Yule mama kahama ambae mume wake aligongwa na trafiki mlevi asingemuona rais angepata haki yake?
Watanzania wote wenye vikesi vyao wakimpelekea raisi huyo rais atafanya kazi gani ya urais na hizo kesi ataziamulia lini?
Moja ya matatizo makubwa ya Afrika ni haya.
1. Watu wengi wanapenda shortcuts. Kuna mifumo imeoza, badala ya kujikita tubadili mifumo kila mtu afaidike, tynakimbikia kwa mtu mmoja aliye juu ambaye hawezi kusaidia kila mtu.
2.Watu wengi hawana long term planning for long term solution. Wanaoenda kuangalia inapoishia oua tu. Mama hiyu ana tatizo? Mpelekee rais alitatue. Hatuangalii kesho yatatokea matatizo ishirini kama hayo kika wilaya, na keshokutwa ishirini mengine. Rais atataua yote hayo? Kwa nini tusiangakie tatizo la kimfumo?
3. Watu engi wana ubinafsi. Mtu anataka kutatua tatizo lake yeye tu, hajali wengine watatauaje matatizo yao.
4. Wengi wanatumia hisia badala ya mantiki. Mtu akija na story yenye kutia huruma, tunashindwa kuangalia tatizo kwa ujumla wake na kutoa mpango wa kuwajibisha watu wa chini wasiofanya kazi zao vizuri. Tunataka kwenda kwa rais tu kwa kutumia hisia.
5. Watu wengi wanaoenda kuangalia watu badala ya mifumo, kua zia juu badala ya chini.
Kwa kufikiri hivi, nchi haiwezi kuendelea.
Mtampelekea rais vikesi vya kuibiana nguo, hata huyo rais mwenyewe atawadharau na kuona hawa watu hawafai kuheshimiwa nami.
Ndiyo maana li Magufuli linatukana tukana ovyo live nila aibu.
Lishaona watu wenyeee hawa wengi wana syndrome ya hewala hewala.
Wengi wao wanamuona Magufuli kama demigod.