Kwanini anaanza kumshukuru Mungu badala ya Samia? Mwanangu nimekukubali. Sina shaka akina Kikwete na Mwigulu watakosa usingizi wasijue huu unaweza kuwa mwanzo wa mwisho. Afande umekosea kuingiza mambo madogo kama sakata la tapeli gwajima. Hapo, umeniboa sana mwanangu.
Waliomtuma huyu dogo wajanja na wanaweza kuzua jambo. Akikamatwa, wanajeshi wa rika lake wanaweza kuwageuka wakubwa zao. Wasipomkamata, itaonekana jeshi liko nyuma yake. Lolote litakalofanyika, laweza kuwa kitufe cha kuiingiza Tanzania kwenye jeshi kutwaa madaraka. Sijui haya ndiyo madhara ya Kapteni Ibrahim Traore au legacy ya Magufuli.