Mwanamke ajiua na wanawe (4) kwa sumu kisa mke mwenza kajengewa nyumba

Mwanamke ajiua na wanawe (4) kwa sumu kisa mke mwenza kajengewa nyumba

Huyo jamaa afungwe!.. mwanamke ana miaka 25 ameshamzalisha watoto wanne alafu anaoa tena mbele ya macho ya huyo mke mkubwa? Afungwe
Kuna Sheria inakataza kuoa mke wa pili,wa tatu, wa nne au hata 10?
Ulisema afungwe ni mawazo yako, lakini kwa Sheria gani?

Inasikitisha Sana,lakini Sheria haipo hivyo...
 
Katika tukio la kusikitisha na kuzua maswali mengi kwa jamii, mwanamke mmoja aitwaye Kangw’a Tungu Mahigi (25), mkazi wa Kijiji cha Lugubu, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, amefariki dunia kwa kunywa sumu aina ya Ruruka 80 WDG, inayotumika kuua viwavi jeshi vinyamizi — huku pia akiwanywesha watoto wake wanne, ambao wote wamepoteza maisha

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia, ambapo marehemu alikuwa mke mkubwa katika ndoa ya ‘wake wengi’, na alikuwa akilalamika kunyimwa huduma sawa na mke mdogo, ikiwemo mume wake kujenga nyumba kwa mke mdogo huku yeye akikosa makazi bora

Majina ya watoto waliofariki ni Sengi James (miaka 8), Simon James (miaka 6), Elisha James (miaka 3) na Kashinje James (miezi 7)

Kamanda Abwao amesema kuwa mume wa marehemu anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo, ikiwa ni pamoja na nafasi yake katika muktadha wa mgogoro wa kifamilia uliokuwepo kabla ya tukio


Mwanaume mwenzangu umezingua mkuu Tena sana!!!

Huwa hatujengei mdogo wakati mkubwa hana nyumba!

Japo maamuzi ya mkeo mkubwa ni ya kijinga!Nyumba Ina matter sana kwenye maisha ya Hawa viumbe!japo wakishajengewa tu na kupewa uhakika wa life sarakasi zinaanza!!

Elewa sarakasi !Mimi nimeziona chini ya jua!!
 
Kuna Sheria inakataza kuoa mke wa pili,wa tatu, wa nne au hata 10?
Ulisema afungwe ni mawazo yako, lakini kwa Sheria gani?

Inasikitisha Sana,lakini Sheria haipo hivyo...
Wiki ijayo naenda kuona kifaa ambacho Mzee anaona kinafaa kubebwa ni baada ya huyu makelele kuzidi baada ya kuwa na kaya niliojenga plus uhakika wa kipato!!
 
Hiyo nguvu angeitumia pahala pengine katika kuleta maendeleo. That is a wastage of energy
 
Katika tukio la kusikitisha na kuzua maswali mengi kwa jamii, mwanamke mmoja aitwaye Kangw’a Tungu Mahigi (25), mkazi wa Kijiji cha Lugubu, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, amefariki dunia kwa kunywa sumu aina ya Ruruka 80 WDG, inayotumika kuua viwavi jeshi vinyamizi — huku pia akiwanywesha watoto wake wanne, ambao wote wamepoteza maisha

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia, ambapo marehemu alikuwa mke mkubwa katika ndoa ya ‘wake wengi’, na alikuwa akilalamika kunyimwa huduma sawa na mke mdogo, ikiwemo mume wake kujenga nyumba kwa mke mdogo huku yeye akikosa makazi bora

Majina ya watoto waliofariki ni Sengi James (miaka 8), Simon James (miaka 6), Elisha James (miaka 3) na Kashinje James (miezi 7)

Kamanda Abwao amesema kuwa mume wa marehemu anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo, ikiwa ni pamoja na nafasi yake katika muktadha wa mgogoro wa kifamilia uliokuwepo kabla ya tukio


Ila wasukuma wana akili za kipimbi sana. Sasa si angejiua yeye mwenyewe huyu mpuuzi awaache watoto waishi? Watoto wanahusikaje na hayo mawivu yake?
 
Nilikua mtoto wa around 3 - 4 years old, sikua na kumbukumbu nzuri zaidi ya yeye Mama kusema aliwahi kutunywesha Sumu wanae wote, na akasema sababu Kwa Nini....!?

So sikuwahi kumchukia Wala sikuweka kitu Moyoni, tu mpaka kesho Huwa inanifikirisha.
Daah noma sana, kwa mimi na akili zangu za saivi sijui ningewaza nini juu yake.
 
Mama yangu mwenyewe alifanya hivyo hivyo kwangu na Kwa Ndugu zangu tukiwa na Umri kama huo, Kwa Idadi kama hiyo....!

Bahati nzuri kwetu hakuna aliyepoteza Maisha zaidi ya kulazwa Hospital.........!

Fear Women....!!!
Duh
 
Mwanaume anasemaje?.Maana naona wengi mnamlaumu mwanaume kwakuoa mke mwingine lakini je mnajua sababu iliyopelekea jamaa akaoa mwingine.Kama mwanamke kafanya maamuzi yakijinga yakujiua na watoto wadogo hivyo unadhani kipindi cha uhai wake alikua ni mtu mwenye roho mbaya kiasi gani?.Inawezekana jamaa alipitia mengi ikabidi akatafute faraja kwingine.Mimi nahisi tatizo lilianzia kwahuyo mwanamke mwenyewe ila sema wanaume wengi hawasemagi utamuona tu kajikataa kajishikisha kwa mchepuko akiona pako vizuri anahalalisha.
 
Afadhali angejiua mke mwenza kuteuliwa DC au hata raisi jamani, nyumba tu!
Halafu nyumba zenyewe sasa!!..napajua vizuri huko,ni igunga ndani bush,kuna fala huko namdai hela ya nyanya ndoo sita mwaka wa saba huu hajalipa
 
Hatari sana arhari za ndoa za utotoni. 25 watoto wanne aiseeeeeee
 
Inasikitisha sana kwa kukatili maisha ya watoto wasio na hatia.
 
Mama yangu mwenyewe alifanya hivyo hivyo kwangu na Kwa Ndugu zangu tukiwa na Umri kama huo, Kwa Idadi kama hiyo....!

Bahati nzuri kwetu hakuna aliyepoteza Maisha zaidi ya kulazwa Hospital.........!

Fear Women....!!!
Doh
 
Si jambo zuri alilolifanya ila kiukweli mimi siwezi mlaumu sababu sijui alipitia yapi hadi kufikia maamuzi ya kujitoa uhai yeye na watoto wake. Unaambiwa jambo hadi likufike ndio utaelewa.

Wapumzike kwa amani.
 
Back
Top Bottom