Wapo ambao wanataka muanze pamoja. Mfano ni juu yangu mimi mwenyewe, nilimuimbisha pisi kali moja hivi akanikubalia, katika mapenzi yetu siku moja nikaamua kumpeleka kwenye viassets vyangu, hakika siku hiyo alinyong'onyea sana. Baadae tumekaa sehemu na katika kumuuliza mbona umekuwa hivyo, jibu alilonipa nilichoka mkuu. Aliniambia "NILITAMANI SANA MWANAUME AMBAYE NITAANZA NAE KWA PAMOJA SIO NILIYEMKUTA NA KILA KITU" Mkuu nilichoka. Nilijua kuwa atafurahi na aamini amepata sehemu sahihi kumbe kinyume chake