuhumiwa wa wizi wa vifaa vya mwanajeshi?

Je wewe upo upande gani katika utetezi?

Kujichukulia sheria mkonini ni kosa na kumuibia mwanajeshi nalo ni kosa.

Sema sasa upo upande gani wa shilingi,maana pyepyepye nyiiiiingi!
Unauhakika alimuibia? Ishu haikufika mahakamani unaanza ku...
 
Kiranga,
Use common sense.hapa watu waliteswa na mmoja alifariki.huko ni kuibiana nguo? Unaweza jifanya mjuaji kumbe makamasi tu.Watu wamefungiwa ndani ya ofisi ya kata na kuteswa kwa kipigo kikali.
 
Back
Top Bottom