Mwanamke alivyosababisha nichelewe usaili wa mrija wa asali

Ndugu wanaJF

Jumamosi (01/10/2022) nilileta uzi jukwaani nikiomba kwa aliyetangulia kubarikiwa pesa, aniwezeshe nauli niende kwenye usaili kule kwenye makao makuu ya nchi (kibiashara na Ikulu). Wadau wawili waliniwezesha kiasi cha Tshs 25,000/=.

Baada ya wezesho hilo, nikawa na pungufu ya takribani Tshs 65,000/=. Hadi inafika mida ya saa kumi na mbili jioni, nikawa nimeshakata tamaa ya kuendelea na safari. Kwa vile kulikuwa na sherehe ya harusi, nikaamua nisogee kwenye eneo la harusi hiyo.

Mungu si Athumani, Mathayo wala si Mwanamalundi. Nikiwa ndiyo nina kama dakika takribani 10 tokea nifike kwenye eneo la harusi, hamadi naitwa na mmoja wa ndugu aliyekuwepo mahali hapo. Aliniwezesha kiasi cha Tshs 60,000/=, hivyo ikabidi nianze safari (hapo ni saa 1 na dakika zake nyingi tu).

Safari ya kuelekea Geita mjini ikaanza, nilifanikiwa kufika Geita mjini saa 3 na dakika kama 5 hivi, ajabu ni kwamba mabasi yote ya Dar yalikuwa yamekodiwa (kusafirisha wanafunzi kwenda likizo). Nilipata basi moja liendalo Tabora (wanifaulishe Nzega kwenye basi la Travel Partiner litakalo Bukoba kwenda Dar, maana hilo la kwenda Tabora huyatangulia mabasi yote yatokayo Bukoba.

Asubuhi ikafika (02/10/2022), nilijihimu mapema tu saa 11 na dakika 10, hadi inafika na dakika 35 nilikuwa tayari niko stendi. Kama na dakika 50 akaingia mwanamke mmoja ndani ya Basi, na huyo ndiye aliyefanya nisifanikiwe kufika kwenye usaili.

Nitaendelea saa 2 usiku.
Nimeamini jamii forum kuna watu wana akili nyingi sana na wanajua kusoma psychology ya mtu hata kupitia maandishi tu...huyu jamaa juzi na uzi wake aliomba mchango wa nauli akisema awahi kwenye usahili wa kulamba asali....
Asilimia kubwa ya watu walionyesha kumcrash na baadhi ya hoja nazozikumbuka ni kuwa hayuko Sirius na mambo ya msingi, hakuwa na haja ya kuweka details za wasaili wake na majina ya wanaosailiwa nadhani tunakumbuka vizuri
Na hata baadhi ya watu wakamkanya kuwa anachezea maisha....
Sasa baadhi ya wasamaria na pengine kutoka humu humu wamejinyima wanakusudia halafu unarudi na maada ya kipumbavu kuwa mwanamke mwanamke...hivi mtu aliyekusaidia kwa lengo zuri lako akiona hiki unachoandika unafikiri atajiskiaje.....
Hamna kitu humu.....
 
Hujasoma mpaka mwisho lakini povu kama lote. Relax, rudi hapa saa 2, naamini unachofikiria kitakuwa tofauti na uhalisia.
 
Sawa kaka, hata kama hitimisho lako ni tofauti na wadau wengi wanavyofikiria lakini uwandishi wako unapoteza sifa ya SERIOUSNESS. Mbaya zaidi uzi wako uliopita ulihusu jambo ambalo ni very SIGNIFICANT ingawa nalo lilikuwa na mapungufu kadhaa lakini walioguswa walikuwezesha, sasa unapokuja na hoja ambayo ina jambo lenye haja ya hadhira kufahamu alafu njia ya uwakilishaji ulioichagua inatatiza watu.
Above all it's you who decide which way to address your issue up to audiance, ila ujue kuwa uwakilishaji wa jambo huwajengea picha hadhira jinsi mwakilishi alivyo.
 
I appreciate your brevity.
 
Sisi tutasema nini tena Mkuu ikiwa wewe umeamua iwe hvyo...

Bangi ya Uyui Tabora siku hizi imekuwa maarufu kuliko cha Arusha...
 
Kwa hiyo mkuu unatumia bangi?

Hivi wavuta bangi huwa mnatafuta nini hasa kwenye bangi? Moshi ama?
 
Nimeamini jamii forum kuna watu wana akili nyingi sana na wanajua kusoma psychology ya mtu hata kupitia maandishi tu...huyu jamaa juzi na uzi wake aliomba mchango wa nauli akisema awahi kwenye usahili wa kulamba asali....
Asilimia kubwa ya watu walionyesha kumcrash na baadhi ya hoja nazozikumbuka ni kuwa hayuko Sirius na mambo ya msingi, hakuwa na haja ya kuweka details za wasaili wake na majina ya wanaosailiwa nadhani tunakumbuka vizuri
Na hata baadhi ya watu wakamkanya kuwa anachezea maisha....
Sasa baadhi ya wasamaria na pengine kutoka humu humu wamejinyima wanakusudia halafu unarudi na maada ya kipumbavu kuwa mwanamke mwanamke...hivi mtu aliyekusaidia kwa lengo zuri lako akiona hiki unachoandika unafikiri atajiskiaje.....
Hamna kitu humu.....
Kuliko kusaidia humu bora hiyo hela kuinywa beer.... #vijanawaovyo
 
Kama ni muungwana rudisha hela za haonwaliokuchangia.. sidhani kama utakuja na stori yoyote hyo saa mbili ambayo itafanya tukuonee huruma. Lengo kuu ilikua kwenda kwenye usaili, kama hukwenda with any reason tofauti na kuugua au kufa hautakua mstaarabu. Maana kama n usafiri hata lori ungepanda ungefika.
Hopeless!
 
Hujasoma mpaka mwisho lakini povu kama lote. Relax, rudi hapa saa 2, naamini unachofikiria kitakuwa tofauti na uhalisia.
Nirudi hadi mwisho kuona jinsi huyo mwanamke aliyokukosesha usaili ambao watu walijinyima wakichangia sio...we jamaa nadhani there is something wrong in your mind...umeshasema kwenye kicha cha uzi wako huu kwamba mwanamke kakukosesha usaili hiyo tu inatosha kuonyesha hauko Sirius na jambo ulilokuwa unaenda kufanya na ambalo watu wamekuchangia ..ko nikirudi ndio mwisho wa story utakuwa umewahi kwenye usaili sio....acha kuchezea akili za watu bwana
 
Ndugu wanaJF

Jumamosi (01/10/2022) nilileta uzi jukwaani nikiomba kwa aliyetangulia kubarikiwa pesa, aniwezeshe nauli niende kwenye usaili kule kwenye makao makuu ya nchi (kibiashara na Ikulu). Wadau wawili waliniwezesha kiasi cha Tshs 25,000/=.

Baada ya wezesho hilo, nikawa na pungufu ya takribani Tshs 65,000/=. Hadi inafika mida ya saa kumi na mbili jioni, nikawa nimeshakata tamaa ya kuendelea na safari. Kwa vile kulikuwa na sherehe ya harusi, nikaamua nisogee kwenye eneo la harusi hiyo.

Mungu si Athumani, Mathayo wala si Mwanamalundi. Nikiwa ndiyo nina kama dakika takribani 10 tokea nifike kwenye eneo la harusi, hamadi naitwa na mmoja wa ndugu aliyekuwepo mahali hapo. Aliniwezesha kiasi cha Tshs 60,000/=, hivyo ikabidi nianze safari (hapo ni saa 1 na dakika zake nyingi tu).

Safari ya kuelekea Geita mjini ikaanza, nilifanikiwa kufika Geita mjini saa 3 na dakika kama 5 hivi, ajabu ni kwamba mabasi yote ya Dar yalikuwa yamekodiwa (kusafirisha wanafunzi kwenda likizo). Nilipata basi moja liendalo Tabora (wanifaulishe Nzega kwenye basi la Travel Partiner litakalo Bukoba kwenda Dar, maana hilo la kwenda Tabora huyatangulia mabasi yote yatokayo Bukoba.

Asubuhi ikafika (02/10/2022), nilijihimu mapema tu saa 11 na dakika 10, hadi inafika na dakika 35 nilikuwa tayari niko stendi. Kama na dakika 50 akaingia mwanamke mmoja ndani ya Basi, na huyo ndiye aliyefanya nisifanikiwe kufika kwenye usaili.

Nitaendelea saa 2 usiku.
Hii ni series kama Egoli?
 
Kama ni muungwana rudisha hela za haonwaliokuchangia.. sidhani kama utakuja na stori yoyote hyo saa mbili ambayo itafanya tukuonee huruma. Lengo kuu ilikua kwenda kwenye usaili, kama hukwenda with any reason tofauti na kuugua au kufa hautakua mstaarabu. Maana kama n usafiri hata lori ungepanda ungefika.
Hopeless!
Hapo tuu...hoja ni uende kwenye usaili na watu wamekuchangia uende ..kama hujaenda rudisha pesaa hayo ya mwanamke ni story yako ambayo haitabadili uhalisia kwamba hukwenda.....
 
Nirudi hadi mwisho kuona jinsi huyo mwanamke aliyokukosesha usaili ambao watu walijinyima wakichangia sio...we jamaa nadhani there is something wrong in your mind...umeshasema kwenye kicha cha uzi wako huu kwamba mwanamke kakukosesha usaili hiyo tu inatosha kuonyesha hauko Sirius na jambo ulilokuwa unaenda kufanya na ambalo watu wamekuchangia ..ko nikirudi ndio mwisho wa story utakuwa umewahi kwenye usaili sio....acha kuchezea akili za watu bwana
Duh, sema unapovuka sana mkuu. Twende taratibu mkuu.
 
Hapo tuu...hoja ni uende kwenye usaili na watu wamekuchangia uende ..kama hujaenda rudisha pesaa hayo ya mwanamke ni story yako ambayo haitabadili uhalisia kwamba hukwenda.....
Kuna mmoja hana namba lilikuja jina tu, nishauri namrudishiaje? Ndugu yeye ilikuwa ni mkopo (lazima niulipe), mwanaJF mmoja aliyetuma ndiye kuna namba na nitairudisha pesa yake maana haijatumika kwa lengo nililoiombea.
 
Back
Top Bottom