TANZIA MwanaJF Dada Niah amefariki dunia akipatiwa matibabu Dodoma General hospital

TANZIA MwanaJF Dada Niah amefariki dunia akipatiwa matibabu Dodoma General hospital

Misimamo ya kidini na kiimani ni mingi mno katika huu ulimwengu, sioni haja ya kuileta kwenye huu uzi tena unaomuhusu mtu ambae hatupo nae na ikiwa JF ni jukwaa huru kila mmoja wenu anaweza fungua uzi wake na kuelezea namna anavyoamini yeye kama yeye.
 
Screenshot_20240821-145457~2.jpg
 
Nimepita kwenye mitaa ya wakristo, msiba umefana kweli kwa maneno ya imani na matumaini juu ya kifo cha ndugu yao lengo ni kujitia moyo kwamba wanakokwenda ni mbinguni

Apumzike kwa amani,
Rip,
Na majirani zao pia walikuwepo,
inna lilah,
Ndugu zanguni kwenye kipindi cha majonzi kama hiki ndio kipindi cha kuwekana wazi,
Ni kwanini mamalia pekee anayeenda mbinguni baada kufa ni huyu anayezaa kwa kujificha, anakula kistaarabu, anavaa nguo, ana mwili na roho, vipi kuhusu ng'ombe, mbuzi, au kondoo na wao wanaenda wapi?.

Turudi kwenye asili ndugu zanguni, hii miungu ya kizungu inayowapeleka mbinguni baada ya kufa ni ya kizushi,

Poleni kwa msiba, aliyekufa amekufa, hana anakokwenda, mnaishi leo lakini mnakubali lugha ya imani na matumaini inalaghai fahamu za akili,

Apumzike kwa amani, wapi modernist? Do you guys have common senses?!!
 
Kwa majonzi makubwa nachukua nafasi hii kuwatangazia ya kwamba dada mama na ndugu yetu mwanaJamiiForums mwenzetu dada niah ametwaliwa kutoka maisha haya..! Amefariki juzi tarehe 2 Dodoma General hospital alikokuwa akipatiwa matibabu

Msiba uko nyumbani kwake Dodoma na ndugu yetu Mwifwa yuko huko hivyo atatujuza zaidi
Mara ya mwisho kabla ya kurejea nchini alikuwa Lebanon Beirut ambapo mumewe ni mwambata wa ubalozi kule.. Mumewe si raia wa Tanzania

Mazishi ni kesho mjini Bukoba ambako ndiko asili yake
Nilimfahamu mwaka 2017 hapa JF na baadae nje ya JF.. Alikuwa ni mama mwenye upendo mkuu ushauri mwanana asiye na majivuno na aliyekuwa anaisaidia bila kubagua

Hakuwa mshiriki sana kwa maana ya kuandika lakini alikuwa msomaji mzuri sana wa karibia kila kilichokuwa kikiandikwa hapa

Alikuwa dada na rafiki mwema kwangu. Nitamkumbuka daima

Kwa ruhusa maalum naweka picha yake ya msibani hapa.

Pumzika kwa amani dada yangu niah 😪

View attachment 3115403
Alale anapostahili
 
Pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu. Mungu Mwema awe faraja kwao!
 
Back
Top Bottom