Barnabas Mashamba
JF-Expert Member
- Jul 4, 2020
- 797
- 2,233
Ndugu wanaJF
Jumamosi (01/10/2022) nilileta uzi jukwaani nikiomba kwa aliyetangulia kubarikiwa pesa, aniwezeshe nauli niende kwenye usaili kule kwenye makao makuu ya nchi (kibiashara na Ikulu). Wadau wawili waliniwezesha kiasi cha Tshs 25,000/=.
Baada ya wezesho hilo, nikawa na pungufu ya takribani Tshs 65,000/=. Hadi inafika mida ya saa kumi na mbili jioni, nikawa nimeshakata tamaa ya kuendelea na safari. Kwa vile kulikuwa na sherehe ya harusi, nikaamua nisogee kwenye eneo la harusi hiyo.
Mungu si Athumani, Mathayo wala si Mwanamalundi. Nikiwa ndiyo nina kama dakika takribani 10 tokea nifike kwenye eneo la harusi, hamadi naitwa na mmoja wa ndugu aliyekuwepo mahali hapo. Aliniwezesha kiasi cha Tshs 60,000/=, hivyo ikabidi nianze safari (hapo ni saa 1 na dakika zake nyingi tu).
Safari ya kuelekea Geita mjini ikaanza, nilifanikiwa kufika Geita mjini saa 3 na dakika kama 5 hivi, ajabu ni kwamba mabasi yote ya Dar yalikuwa yamekodiwa (kusafirisha wanafunzi kwenda likizo). Nilipata basi moja liendalo Tabora (wanifaulishe Nzega kwenye basi la Travel Partiner litakalo Bukoba kwenda Dar, maana hilo la kwenda Tabora huyatangulia mabasi yote yatokayo Bukoba.
Asubuhi ikafika (02/10/2022), nilijihimu mapema tu saa 11 na dakika 10, hadi inafika na dakika 35 nilikuwa tayari niko stendi. Kama na dakika 50 akaingia mwanamke mmoja ndani ya Basi, na huyo ndiye aliyefanya nisifanikiwe kufika kwenye usaili.
Nitaendelea saa 2 usiku.