Mwanamke alivyosababisha nichelewe usaili wa mrija wa asali

Ndugu wanaJF

Bila shaka tuliishia hapa

Asubuhi ikafika (02/10/2022), nilijihimu mapema tu saa 11 na dakika 10, hadi inafika na dakika 35 nilikuwa tayari niko stendi. Kama na dakika 50 akaingia mwanamke mmoja ndani ya Basi, na huyo ndiye aliyefanya nisifanikiwe kufika kwenye usaili.

Tuendelee

Mwanamke huyo alikuwa ni mama mwenye watoto wawili wa kiume (umri kati ya 4 - 5 kwa mkubwa na 2 - 3 kwa mdogo) akiwa na sifa zifuatazo.
1. Akioga maji yanatiririka bila mkwamo (japo yupo katikati ya ujana na uzee).
2. Mweupe (siyo weupe wa mkorogo).
3. Macho ya vidume hayawezi kukwepa kutazama kwa nyuzi zote 360 n.k.

Mama huyo katika kuhojiwa na mkatisha tiketi akasema anaelekea Singida (kumbuka route ya hilo gari ni Tabora), hivyo ikabidi aelezwe kuwa

"Tunaelekea Tabora, tutakushusha Nzega tukufaulishe kwenye mabasi ya Bukoba, uko tayari"? Mama akasema niko tayari (japo ya wasiwasi kwa mbali.

Hatimaye ilipofika saa 12:09 asubuhi, safari ilianza rasmi. Route ilikuwa ni Geita - Katoro - Lulembela - Ushirombo - Masumbwi - Kahama - Tinde - Nzega hadi Tabora.

Tulifika Katoro around saa 12:40s. Tulikaa pale hadi inafika saa 1:10 asubuhi safari bado haijaanza.

Ndipo yule mwanamke (niliyemwelezea hapo juu) akaanza maneno yafuatayo, "washeni gari tuondoke, mnataka nichelewe mabasi ya Singida?". Aliweka zogo hapo kwa dakika kama mbili hivi.

Hatimaye tukatoka Katoro saa 1:15 asubuhi, kwa wenyeji wa Katoro, njia ya Iparamasa (karibu na Katoro sec school) kuna lile jengo (nadhani la maduka, ni la ghorofa), wakapitia pale wachukue mizigo, hapo ndipo Kimbembe kikaanza.

Mama akapata mchecheto zaidi ya aliokuwa nao stendi, acha aanze kuwalazimisha kuwasha gari (huku mizigo bado inapakiwa). Kuna wanaume wanne wakamsapoti mama, wacha waanze kutukana dreva wakimwambia arudishe nauli zao.

Maneno makali yalirushwa kwa kama dakika kumi (wakati maneno yanaanza dreva alikuwa ashaanza kutoa gari, ikabidi asimame maana wanamlazimisha asimame. Hatimaye huyo mwanamke akatoa kauli ifuatayo

"Hamnijui mimi ni nani, leo nawaonyesha, subirini tufike kwa trafiki".

Dreva katika kuwashauri watulie, aliongea kauli ifuatayo, "jamani, mnavyonipigia makelele, hamuoni mnanichanganya na mnaweza sababisha nikose umakini na kupelekea hata gari kupinduka". Mama na wapambe wake wakaitafsiri dreva anawaambia atapindua gari. Hatimaye dreva alimwachia konda aendeshe gari.

Safari ikaanza tena baada ya upepo wa kishetani kutulia mnamo saa 2:39 asubuhi (yaani abiria wakawa wamekula muda mrefu kuliko ule uliotumika kupandisha mizigo), (thinking illogically).

Tumetembea kidogo tu, kwa wenyeji wa Katoro, kuna trafiki wana kituo mitaa jirani na nguzo za gridi ya taifa (sijui jina), konda aliposhuka tu, mama alitoka mbio hadi kwa trafiki ofisa na kushusha tuhuma kedekede kama ifuatavyo (akisapotiwa na vidume vinne, sijui vilikuwa vimemtamani).
1. Dreva ametutishia atatuangusha njiani, hivyo sitaki aendeshe gari (kumbuka muda huo anayeendesha gari ni konda).
2. Wananichelewesha kufika Singida, hivyo naomba gari irudi stendi (ya Katoro) nikarudishiwe nauli nitafute gari nyingine.
3... Mimi nilikuwa ndani ya gari hivyo mashitaka mengine sikuyasikia vizuri.

Baada ya kama dakika 20 za kusikiliza kila upande (mama na wapambe) pamoja na dreva na konda, hatimaye gari ikaamuriwa kurudi. Dreva akageuza gari uelekeo wa kurudi Katoro na kusimama hapo kwa trafiki ili kesi iendelee.

Ngoja nipumzike kidogo, naendelea saa 4:30 usiku huu.
 
Ndugu wanaJF

Jumamosi (01/10/2022) nilileta uzi jukwaani nikiomba kwa aliyetangulia kubarikiwa pesa, aniwezeshe nauli niende kwenye usaili kule kwenye makao makuu ya nchi (kibiashara na Ikulu). Wadau wawili waliniwezesha kiasi cha Tshs 25,000/=.

Baada ya wezesho hilo, nikawa na pungufu ya takribani Tshs 65,000/=. Hadi inafika mida ya saa kumi na mbili jioni, nikawa nimeshakata tamaa ya kuendelea na safari. Kwa vile kulikuwa na sherehe ya harusi, nikaamua nisogee kwenye eneo la harusi hiyo.

Mungu si Athumani, Mathayo wala si Mwanamalundi. Nikiwa ndiyo nina kama dakika takribani 10 tokea nifike kwenye eneo la harusi, hamadi naitwa na mmoja wa ndugu aliyekuwepo mahali hapo. Aliniwezesha kiasi cha Tshs 60,000/=, hivyo ikabidi nianze safari (hapo ni saa 1 na dakika zake nyingi tu).

Safari ya kuelekea Geita mjini ikaanza, nilifanikiwa kufika Geita mjini saa 3 na dakika kama 5 hivi, ajabu ni kwamba mabasi yote ya Dar yalikuwa yamekodiwa (kusafirisha wanafunzi kwenda likizo). Nilipata basi moja liendalo Tabora (wanifaulishe Nzega kwenye basi la Travel Partiner litakalo Bukoba kwenda Dar, maana hilo la kwenda Tabora huyatangulia mabasi yote yatokayo Bukoba.

Asubuhi ikafika (02/10/2022), nilijihimu mapema tu saa 11 na dakika 10, hadi inafika na dakika 35 nilikuwa tayari niko stendi. Kama na dakika 50 akaingia mwanamke mmoja ndani ya Basi, na huyo ndiye aliyefanya nisifanikiwe kufika kwenye usaili.

Nitaendelea saa 2 usiku.
Sawa profesor wa maths

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu wanaJF

Bila shaka tuliishia hapa

Asubuhi ikafika (02/10/2022), nilijihimu mapema tu saa 11 na dakika 10, hadi inafika na dakika 35 nilikuwa tayari niko stendi. Kama na dakika 50 akaingia mwanamke mmoja ndani ya Basi, na huyo ndiye aliyefanya nisifanikiwe kufika kwenye usaili.

Tuendelee

Mwanamke huyo alikuwa ni mama mwenye watoto wawili wa kiume (umri kati ya 4 - 5 kwa mkubwa na 2 - 3 kwa mdogo) akiwa na sifa zifuatazo.
1. Akioga maji yanatiririka bila mkwamo (japo yupo katikati ya ujana na uzee).
2. Mweupe (siyo weupe wa mkorogo).
3. Macho ya vidume hayawezi kukwepa kutazama kwa nyuzi zote 360 n.k.

Mama huyo katika kuhojiwa na mkatisha tiketi akasema anaelekea Singida (kumbuka route ya hilo gari ni Tabora), hivyo ikabidi aelezwe kuwa

"Tunaelekea Tabora, tutakushusha Nzega tukufaulishe kwenye mabasi ya Bukoba, uko tayari"? Mama akasema niko tayari (japo ya wasiwasi kwa mbali.

Hatimaye ilipofika saa 12:09 asubuhi, safari ilianza rasmi. Route ilikuwa ni Geita - Katoro - Lulembela - Ushirombo - Masumbwi - Kahama - Tinde - Nzega hadi Tabora.

Tulifika Katoro around saa 12:40s. Tulikaa pale hadi inafika saa 1:10 asubuhi safari bado haijaanza.

Ndipo yule mwanamke (niliyemwelezea hapo juu) akaanza maneno yafuatayo, "washeni gari tuondoke, mnataka nichelewe mabasi ya Singida?". Aliweka zogo hapo kwa dakika kama mbili hivi.

Hatimaye tukatoka Katoro saa 1:15 asubuhi, kwa wenyeji wa Katoro, njia ya Iparamasa (karibu na Katoro sec school) kuna lile jengo (nadhani la maduka, ni la ghorofa), wakapitia pale wachukue mizigo, hapo ndipo Kimbembe kikaanza.

Mama akapata mchecheto zaidi ya aliokuwa nao stendi, acha aanze kuwalazimisha kuwasha gari (huku mizigo bado inapakiwa). Kuna wanaume wanne wakamsapoti mama, wacha waanze kutukana dreva wakimwambia arudishe nauli zao.

Maneno makali yalirushwa kwa kama dakika kumi (wakati maneno yanaanza dreva alikuwa ashaanza kutoa gari, ikabidi asimame maana wanamlazimisha asimame. Hatimaye huyo mwanamke akatoa kauli ifuatayo

"Hamnijui mimi ni nani, leo nawaonyesha, subirini tufike kwa trafiki".

Dreva katika kuwashauri watulie, aliongea kauli ifuatayo, "jamani, mnavyonipigia makelele, hamuoni mnanichanganya na mnaweza sababisha nikose umakini na kupelekea hata gari kupinduka". Mama na wapambe wake wakaitafsiri dreva anawaambia atapindua gari. Hatimaye dreva alimwachia konda aendeshe gari.

Safari ikaanza tena baada ya upepo wa kishetani kutulia mnamo saa 2:39 asubuhi (yaani abiria wakawa wamekula muda mrefu kuliko ule uliotumika kupandisha mizigo), (thinking illogically).

Tumetembea kidogo tu, kwa wenyeji wa Katoro, kuna trafiki wana kituo mitaa jirani na nguzo za gridi ya taifa (sijui jina), konda aliposhuka tu, mama alitoka mbio hadi kwa trafiki ofisa na kushusha tuhuma kedekede kama ifuatavyo (akisapotiwa na vidume vinne, sijui vilikuwa vimemtamani).
1. Dreva ametutishia atatuangusha njiani, hivyo sitaki aendeshe gari (kumbuka muda huo anayeendesha gari ni konda).
2. Wananichelewesha kufika Singida, hivyo naomba gari irudi stendi (ya Katoro) nikarudishiwe nauli nitafute gari nyingine.
3... Mimi nilikuwa ndani ya gari hivyo mashitaka mengine sikuyasikia vizuri.

Baada ya kama dakika 20 za kusikiliza kila upande (mama na wapambe) pamoja na dreva na konda, hatimaye gari ikaamuriwa kurudi. Dreva akageuza gari uelekeo wa kurudi Katoro na kusimama hapo kwa trafiki ili kesi iendelee.

Ngoja nipumzike kidogo, naendelea saa 4:30 usiku huu.
Hizi drama za wabongo bwana.....we jamaa kubali tu kuwa hauko Sirius....kwa mtu anayewahi usaili wala asingesubiri kufuatilia hizi bongo movie huku akijua muda wake ni limited.....acha tuendelee kufurahisha macho
 
Nimeona watu wanaanza kukulaumu bila kujuwa tatizo la msingi kila mtu aliongea lake ilimradi tu sasa ona ulivyopindua meza tofauti na fikra za wengi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Nirudi hadi mwisho kuona jinsi huyo mwanamke aliyokukosesha usaili ambao watu walijinyima wakichangia sio...we jamaa nadhani there is something wrong in your mind...umeshasema kwenye kicha cha uzi wako huu kwamba mwanamke kakukosesha usaili hiyo tu inatosha kuonyesha hauko Sirius na jambo ulilokuwa unaenda kufanya na ambalo watu wamekuchangia ..ko nikirudi ndio mwisho wa story utakuwa umewahi kwenye usaili sio....acha kuchezea akili za watu bwana
Kuna namna ban zinakata stimu ya kumjibu mtu aliyevuka mipaka ya utu na ustaarabu
 
Hizi drama za wabongo bwana.....we jamaa kubali tu kuwa hauko Sirius....kwa mtu anayewahi usaili wala asingesubiri kufuatilia hizi bongo movie huku akijua muda wake ni limited.....acha tuendelee kufurahisha macho
Hakika
 
Tuendelee

Baada ya kuona trafiki hajapata ufumbuzi hadi dakika 40 tokea asimamishe gari (alikuwa anawasiliana na mkuu wake), ilibidi nisogee karibu na kuongea maneno yafuatayo

"Mpaka sasa, muda tuliosimama hapa ni mrefu kuliko unaolalamikiwa tuliopoteza stendi". Baada ya hapo akazidisha zaidi kuwasiliana na bosi wake na hatimaye akaja akaomba tiketi za wote wanaosafiri kuelekea Singida, Dom, Moro, Dsm. Tukakusanya na hatimaye akaamuru tukifika Nzega turudishiwe nauli (wakate nauli ya Geita hadi Nzega Tshs 15,000), lakini hii ni kwa wale wanaotaka kutafuta usafiri wao wenyewe wa kuendelea na safari.

Hatimaye, baada ya vuta nikuvute, ilipofika saa 4:19 asubuhi tukaruhusiwa kuendelea na safari.

Twende mdogo mdogo.

1. Wapi muda ulipotea zaidi kati ya stendi na pale kwa matrafiki?
2. Nani aliadhirika kati ya mmiliki wa basi (pamoja na dreva na konda) na abiria akiwemo na huyo mwanamke? Nani alichelewa kwenye mishe zake? Maana mwenye basi bado ataingiza pesa katika kila kituo anachofika.

Yote haya ilikuwa sababu ya "ego", kuonyesha ujuaji usio na tija yoyote ile.

Kwa mliopita njia ya Katoro - Lulembela - Ushirombo, unaweza kadiria kwa kutoka saa nne tungefika Kahama saa ngapi?

Tulifika Kahama saa 6 kuelekea saa 7 na kutoka saa saba na dakika kadhaa. Tulifika Nzega saa 9 kasoro dakika kama 14. Basi la Travel Partiner ambalo ndilo ilikuwa tufaulishwe likawa limeshapita.

Kilichofuata ikabidi kusubiri lolote litakalokuwa linaenda Dar.

Tukaelekea barabarani (mabasi mengi ya route ndefu hayaingii ndani ya stendi ya Nzega) nadhani wenyeji mtakubaliana nami katika hili. Tuliotoka kwenye hilo gari tulikuwa watatu (wengine walielekea wanakojua wao), yule mama ilibidi atafute bajaji aende mjini Nzega kutafuta sehemu ya kulala (maana waliamua kumchomea kwenye basi liitwalo Malagwa Express (sijui kama nimepatia spelling lifanyalo safari kati ya Dar na Singida). Tulikuta vijana watatu pale barabarani na wakatueleza hivi.

"Tupo hapa tokea saa 2 asubuhi, kila basi linalokuja linakuwa limejaza abiria". Punde kweli nikashuhudia mwenyewe, ilipita Frester bus, piga mkono hata kupunguza mwendo kidogo haikupunguza. Ikafuatia basi nyingine (nilishika rangi yake tu si jina, ilikuwa na rangi ya blue bahari inatoka Bukoba). Mpaka hapo kukawa na basi moja tu lililosalia, nalo ni Friends litokalo Kampala. Huwa linapita Nzega around saa 12, lakini walipofanya mawasiliano, lilikuwa limejaa pia.

Ilibidi kwenda njia panda (wenyeji naamini mnapajua pale watu wanapotega usafiri wa ama lori, private cars) kwa pale Nzega. Ni njia panda ya barabara iendayo Tabora mjini.

Kabla ya kwenda njia panda zilikuja gari mbili muundo wa Coaster (zilibeba wanamziki), moja ilikuwa na lebel ya Fiesta na nyingine ilikuwa na logo ya clouds tv kwa nyuma, kuongea na dreva hakuwa na noma, alikuwa tayari kutubeba, ila wasanii wakadai hawataki mtu aongezeke asiye msanii.

Pale njia panda, malori mengi yalikuwa yanapitiliza pasi ya kusimama, na yaliyosimama madereva walidai hawatibiwi (watalala njiani).

Around saa moja ndipo lori moja likaja na jamaa akasema anatoboa, lakini mida itakayofika mjini ni kuanzia saa nne asubuhi ya tarehe 03/10/2022 kwenda mbele. Wakati huo usaili unaanza saa 2:00 asubuhi, nikaona nitapoteza muda na pesa bure, nikaona hiyo si haki yangu.

Hivyo nilitafuta lodge ya bei nafuu na kuchapa usingizi (iliitwa Itongela (sidhani kama nimeandika jina sahihi)).

Jana nikasubiri gari nililopanda hadi Nzega, wakanipa lifti (bure) hadi Geita.
 
Mlionitumia pesa (wawili wa humu JF), mmoja ilileta namba mwingine haikuleta namba.

Uzi huu nimeuleta mahsusi kwa ajili yenu, natambua mlijinyima mkatoa mali yenu, japo ndiyo hivyo, nilipambana ikashindikana. Kwa ambaye wakati anatuma ilileta na namba, nitakurudishia kesho (maana niliona nikirudisha pesa pasipo maelezo ya kwanini inarudi isingekuwa sawa). Walau sasa hivi hata ukiona muamala utajua pesa imerudi kwa sababu haikutumika kwa lengo kusudiwa.

Kwa ambaye ulituma pesa kupitia wakala nadhani (....STORE...), nitafunga PM yangu hadi kesho saa nne, utaniandikia namba yako huko (utaje na jina la agent lililokuja huku) nami nitakurudishia pesa yako.

Asanteni sana. Kesho nitakuja na uzi wa the way forward (maana kama ajira imekosekana, maisha ya utafutaji sharti yasonge).
 
Back
Top Bottom