Serengeti boy kamalizwa na lishangaziMwanamke aitwaye Pendo Medusela (37), mkazi wa Manispaa ya Shinyanga, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake, Timithoy Magesa (35), kwa kumkata kwa wembe sehemu mbalimbali za mwili wake kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, amebainisha hayo leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 23, mwaka huu, saa tatu usiku katika nyumba ya wageni ya Bwashee, iliyopo Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Amesema kabla ya mauaji hayo, Pendo alipigiwa simu na mwanamke mwingine kwa kutumia simu ya marehemu, akimuonya aachane naye kwa madai kwamba ndiye anayempenda. na baada ya muda Timothy alimtafuta Pendo na kumtaka wakutane katika nyumba ya wageni hiyo, ili wazungumze.
“Hata hivyo, walipokutana walianza kugombana kuhusu mwanamke aliyempigia simu, hali iliyosababisha Pendo kutumia wembe aliokuwa nao na kumkata Timothy sehemu mbalimbali za mwili na kuvuja damu nyingi,” amesema Kamanda Magomi.
View attachment 3452514
Mbona hujaacha nafasi kati ya neno na neno mkuu🤭KwaumriwaPendolazimaatakuaSingoMaza.
35 male : serengeti boySerengeti boy kamalizwa na lishangazi
Matumizi mabaya ya nyumba za wageni
Mnaenda kusuluhisha ugomvi nyumba ya wageni kweli?
Timothy alimtafuta Pendo na kumtaka wakutane katika nyumba ya wageni hiyo, ili wazungumze.
Hati kupigwa maweMbona hujaacha nafasi kati ya neno na neno mkuu🤭
Hili ni tatizo.😹😹😹 Swafiiiii
Mbona watu wanauga na wako vizuri tu wanaendelea tu kula bats as if they didn't killDhambi ya kuua iskiage hivyo hivyo,utapokea mateso pande zote.
Marehemu atakusumbua sana maisha yako yote...
Dunia/watu watakuweka angle mbaya mnoo...hta Kama hujaenda jela.
Mbaya zaidi Huyo aliyekuumba wewe na marehu anakusubiri kwa hamu yani.
Utakuwa hutulii huli wala kulala kwa amani maisha yako yote,yan hapa Duniani moto Akhera/mbinguni moto.
Dhambi ya kuua ni mbaya sana ndg zangu,usije ukajifanya siku una vihasira vyako vya kijinga ukamtoa mtu uhai wake,yan utapata matatizo makubwa mnoo, Hata ukitoroka ni kazi bure
Sana tuInasikitisha sana