Mwanamke ajiua na wanawe (4) kwa sumu kisa mke mwenza kajengewa nyumba

Katika tukio la kusikitisha na kuzua maswali mengi kwa jamii, mwanamke mmoja aitwaye Kangw’a Tungu Mahigi (25), mkazi wa Kijiji cha Lugubu, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, amefariki dunia kwa kunywa sumu aina ya Ruruka 80 WDG, inayotumika kuua viwavi jeshi vinyamizi — huku pia akiwanywesha watoto wake wanne, ambao wote wamepoteza maisha

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia, ambapo marehemu alikuwa mke mkubwa katika ndoa ya ‘wake wengi’, na alikuwa akilalamika kunyimwa huduma sawa na mke mdogo, ikiwemo mume wake kujenga nyumba kwa mke mdogo huku yeye akikosa makazi bora

Majina ya watoto waliofariki ni Sengi James (miaka 8), Simon James (miaka 6), Elisha James (miaka 3) na Kashinje James (miezi 7)

Kamanda Abwao amesema kuwa mume wa marehemu anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo, ikiwa ni pamoja na nafasi yake katika muktadha wa mgogoro wa kifamilia uliokuwepo kabla ya tukio

So sad
 
Wanaume huwa wanachukulia poa lakini hamna ndoa zinakuwaga na migogoro kama ndoa za wake wengi.

Sababu wengi hawawatimizii wanawake kwa usawa.
Ila ndoa za wake wengi. Wanaume wengi wanaoa kama kumkomoa mke mkubwa au kumuonesha kama “yeye mwanaume” anaweza akapat mtu mwengine.
 
Duh🤔 huyu mama alichukua uamuzi mgumu Sana kujiangamiza yeye pamoja na watoto wote.

Mume alinusurika Tu hapa kwa sababu hiyo sumu ingemhusu na yeye kama angekuwa karibu
 
Wanaume huwa wanachukulia poa lakini hamna ndoa zinakuwaga na migogoro kama ndoa za wake wengi.

Sababu wengi hawawatimizii wanawake kwa usawa.
Kwani wanawake hamuwezi kujitimizia ? Uvivu wenu ndio changamoto
 
Katika tukio la kusikitisha na kuzua maswali mengi kwa jamii, mwanamke mmoja aitwaye Kangw’a Tungu Mahigi (25), mkazi wa Kijiji cha Lugubu, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, amefariki dunia kwa kunywa sumu aina ya Ruruka 80 WDG, inayotumika kuua viwavi jeshi vinyamizi — huku pia akiwanywesha watoto wake wanne, ambao wote wamepoteza maisha

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia, ambapo marehemu alikuwa mke mkubwa katika ndoa ya ‘wake wengi’, na alikuwa akilalamika kunyimwa huduma sawa na mke mdogo, ikiwemo mume wake kujenga nyumba kwa mke mdogo huku yeye akikosa makazi bora

Majina ya watoto waliofariki ni Sengi James (miaka 8), Simon James (miaka 6), Elisha James (miaka 3) na Kashinje James (miezi 7)

Kamanda Abwao amesema kuwa mume wa marehemu anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo, ikiwa ni pamoja na nafasi yake katika muktadha wa mgogoro wa kifamilia uliokuwepo kabla ya tukio

Upumbavu tu uchunguzi upi? Wamwachie jamaa aendelee na maisha wanavyojua kushadadia kesi zisizo na umaana. Huyo dada labda hakujua kuchekecha vizuri angevuta subra hao watoto alioua labda ndo wangemjenge nyumba
 
Mwanaume asiyewajibika hana tofauti na zigo la mavi, hao watoto itakuwa walikuwa na maisha magumu sana kuliko kuwaacha nyuma bi mkubwa kaona aende nao.

Hapa ndio ndoa ya mke mmoja inapochukua points 3 za mezani
 
Inategemea sana. Mimi ni product ya ndoa ya wake wawili mamangu aliolewa kama mjane mke wa pili akiwa na watoto watatu kabla ndio nikapatikana mimi. Tuliishi pamoja na mke mkubwa ambae alikua na watoto 5 tayari. Nililelewa na wamama wawili kwenye nyumba moja vizuri kabisa.
Hao ni wale waliokuwa wanaishi pamoja ndo mana Babako akawa anafanya usawa.

Kwa wale wenyw wake wanaokaa mbali mbali ni wachache sana wanaofanya usawa wengi pale penzi lilipo na nguvu ndo atafanya kwa juhudi zote.
 
Back
Top Bottom