Mwanamke aliniharibia kabisa maisha yangu, hawa viumbe hatari sana

Kwa kifupi nachoona huyo mkeo hakuwa chaguo lako! Wala wewe hukuwa chaguo lake!
Alikubali kuolewa na wewe ili atimize lengo lake la kusoma! Baada ya kutimiza malengo yake huenda bado angekuacha au angekuendesha anavyotaka!
Ndiyo hapo mnapoambiwa "Usioe Sura Oa mke"!
Anyway, hata hivyo bado machoni pa Mungu ni mkeo! Sahau yote ukimpata anza naye upya!
Changamoto iliyopo sisi kwetu wanaume, Kutokuwa na kazi siyo excuse ya kutotunza familia yako.Hilo wake zetu hawalitambui! Wanatuchekea kama tunaleta sukari, Unga, mchele,Mafuta, nk ndani ya nyumba! Ole wako vikosekane ndani UTAJUTA.
 
Hapo kwenye "asimzidi kipato" pana utata. Maisha ni kupanda na kushuka. Lolote laweza kutokea wakati wowote!
 
Pole man
 
Umetisha Mkuu

Ila unamaanisha nini unaposema mwanamke asikuzidi akili?
 
Hapana penda mtoto wa MaMkwe mazima. Akizingua tokomea mazima pia. Be flexible[emoji3]
 
Pole sana mkuu,haikuwa riziki
 
Umeandika vizuri sana!! Kwenye jamii yetu imejengwa tabia Ya kuona wizi Kazini ni kitu cha kawaida kabisaa.. Ukisoma maelezo Ya huyu Dogo ni wazi aliiba Kazini.. Wizi ni laana ndugu zangu haijalishi umeiba wapi? Kiufupi aliharibu maisha yake mwenyewe Kwa wizi. Mwanamke wala hahusiki Kwa sababu Hakuna popote aliposema mwanamke ndo alimshauri kufanya makosa Kazini.. Anadai alikuwa anampenda Sana mke wake, Kwa hiyo wangekula huo upendo au wangekula Faraja.. Vipi kutibiwa, ingetokea mmojawao kuumwa wangetibiwa na upendo!? Tafuta pesa Kijana acha kutafuta huruma!
 
Umetisha Mkuu

Ila unamaanisha nini unaposema mwanamke asikuzidi akili?
akili ninayozungumzia ni ile common sense yaani mfano inakuja mada fulani halafu anaona unachangia utumbo hapo atakudharau, kifupi uwe mjanjamjanja wa kujua mambo mengi kuliko yeye, kupika upo vizuri, masuala mbalimbali ya nchi unakuwa na uelewa nao japo basics, ukija kwenye mpira angalau hata kama sio shabiki ila ujue hata taifa stars ni nini. Mwanamke anataka mwanaume aliyemzidi kwa akili, maono, usafi ,fedha n.k. hapo ndio heshima ya kiume inapokuja.
 
Nilikua kwnye bwawa la umeme rufiji (JNHPP.).. kule lazima upambane mkuu hakuna namna!..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…