Mwanamke aliyejifanya Msukule akamatwa na wananchi akiiba, Arusha

Mwanamke aliyejifanya Msukule akamatwa na wananchi akiiba, Arusha

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mwanamke mmoja anayedhaniwa kuwa ni msukule amekamatwa mkoani Arusha, ndani ya duka la dada mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe

Mwanamke huyo alikutwa akiiba vitu mbalimbali, ikiwemo viatu na nguo, kitendo kilichowashangaza wateja na majirani waliokuwa karibu na eneo hilo
‎
‎Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa hali ya taharuki ilitanda baada ya kuona mwanamke huyo, licha ya kuvaa baibui linalofunika mwili mzima, akihusishwa na wizi wa wazi. Baadhi ya wananchi walidai kuwa kitendo hicho kilionekana cha ajabu kutokana na muonekano wake wa kificho
‎
‎Mwenyekiti wa mtaa husika amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kueleza kuwa mara baada ya kupata taarifa alilazimika kuwasiliana na Jeshi la Polisi. Polisi walifika katika eneo hilo na kumchukua mwanamke huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi na hatua za kisheria


 
Back
Top Bottom