Kwa kawaida pesa haiwezi kuchukua nafasi ya mwanaume. Ni kweli baadhi ya wanaume wanaogopa kuoa wanawake wenye pesa na wapo wanaume wanaotaka kuoa wanawake wenye pesa.Mwenye kuamua uolewe au usiolewe ni wewe mwanamke kwa namna utakovyo kuwa unaishi ikiwa pamoja na kauli zako katika harakati za maisha. Nijuavyo mimi kwenye ndoa hatuoi au kuolewa na pesa, elimu, ama social status.Tunaoa au kuolewa na mtu (personality) tukitegemea maisha yenye furaha, Kwa sababu kufurahi ndicho kitu kinachopendwa na wengi.Mtu anaweza kuoa mwanamke asiye na pesa asipate furaha.Kwa sababu kufurhi ni pamoja na kuthibitisha kuwa wewe ni mwanamke au mwanaume kwelikweli, uthibitisho kuo huanzia kwenye ndoa na unaextend kwenye mambo mengine.Kuwa na pesa bila mume haviwezi kukuletea furaha.Ndoa ni jambo muhimu sana liletalo furaha ikitokea umeolewa au kuoa the right man or woman respectively. Kwa mwanamke mwenye pesa, endelea kutafuta pesa, ishi maisha yenye staha, tawala pesa zako, usitawaliwe na pesa, ishi simple life, usinjionyeshe kuwa unapesa, wala unahitaji la kuolewa. Wapo wanaume wa maana wanaotaka wanawake wa aina hiyo, watakufuata, na wewe usijirahisi walakuwa mgumu sana.Test to prove mtu anakuhitaji wewe na siyo pesa zako maana lolote laweza tokea kwenye maisha pesa zikaisha.Kama mtu kakuoa wewe na siyo pesa, pesa zikiisha wewe unaendelea kuwepo na ndoa inadumu na akioa pesa zako na siyo wewe pesa zikiisha na ndoa inaisha.