Mwanamke ajeruhiwa kwa risasi za polisi maeneo ya Sinza Dar es salaam

Loh
Polisi polisi polisi.

Mbona wanyama hivi?
 
Pole dada yangu jamani.
 
Negligence

Halafu utakuta huyo askari alofanya hivyo anaachwa tu na ishu kupotezewa.


RIP Akwilina
 
Ya marehemu AKWILINA yanataka kujirudia tena risasi imepigwa juu lakn imempata mtu begani

Muliro jumanne maelezo yako hayatoshelezi

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Inakuwaje polisi wanatumia risasi za moto katika tukio dogo kama hilo? mitaala inayotumika ktk mafunzo ya upolisi ipitiwe tena maana jeshi limejaaa mananga watu
 
uzembe kwa maana ipi???

kapigwa sehemi isiyo sahihi au alitakiwa auwawe kabisa dada mariamu??
Hivi sayansi ya fizikia ndio isemavyo? Kwamba risasi inapigwa juu halafu inampata mtu begani.
Ni ujinga uliopitiliza badala ya mkuu wao kusema askari amefanya kosa la kutumia silaha . Unatafuta kivuli.
Hivi huyo askari anasifa za kuwa kweli askari? Hawa ndio wanaotegemewa kuzua uhalifu. Kweli?
 
Naiona hadithi ya binti Akwilina inajirudia.Risasi ilipigwa juu.Juu wapi?Ghorofani? Kwenye mti?Angani?Juu.Juu wapi?
 
Hujayasikia ya marehemu Akwilina wewe?
Askari polisi wakiona kundi la watu ni aidha wanachanganyikiwa au wanatafuta sifa.Na pengine wanakuwa wanaongozwa na akili za ukevi tu.Ni hali imeshindikana vipi hadi urushe risasi?Huwa wanafikiria madhila yanayoweza kutokea kwa wananchi au hata wao wenyewe?Full kutetemeka ndiyo wanafanya mahovyohovyo.
 
uzembe kwa maana ipi???

kapigwa sehemi isiyo sahihi au alitakiwa auwawe kabisa dada mariamu??
Uzembe ni jambo lolote kulitenda kinyume na utaratibu.

Huo ni uzembe wa hali ya juu kuweza kumfikisha mhusika kwenye mahakama za kinidhamu!

Hauwezi hata siku moja ukamjeruhi mtu, eti ukadai ni bahati mbaya wakati askari mhusika alishapata mafunzo "bora" namna ya ushikaji na utumiaji sahihi wa silaha.

Kwenda kinyume na hapo ni uzembe wa kiwango cha lami.

Nimemshangaa Rpc kuanza kukinga kifua kwa askari mzembe!

Jeshini hakuna bahati mbaya kwa kufanya kosa lolote lile.

Yakiishia kwenye meza za media bila mhusika kufunguliwa mashitaka na kufikishwa mahakamani, hata huyo mama mjeruhiwa, kupata stahiki zake za fidia itakuwa ni vigumu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…