KWELI Mwanamke akiwa hedhi, haruhusiwi kuingia msitu wa Nyumbanitu

KWELI Mwanamke akiwa hedhi, haruhusiwi kuingia msitu wa Nyumbanitu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Hii dunia ina vitu vya ajabu sana na vya kushangaza. Kuna historia baadhi unaweza unaweza kushangazwa nazo mojawapo ikiwa hii niliyopata kusimuliwa.

Msitu wa Nyumbanitu una historia nyingi za kushangaza. Msitu huu upo katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoa wa Njombe. Msitu huu nimepata kusimuliwa kuwa endapo mwanamke atakuwa kwenye siku zake basi hatoruhusiwa kuingia katika msitu huo, Ikiwa atakaidi basi akiingia kwenye huo msitu ndio utakuwa mwisho wake wa kuonekana maana atapotea mazima.

Nadhani hili jambo mnaona linavyostaajibisha. Najiuliza huu msitu una nguvu na miujiza gani mpaka uweze kuwatendea hivyo dada zetu.

Msitu.jpg
 
Tunachokijua
Nyumbanitu na msitu unaopatikana katika kijiji cha Mlevela, kata ya Mdandu, Wilaya ya Wanging'ombe, ni kilomita 15 kutoka Njombe mjini.

Jina "Nyumbanitu" ni muunganiko wa maneno mawili; nyumba na nitu. Neno "Nitu" manaa yake ni Giza au Nyeusi. Hivyo Nyumbanitu maana yake ni nyumba yenye giza au nyumba nyeusi.

Maajabu yake
Nyumbanitu si nyumba, kama lilivyo neno lenyewe, bali ni msitu mdogo, wenye ukubwa wa hekta moja na nusu (1.5) tu, lakini una mambo ya kustaajabisha.

Kuna watu ambao huenda Nyumbanitu kuomba mizimu iwape baraka katika mambo yao. Kuna ambao huenda kuchuma dawa, wengine huenda kujifunza mila na desturi za mahali hapo ambazo pengine zinahusiana na ushirikina n.k.

Maajabu ya msitu huo ni kuku weusi wenye midomo myekundu ambao wahifadhi wanasema hawazeeki, hawafugwi na wala hawaliwi.

1601123024765-png.1581432

Mfano wa kuku wanaopatikana kwenye msitu huo
Kuku hao huonekana kwa wingi wakati wa mavuno na inapofika masika, hawaonekani tena.

Pia, inasemekana huwa kuna ng’ombe na kondoo ambao huingia kwa msimu na rangi ya wanyama wanaongia kwenye msitu huo ni nyeusi. Inadaiwa kuwa mtu anayeiba kuku hawa anaweza kugeuka kuwa kichaa.

Septemba 2022, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iliutangaza rasmi msitu huu kuwa miongoni mwa vivutio muhimu vya utalii na utamaduni Tanzania.

Wanawake wenye hedhi kuingia kwenye msitu huo
Kabla ya kuingia kwenye msitu huo, waangalizi wa msitu hutoa tangazo la kuwataka wanawake walio katika siku zao, yaani kwenye hedhi, kutothubutu kuingia.

“Ni mwiko na ikiwa utajidanganya kufanya hivyo, basi miaka yako yote utabaki hivyo hivyo, hakuna dawa ya kutibu”

Maneno haya yanathibitishwa na mwandishi mmoja wa gazeti la Mwananchi aliyetembelea msitu huo kupitia andiko lililochapishwa na gazeti hilo Agosti 28, 2016.

Aidha, Septemba 26, 2020, Mtumiaji wa JamiiForums aliwahi pia kuweka andiko lenye ujumbe unaofanana na huu. Alisema;

Si ruhusa Kwa wanawake walio katika siku zao, yaani kwenye hedhi kuingia ndani ya msitu huo. Ni mwiko kabisa, na ikiwa mwanamke atajidanganya kufanya hivyo, basi miaka yake yote atabaki akitokwa na damu ya hedhi bila ukomo na hakuna dawa ya kumtibu.

Wanawake wajawazito pia hawaruhusiwi kuingia. Marufuku hii imeandikwa kwenye ubao maalumu nje kabisa ya msitu huo mdogo. Ili kuhakikisha kuwa wageni (watalii) hawakiuki marufuku hiyo, mwenyeji huirudia marufuku hiyo kwa mdomo ili kutilia mkazo.


Sharti lingine kabla ya kuingia msituni humo ni kuvua viatu, kofia na vilemba. Baada ya kufuata taratibu zote, mwenyeji huomba ruhusa ya kuingia msituni kwa kuongea maneno ya kibena.

Mtu yeyote anayepuuzia masharti haya hupatwa na kitu kibaya, ikiwemo kupotelea msituni humo

Julius Msigwa, mwongozaji wa watu wanaotembelea msitu huo akifanya mahojiano na Gazeti la Mwananchi anasema simulizi za ajabu za msitu huu na kuwapo kwa imani za kishirikina, ziliwafanya baadhi ya waumini wa Kikristo wanaojulikana kama walokole vijiji vya jirani kuamua kuingia ili kufanya maombi.

“Hili si tukio la siku nyingi, hawa watu walitaka kuja kukemea mashetani ndani ya msitu. Siku ya maombi yao, walokole hao walijikusanya na kuanza safari hadi msituni. Walipofika waliamua kuingia bila kukutana na mwenyeji yoyote wala kufuata mila na desturi za kuingia msituni ili kutoka salama.

“Walikuja moja kwa moja hadi kwenye mti huu, walianza kukemea na kuvuruga utaratibu wa hivi vifaa vya matambiko,” anasema.


Julius anasema watu hao waliendelea na maombi kwa siku nzima, ilipoisha wakataka kuanza safari ya kutoka ndani ya msitu.

Julius anasema hakukuwa na njia ya kuwawezesha kutoka ndani ya msitu.

“Walijikuta wakiendelea kupiga kelele, wakizunguka msitu mzima lakini hakukuwa na msaada kwa wao kutoka"

"Watu waliokuwa wakipita nje ya msitu walisikia kelele, hata hivyo hawakuwa na msaada wowote kwani hata wao hawawezi kuingia bila kufuata taratibu"

Ushahidi wa madai ya kufanya hedhi isikome
JamiiForums haijapata uthibitisho wa moja kwa moja kutoka kwa mwanamke aliyewahi kupatwa na tatizo hili, lakini imezungumza na Mpokezi wa Wageni na Kiongozi wa Kimila katika Msitu wa Nyumbanitu, Julias Vangamel, anaelezea:

Nyumbanitu ni Msitu wa Mila, sehemu zote zenye Misitu ya Kimila kuna taratibu na miiko yake, hivyo ni kweli kuwa sehemu ya miiko iliyopo ni kuwa Mwanamke hatakiwi kuingia akiwa katika siku zake za hedhi.

Mila zikishawekwa lazima zisuatwe kwa kuwa tofauti na hapo kutakuwa na madhara yake.

Mwanamke akiingia kwenye pango lililopo katika Msitu wa Nyumbanitu akiwa kwenye mzunguko wake wa hedhi anaweza kujikuta anaendelea kuwa hivyo siku zote, yaani mzunguko wa hedhi ambao hauna ukomo.

Madhara ya aina hiyo yamewahi kutokea miaka ya nyuma, ndio maana likawekwa hilo angalizo, kwa miaka ya hivi karibuni haijawahi kutokea.

Wanawake wakifika hapa kwa ajili ya kuingia pangoni wanajulishwa masharti ya kimila ikiwemo hilo na wanalizingatia.


Uthibitisho huu hautofautiani na maelezo yaliyofafanuliwa awali kutoka kwenye vyanzo mbalimbali, yote kwa pamoja yakiweka ukweli wa msingi wa madai haya.

Aidha, Vangamel ameiambia JamiiForums kuwa Agosti 7, 2023, Wanafunzi zaidi ya 200 kutoka shule mbalimbali walitembelea msitu huo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali.
Kuna kuzimu mbili ndogo na kubwa.
Ndogo ni hizi zilizopo Duniani tumefungwa macho hatuzioni isipokuwa wenye jicho la Tatu .
Haya ni magereza wamefungwa mateka kumbuka hakuna mwanadamu yeyeto mwenye uwezo wa kuua mtu au kutoa uhai wa mtu isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee hata mchawi Hana uwezo huo isipokuwa mchawi anachofanya ni kiini macho kupofusha macho.

Mchawi anao uwezo wa kumchukua mtu yeyeto mwenye dhambi amtakae na kumpeleka kwenye magereza zao maisha yaendelee wakiwatumikisha kazi,kuwala nk.
Unakuwa upo Duniani uoni na wanadamu isipokuwa Mungu anakuona, wachawi,baadhi ya wanyama wanakuona, mtoto mdogo asiyeongea anakuona,vichaa , waganga nk Wana uwezo huo wa kuona.
Pana watu wanaishi Duniani na kuzimu hizi za Duniani zikiwemo hizo nyumba nitu, Gamboshi, Ngende,ziwa Victoria, Tanganyika,nyasa,manyoni singida,Mbeya,chini ya mlima Kilimanjaro nk.Mfano wote wale wa Mv Bukoba wao wapo chini ya ziwa kuna mji na maisha yanaendelea.
Kama una urafiki na mganga yeyeto atakuthibitishia Siri hii.
Pana watu mchana wapo Duniani Usiku wanarudi kuzimu.Mitume na manabii wa uongo wasanii wakubwa,wanasiasa wakubwa, matajiri wanaijua Siri hii na codes za kufungua ili kuingia huko kwenye vikao vyao.
Kuzimu kubwa hii ni makao ya shetani na malaika zake hii ipo nje ya Dunia Ina vyumba au magereza 351 gerezani moja ni sawa na bara moja la Africa kila dhambi na gereza lake.
Ukifa kuzimu ndogo unaenda kubwa ukifa dhambini Duniani unaenda kuzimu kubwa.
Mungu na shetani na malaika zao ndio wenye kuweza kuingia kuzimu kubwa.
Kwa wanadamu ni wale wenye level ya juu ya ushetani yaan wale waliomaliza level ya kuwa mchawi, mchawi akipanda daraja anaingia level ya shetani kama walivyo kina Hittler,au yule aliyeleta corona China tokea kuzimu.
We jamaa!hii shule ulipoitoa ni wapi Mkuu!?

Ina maana hawa masons wanaishi Duniani na kuzimu sio!!?

Kwanini nasikia kuna uchinjaji hasa wa kafara za mbuzi na NG'OMBE Ili mtu ajiunge kwenye vyama vya masons!!?au !!?
 
Hii dunia ina vitu vya ajabu sana na vya kushangaza. Kuna historia baadhi unaweza unaweza kushangazwa nazo mojawapo ikiwa hii niliyopata kusimuliwa.

Msitu wa Nyumbanitu una historia nyingi za kushangaza. Msitu huu upo katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoa wa Njombe. Msitu huu nimepata kusimuliwa kuwa endapo mwanamke atakuwa kwenye siku zake basi hatoruhusiwa kuingia katika msitu huo, Ikiwa atakaidi basi akiingia kwenye huo msitu ndio utakuwa mwisho wake wa kuonekana maana atapotea mazima.

Nadhani hili jambo mnaona linavyostaajibisha. Najiuliza huu msitu una nguvu na miujiza gani mpaka uweze kuwatendea hivyo dada zetu.

JamiiForums naona sasa mnaaza kusonga chai jamani.

Hayo yote Tanzania hii?
 
We jamaa!hii shule ulipoitoa ni wapi Mkuu!?

Ina maana hawa masons wanaishi Duniani na kuzimu sio!!?

Kwanini nasikia kuna uchinjaji hasa wa kafara za mbuzi na NG'OMBE Ili mtu ajiunge kwenye vyama vya masons!!?au !!?
Masoni ni moja ya vyama vya kichawi vipo vingi sana Duniani tena visivyoingiliana Wala kufanana.
Masonic hawachinji wanyama wanaochinja ni hawa wachawi na washirkina wadogo wadogo.

Mason ni kati ya vyama vikubwa vya kichawi Dunia vyenye malengo ya kidunia vipo vyama vingi sana
 
Masoni ni moja ya vyama vya kichawi vipo vingi sana Duniani tena visivyoingiliana Wala kufanana.
Masonic hawachinji wanyama wanaochinja ni hawa wachawi na washirkina wadogo wadogo.

Mason ni kati ya vyama vikubwa vya kichawi Dunia vyenye malengo ya kidunia vipo vyama vingi sana
NASHUKURU mkuu!

Japo nina maswali mengi sana!
Lakini haya yanatosha!

Hawa mashehe wanaowaambia wateja wao wanunue mbuzi zichinjwe hawa sielewi wanafanya KAZI ipi!?je ya mason au uchawi wa KAWAIDA!

Unakuta ng'ombe au mbuzi anachinjwa KWA ajili ya MAELEKEZO fulani ya uganga wa utafutaji wa KAZI fulani fulani!!

Hii ni kumuunga mtu na kuzimu Ili hao wazee wa kuzimu wanmsaidie mhusika kupata anachotaka taka au ni nini hasa!!?

Wale wa pwani wanajua hii kitu!

Unamaelezo yoyote ya hii kitu!?NASIKIA HATA mzee mchonga alifanyiwa hii kitu ya kuchinja Ili mambo yakae sawa!ni KWELI!?
 
NASHUKURU mkuu!

Japo nina maswali mengi sana!
Lakini haya yanatosha!

Hawa mashehe wanaowaambia wateja wao wanunue mbuzi zichinjwe hawa sielewi wanafanya KAZI ipi!?je ya mason au uchawi wa KAWAIDA!

Unakuta ng'ombe au mbuzi anachinjwa KWA ajili ya MAELEKEZO fulani ya uganga wa utafutaji wa KAZI fulani fulani!!

Hii ni kumuunga mtu na kuzimu Ili hao wazee wa kuzimu wanmsaidie mhusika kupata anachotaka taka au ni nini hasa!!?

Wale wa pwani wanajua hii kitu!

Unamaelezo yoyote ya hii kitu!?NASIKIA HATA mzee mchonga alifanyiwa hii kitu ya kuchinja Ili mambo yakae sawa!ni KWELI!?
Shehe yeyeto anaechinja kwa manuizo huyo ni mshirikina sawa na wengine katika uislam hakuna kitu kama Hicho.
Uislam ushirikina ni haramu.
Hao ni wachawi sawa na wale mitume na manabii wa uongo tu.
Zipo elimu za tiba za kiislam zisizohusisha manuizo yeyeto.

Mchonga alitumia uchawi unaitwa dagoo ni uchawi wa fimbo, mavazi ya chui Mobutu,bokasaa, uchawi wa mkia wa wanyama nk wakiinua fimbo juu au kupunga mikia ya wanyama juu kwenye mikutano wanakuwa wanaziita zile roho saidizi kwao na mkutano wote kimya hakuna anaepinga hata mmoja
 
Back
Top Bottom