Mwanajeshi kumshambulia dereva wa daladala ikiwa na abiria ni kuhatarisha maisha ya abiria pia

Mwanajeshi kumshambulia dereva wa daladala ikiwa na abiria ni kuhatarisha maisha ya abiria pia

Dereva wa daladala huwa wanamatatizo naamini mwenye kosa ni dereva.. msijifanye hamuwajui hao dereva wa daladala..
clips kama hizi wakati kama huu wa mnaojiandaa na maandamano.. message sent
 
Kosa litakuwa ni kutembeza kichapo huku gari likiwa linatembea angemwambia aegeshe kwanza ila hao madereva wa bodaboda,bajaji na daladala wanastahili makofi si kwa wanajeshi tu.

Wenye dhamana wanajali pesa/faini tu na si kingine kwa hao madereva wasiojitambua na abiria wanasubiri itokee ajali ndiyo walalamikie mwendo wa dereva.
 
Wanaume wa dar wanazingua sana,uwakute sasa na vibukta vyao asubuhi wanakimbia pembezoni mwa barabara,na vifua kama njiwa,utadhani wapo serious [emoji3][emoji3],gari zima wameshindwa kumkalisha huyo mpuuzi.
Nyie mpaka askari wa wanyapori wanawadhalilisha na ng'ombe zenu wachukua ndio unakuja kuongelea wanaume wa Dar.
 
Kama CDF anapita humu aangalie namna ya kubadili vigezo vya kitaaluma kwa watu wanaojiunga na Jeshi.

Mtu akiwa amefeli ana D zake mbili anakimbilia JKT kisha JWTZ matokeo yake anafanya kazi akichoka anatafuta fani ya udereva anakuwa dereva wa magari ya jeshi anakuja barabarani na akili za kijinga ndo matokeo yake anapiga dereva raia kwa kosa la barabarani bila kujali usalama wa watu ndani ya gari.

Likely ni private au Cpl hawezi kuwa kafika Sgt, mambo ya kijinga kabisa.


Hilo gari la jeshi lina namba watamjua ni askari gani wamshughulikie arudi kwao kijijini kuwa mlinzi wa maduka binafsi
 
Unakuta mtaani Raia anajitapa mimi mwanajeshi awezi nifanya chochote..

Ndio hayo hayo kwenye daladala anafanya ubabe anajibu hivyo.. mwanajeshi ni mtu mstaarabu sana hawezi kukurupuka kufanya maamuzi kama hujamkosea..

Hapo kuna dereva kufanya makosa na bado kumjibu shombo.. tangu tukio la majaji la mwanajeshi MUNA.. raia hamjajifunza tu..?
 
Back
Top Bottom