Huu uzi ni ukweli 100%.
Kuna workshop fulani niliwahi kufanya kazi, sehemu ambayo watu walitembeza vitu mbalimbali kuuza. Kuna manzi moja kama 22yrs alikuwa anauza juisi mida ya mchana kila siku.
Yule manzi alikuwa mzuri wa sura, umbo, sauti, na kila siku alipendeza tofauti, mtu muongeaji na wa kujichanganya na watu. Kwa kuwa pale workshop wafanyakazi wengi tulikuwa wanaume tena bachelors, wanawake walivalia namna ambavyo waliamini watateka attention ya wanaume ili kurahisisha biashara na udangaji.
Ikawa kila yule manzi muuza juisi anapofika masela wanachanganyikiwa balaa, wataanza kumwita kwa jina, kila mmoja anataka kuwa wa kwanza kuhudumiwa juisi, mwingine hata change hadai, kila mtu anataka amsemeshe yaani shobo mwanzo mwisho.
Lakini Mimi nilimuona wa kawaida tu, wala sikuwahi kupata hamu ya kununua juisi yake. Baada ya muda alishtuka watu wote pale workshop walishawahi kununua juisi kwake na kumshobokea isipokuwa Mimi tu(wengine hawakugundua).
Mara siku moja baada ya kuuzia wengine akaja sehemu nilipokuwa;
Yeye: Kaka mambo?
Mimi: Shwari,
Yeye: juisi?
Mimi: Asante.
Ikawa kila siku lazima ajipitishe mbele yangu kunisalimia na kuuliza kama nahitaji juisi lakini tofauti na salamu pamoja na asante ya kukataaa juisi sikuwa na story ya pili na yeye. Kilichomvuruga zaidi mara kibao amewahi kunikuta na wanawake wengine. Ilifika mahali akimaliza kuuza juisi anakaa sehemu ya mbali kidogo ananipiga chabo halafu kama ana mawazo.
Wanawake ni viumbe wa ajabu sana, ukiwaheshimu wanakudharau na ukiwadharau wanakuheshimu. Hata mkeo ukimuona kama celebrity yeye atakuona kama shabiki. Kanuni ni kuwachokonoa self esteem. Bila kubabaishwa na kiwango chake cha uzuri, mchukulie kama vile .......... Then utaona response yake kwako.