Mwanamke aliyekaa karibu na CAG, says it all!!

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,420
Mimi sikuwa muumini wa Magufuli, lakini naomba kuwaeleza kwa body language ya mwanamke aliyekaa karibu na CAG inasema yote Ripoti ya CAG imejaa siri nzito na siku si nyingi tutaona kuna nini nyuma ya hii report

Huyo mama aliyekaa karibu na msoma repoti simfahamu lakini hisia zangu zinaenda mbali zaidi na kuniambia kuna kitu kwenye hii repoti

Mtazame vizuri utagundua!

 
Uso wa huyo Mama umebeba ujumbe mzito kuliko ripoti yenyewe ya CAG.
Ni awamu ya JPM tu ambapo report ya CAG uwa inamchafua πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ yani mnafurahisha sana.

Kama alijua hakuna madudu kwani alijitoa kwenye mikataba ya transparency? Nini alitaka kuficha?

Ingekuwa JK naye angekuwa kama awamu ya Magu hakika JK angeondoka madarakani akiwa msafi sana. Ni vile aliwaruhusu watu wajadili, vyombo vichambue, report ijadiliwe bungeni ndipo akaonekana fisadi.

Ila kikwete huyu huyu ndiye mwanzilishi wa shule za kata, umeme wa REA, kuunga barabara mikoa yote. Na ni kupitia project kama hizi ndipo watu walipiga pesa ila yeye alikuwa tayari mambo yajadiliwe.
 
Amebanwa na kitu balaa..anaishia kubetua lipsπŸ˜„
 
Awamu ya JK kuwa ilifanya ufisadi fulani haihalalishi wala haizuu kuwa awamu ya Magufuli ilikuwa ni awamu ya ufisadi based on CAG report. Kwa kutumia ripoti ya CAG Magufuli alikuwa mwizi, fisadi, kiongozi mzembe sana na asiejali maslahi ya wananchi.
 
Atachafuliwa ili aonekane hakufaa...ila ipo siku tutamkumbuka...tukubali tukatae...

Ipo siku...
Ni vigumu kumchafua mtu msafi..., tatizo alisafishwa sana na uchafu wote ulifichwa ndio maana huu uozo watu wanashangaa, hii yote aliileta mwenyewe kwa kuepuka transparency, na ninashukuru hii tabia haijaendelea ama sivyo tungeendelea kupigwa bila kujua na kupewa propaganda kwamba sisi ni matajiri wakati uhalisia tumepigika
 
Yaani unafagia chumbani na sebuleni halafu uchafu unaujaza uvunguni mwa kitanda... !!!! Siku anakuja mwingine anautoa uchafu huo nje, wanaanza kubisha kwamba haujatoka kwenye nyumba hiyo, KISA NJE ANAONEKANA MTANASHATI..!!! AJABU..

Si mnakumbuka yule mwalimu kama sijosei wa Kibasila Sec alivyojaza kinyesi ndani ya nyumba na siku anagundulika kila mtu akashangaa..!!!??? NDIO HAYA SASA
 
Hakuna lolote hapo mbona ya Assad waliikataa wailete na yake pia tufaye comparison au na yeye alikuwa na hila na roho mbaya
 
Prof. Adolf Mkenda, ulikuwa Katibu Mkuu wizara ya Maliasili na utalii ,wajibika soon. Kabla hujawajibishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…