Mwanamke ajeruhiwa kwa risasi za polisi maeneo ya Sinza Dar es salaam

Mwanamke ajeruhiwa kwa risasi za polisi maeneo ya Sinza Dar es salaam

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
Mwanamke aitwaye Mariam mkazi wa Sinza Lion Dar es Salaam, amejeruhiwa kwa kupigwa risasi maeneo ya begani katika harakati za Polisi kuwatuliza raia wenye hasira kali waliokuwa wanataka kumpiga mwizi aliyekwapua simu kwenye bodaboda majira ya saa 12:00 asubuhi ya leo Mei 20, 2022

Kwa maelezo ya mashuhuda wa tukio hilo, wanadai baada mwizi huyo kukwapua simu alikimbilia nyumba iliyokuwa jirani na baadaye kidogo walitokea maaskari waliomwokoa mwizi lakini katika harakati za kuwatuliza raia, inadaiwa walifyatua risasi iliyomjeruhi raia huyo ambaye amekimbizwa hospitali

Chanzo: EATV

SOMA PIA:

Muliro azungumzia raia aliyejeruhiwa kwa risasi​

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amethibitisha tukio la mwanamke kujeruhiwa kwa risasi leo maeneo ya Sinza Lion, na kusema imempata kwa bahati mbaya baada ya Askari kufyatua risasi juu kwa lengo la kuwatawanya wananchi waliokuwa wanampiga mwizi wa simu.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 20, 2022, wakati akizungumza na East Africa TV & EA Radio Digital, ili kutoa ufafanuzi wa madai yaliyotolewa na mashuhuda wa tukio hilo kwa kusema kwamba mwanamke huyo aitwaye Mariam amejeruhiwa na polisi.

"Ni kweli tukio hilo limetokea na jeshi linaendelea kulifuatilia, lakini ni kwamba askari walifyatua risasi juu katika juhudi za kumuokoa mtuhumiwa na kwa bahati mbaya kuna mwanamke amejeruhiwa ingawa anaendelea vizuri," amesema Kamanda Muliro.

Aidha Kamanda Muliro akimzungumzia mwizi huyo amesema, "Huyo mtuhumiwa hatujamtambua kwa sababu hajaweza kuongea, alikuwa tayari amepigwa, hawezi kuongea, hivyo tunalichunguza tukio hilo".
 
Hili la "risasi kipigwa juu halafu inampata mtu begani' sijawahi kulielewa.

Imagine risasi inaenda juu then inamlenga mtu begani, maana yake ni sentimita chache ingempiga kifuani, shingoni au mgongoni, ambazo ni sehemu hatari sana.
 
Risasi inapigwa vipi juu halafu impate aliyejeruhiwa? huu uzembe wa hawa askari wetu sijui utakwisha lini, na ajabu kamanda wa polisi anasema simple tu, ni bahati mbaya.

Nitashangaa kama mpaka leo bado kuna mtu asiejua marehemu Akwilina alipigwa risasi na nani. RIP.

Bahati nzuri hiyo risasi haijaua, kama ingeua tungesikia story zile zile toka kwa kamanda wa polisi, ilipigwa juu, ikarudi chini ikakata kona ikampata marehemu.
 
SaSa unaokoa jambaz halfu unaua raia mwema, si upuuzi huo
mahakama ndiyo imepewa mamlaka ya kuhukumu mkuu,wao as long wamemtia ngeu kidogo ila polisi wakafika wangemwacha tu waondoke naye.
 
Haki inapatikana kwa Mungu tuu..Duniani hakuna haki...
Imeisha kiivyo hilo swala la kufyatua risasi hewani na kuto kumjeruhi mtu asee
 
Ninavyojua mimi kisheria huyo mwizi ndiye atagewa kesi ya kumjeruhi Mariam
 
Risasi inapigwa vipi juu halafu impate aliyejeruhiwa? huu uzembe wa hawa askari wetu sijui utakwisha lini, na ajabu kamanda wa polisi anasema simple tu, ni bahati mbaya.

Nitashangaa kama mpaka leo bado kuna mtu asiejua marehemu Akwilina alipigwa risasi na nani. RIP.

Bahati nzuri hiyo risasi haijaua, kama ingeua tungesikia story zile zile toka kwa kamanda wa polisi, ilipigwa juu, ikarudi chini ikakata kona ikampata marehemu.
Inasikitisha sana. Ndio Askari wetu hao
 
Kama si bahati mbaya polisi aliaga kwake kwenda kupiga bega la Mwanamke?
Je Sinza inamajengo ya chini tupu? Je hakuna Watu warefu kuliko Polisi?
Je mkimzingira Polisi hata akipiga juu unafikiri waliomzunguka watakuwa katika hali gani?
Je umefika eneo la tukio au ndiyo kutoa tuhuma tu ?
 
Sasa unaokoa jambazi halafu unaua raia mwema, si upuuzi huo
Hao ndio polisi wa Siro.
Picha ninayopata ni kwamba polisi wanatetea vibaka.
Halafu watu wa Sinza goi goi Sana, mpaka polisi wanakuja shughuli ndogo Kama hiyo mlikua bado hamjamaliza.?
 
Back
Top Bottom