TANZIA MwanaJF mwenzetu Erick Kalemela amefariki dunia

TANZIA MwanaJF mwenzetu Erick Kalemela amefariki dunia

Ninayo masikitiko makubwa kuwataarifu msiba wa mwenzetu Erick Kalemela uliotokea nchini India jana tar 23 Mei 2022 saa 3 asubuhi majira ya India, alipokuwa anapokea matibabu.

Mwili unatarajiwa kuwasili siku ya Alhamisi kwa ajili ya taratibu za mazishi yatakayofanyika kwao Kahama.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Pole sana kwa ndugu kuondekewa na mpendwa wao
 
Huwa nikikutana na tangazo la namna hii, huwa nawaza sana. Hivi sisi ambao hatuna watu au mtu ambaye anatufahamu kwa majina yetu haya ya bandia hapa JF, tukifa, itakuwa kimya tu, kama vile tumeamua kuwa kimya tu, kama Bia yetu alivyoamua kuwa kimyaaaaa!
Bia yetu sijui kapotelea wapi alikuwa anaoneka sana enzi za JPM
 
Mungu akurehemu na kukupokea mwanae mpendwa Erick. Pumzika kwa amani mpita njia mwenzetu, nasi muda si mrefu njia yetu itafika kikomo tuungane nawe huko mapumzikoni kwa BABA.

NB. Tujitahidi kua na michango/comments zisizo na machukizo kwa wengine..Mtu akifa humu ndio tunaanza kuchunguza aina ya michango yake. Ni wazo langu tu lakini
 
Back
Top Bottom