Mwanamke ajiua na wanawe (4) kwa sumu kisa mke mwenza kajengewa nyumba

Mwanamke ajiua na wanawe (4) kwa sumu kisa mke mwenza kajengewa nyumba

Upumbavu na tamaa za watu wazima wawili umeenda kugharimu uhai wa watoto wasiokuwa na hatia.
Makobazi bwana hivi hamuwezi kuishi na mke mmoja mnataka hadi mmpite mudi kwa wingi wa viburudisho


Case za ndoa usizihukumu na mambo ya dini....yule alimpiga mke risasi mwanza....yule aliemchoma mkewe na gunia za mkaa,ilikuwa dini au wivu
 
Katika tukio la kusikitisha na kuzua maswali mengi kwa jamii, mwanamke mmoja aitwaye Kangw’a Tungu Mahigi (25), mkazi wa Kijiji cha Lugubu, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, amefariki dunia kwa kunywa sumu aina ya Ruruka 80 WDG, inayotumika kuua viwavi jeshi vinyamizi — huku pia akiwanywesha watoto wake wanne, ambao wote wamepoteza maisha

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia, ambapo marehemu alikuwa mke mkubwa katika ndoa ya ‘wake wengi’, na alikuwa akilalamika kunyimwa huduma sawa na mke mdogo, ikiwemo mume wake kujenga nyumba kwa mke mdogo huku yeye akikosa makazi bora

Majina ya watoto waliofariki ni Sengi James (miaka 8), Simon James (miaka 6), Elisha James (miaka 3) na Kashinje James (miezi 7)

Kamanda Abwao amesema kuwa mume wa marehemu anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo, ikiwa ni pamoja na nafasi yake katika muktadha wa mgogoro wa kifamilia uliokuwepo kabla ya tukio


Mume hana kosa la jinai.

Na tangu lini polisi wakawa na huruma kiasi cha kuingilia migogoro ya kifamilia?
 
Amekosa uvumilivu
Inaonyesha alikuwa ni mwanamke mtata sana jamaa sasa hivi atafurahia ndoa
 
iyo ruruka ni hatari, niliwahi pulizia viwavi jeshi kwenye mahindi nikasahau kunawa nikala ivo ivo, nilikimbiza mwenge balaaa
 
Back
Top Bottom