Wamejaa hapa wanawake wenye hela zao, lakini wanaogopa kuchangia hii mada!!
Baba askofu hebu tupe uzoefu wako katika hili.
Nimesoma post zote hakuna hata mdada mmoja alie sema kua yeye kamzidi uwezo mumewe na mambo yanaenda! So JS utampata wa level yako!
Tumsifu Yesu Kristu Mtumishi...
Ni kwamba wanawake wenye hela ni watoaji wazuri wa sadaka kanisani...
Akchwale... nasubiri wajitokeze... wakitokea nijulisheni tafadhali niwakaribishe kanisani (si unajua watumishi wa mungu pia wanahitaji neema za sadaka)...😛ray2:
bwana mkubwa...!Basi wewe una lako jambo. Si muda wote unahangaika na scientific proofs? Zimewekwa hapo halafu unahaha kutafuta mlnago wa kutokea!!!!:disapointed:
Soma hapa?
Tumsifu Yesu Kristu Mtumishi...
global warming.Wandugu za leo,
Hivi ukikutana na mwanamke umempenda na unatamani awe wako wa milele (kumuoa) lakini unakuta bahati nzuri (au mbaya kwa wengine) huyo mwanamke yuko safi kimaisha kazi nzuri kama pesa anazo kama mali anazo pia (sio hawa wamama watu wazima hapana wadada tu wenye umri unaofaa kuolewa) utamuoa hata kama wewe huna thamani ya kiuchumi aliyo nayo?
kwa nini nimeuliza hivi, kwa sababu katika mazungumzo ya kawaida tu jana kuna rafiki yangu akaniambia watu wataogopa kutangaza nia kwangu nikiendelea kujijenga kimaisha and it got me thinking.
Sasa wanaume utamuoa tu huyo dada hata kama wewe hali yako si fresh? na wadada utakuwa bread provider kwa huyo mumeo? mapenzi yana nafasi yake na pia uwezo kiuchumi una nafasi. zamani haikuwa hivi lakini kadri siku zinavyozidi kusonga mbele mambo yanabadilika
sasa hii ndugu yangu ni weakness tu ya wanawake walio wengi...!sitakaa nibishe kwamba wanawake HAWANA DHARAU TO THAT LEVEL!Inategemea na jinsi makuzi yako yalivyokuwa wengine dada zetu mkiwa na uwezo tu hata ukisalimiwa kujibu mpaka umthathimini juu mpaka chini sasa hapo inabidi tukuogope
mkuu nashukuru umeliona hili....!Kwa kawaida pesa haiwezi kuchukua nafasi ya mwanaume. Ni kweli baadhi ya wanaume wanaogopa kuoa wanawake wenye pesa na wapo wanaume wanaotaka kuoa wanawake wenye pesa.Mwenye kuamua uolewe au usiolewe ni wewe mwanamke kwa namna utakovyo kuwa unaishi ikiwa pamoja na kauli zako katika harakati za maisha. Nijuavyo mimi kwenye ndoa hatuoi au kuolewa na pesa, elimu, ama social status.Tunaoa au kuolewa na mtu (personality) tukitegemea maisha yenye furaha, Kwa sababu kufurahi ndicho kitu kinachopendwa na wengi.Mtu anaweza kuoa mwanamke asiye na pesa asipate furaha.Kwa sababu kufurhi ni pamoja na kuthibitisha kuwa wewe ni mwanamke au mwanaume kwelikweli, uthibitisho kuo huanzia kwenye ndoa na unaextend kwenye mambo mengine.Kuwa na pesa bila mume haviwezi kukuletea furaha.Ndoa ni jambo muhimu sana liletalo furaha ikitokea umeolewa au kuoa the right man or woman respectively. Kwa mwanamke mwenye pesa, endelea kutafuta pesa, ishi maisha yenye staha, tawala pesa zako, usitawaliwe na pesa, ishi simple life, usinjionyeshe kuwa unapesa, wala unahitaji la kuolewa. Wapo wanaume wa maana wanaotaka wanawake wa aina hiyo, watakufuata, na wewe usijirahisi walakuwa mgumu sana.Test to prove mtu anakuhitaji wewe na siyo pesa zako maana lolote laweza tokea kwenye maisha pesa zikaisha.Kama mtu kakuoa wewe na siyo pesa, pesa zikiisha wewe unaendelea kuwepo na ndoa inadumu na akioa pesa zako na siyo wewe pesa zikiisha na ndoa inaisha.
mkuu nashukuru kwa post yako maridhawa kabisa...!Kwa kawaida katika mila nyingi mwanaume ni mtawala wa nyumba ukiachilia kwa ndugu zetu kina Msimbe ambao huwa wanatawaliwa. Kuatwala maana yake kuwa safi katika nyanja zote. Inapotokea mwanamke kuwa na hali njema ya kipato kuliko mwanaume inakuwa tayari tatizo la kisaikolojia. Huyo mwanaume hata kama hata nyanyaswa atahisi kuwa ananyanyaswa. Kwa hali ya kawaida kuna uwoga kwa wanaume wengi kuoa wanawake kama hao.
Mie niliapa siwezi kuoa mwanamke eti kwa uzuri wake bali awe na hali nzuri ya kiuchumi na akili. Kwa kweli hiyo imenisaidia sana. Leo nakamua na kakazi kangu kazuri Senior Lecturer Chuo Kikuu flani nje ya nchi na mama Senior HR katika sekata flani hapo bongo. Uendeshaji wetu wa familia umekuwa rahisi na mzuri sana kwa wote tunashirikiana in terms of kipato.
Jiulize kwanini maprofesa wengi wake zao ni mama wa nyumbani au wallimu wa upe?
huja challenge journal hata moja ............bali umezikubali ( yaweza kuwa bila ya kujua, but haufutiki ukweli kuwa unakubaliana nazo)
nilikuwa sijachungulia huku. kama unaona hutokewi na uko gado kiuchumi si wewe uanze hizo approach? si kuna wanaume wenye nazo pia? kwani lazima kusubiri wa hali ya kawaida? au unapenda kutoa amri na ukimpata mwenye uwezo mwenzako hamtakaa zizi moja. halafu mi nimetangaza nia humu jamvini kumbe kuna wadau kama wewe mpo mpo tu. ni PM tafadhaliWandugu za leo,
Hivi ukikutana na mwanamke umempenda na unatamani awe wako wa milele (kumuoa) lakini unakuta bahati nzuri (au mbaya kwa wengine) huyo mwanamke yuko safi kimaisha kazi nzuri kama pesa anazo kama mali anazo pia (sio hawa wamama watu wazima hapana wadada tu wenye umri unaofaa kuolewa) utamuoa hata kama wewe huna thamani ya kiuchumi aliyo nayo?
kwa nini nimeuliza hivi, kwa sababu katika mazungumzo ya kawaida tu jana kuna rafiki yangu akaniambia watu wataogopa kutangaza nia kwangu nikiendelea kujijenga kimaisha and it got me thinking.
Sasa wanaume utamuoa tu huyo dada hata kama wewe hali yako si fresh? na wadada utakuwa bread provider kwa huyo mumeo? mapenzi yana nafasi yake na pia uwezo kiuchumi una nafasi. zamani haikuwa hivi lakini kadri siku zinavyozidi kusonga mbele mambo yanabadilika
hizo mi sijakubaliana nazo!wewe tu ndo unalazimisha...!mimi kukubaliana na journal kunamaanisha wewe kupingana na journal zako
hehehe!hii sredi inaonekana teamo ndio starring
Hapa tunajadili journals au wanawake wenye hela zao?hizo mi sijakubaliana nazo!wewe tu ndo unalazimisha...!mimi kukubaliana na journal kunamaanisha wewe kupingana na journal zako
nilikuwa sijachungulia huku. kama unaona hutokewi na uko gado kiuchumi si wewe uanze hizo approach? si kuna wanaume wenye nazo pia? kwani lazima kusubiri wa hali ya kawaida? au unapenda kutoa amri na ukimpata mwenye uwezo mwenzako hamtakaa zizi moja. halafu mi nimetangaza nia humu jamvini kumbe kuna wadau kama wewe mpo mpo tu. ni PM tafadhali