Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
MWANAMKE HAWEZI KUWA MTIIFU KWA MWANAUME BWEGE, ASIYEJIELEWA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Vijana lazima mjue hili. Mkijizama data mtajua wenyewe.
Hakuna mwanamke aliyezaliwa mtiifu. Huyo mwanamke hayupo.
Utiifu umeamrishwa kwenye Dini na tamaduni kwa sababu sio jambo la asili.
Kisaikolojia huwezi kutii kitu unachokiona za kijinga, kibwege, kimezubaa, kipo chini ya viwango.
Mwanamke anapoambiwa awe mtiifu, utiifu upo kwa Mwanaume Mwenye Mamlaka.
Ukishakuwa na Mamlaka Mwanamke automatically atakutiii tuu.
Kuwa mwanaume hakukufanyi utiiwe. Uanaume ni jinsia. Ila majukumu na wajibu wa kiume ndio utafanya mkeo, watoto na familia yako ikutii. Sio kwa sababu unavaa suruali au makende yananing'inia kwenye kaptura.
Pili, mwanamke anatakiwa awe MSIKIVU.
Lakini kisaikolojia Usikivu upo kwa Mtu mwenye AKILI.
Ili mwanamke akusililize, awe msikivu itakupasa uwe na AKILI kumzidi.
Sio akili ndogo alafu utake kuzikilizwa. Unasililizwa kwa kipi. Huna unachoongea. Haoni tofauti yoyote kati yenu.
Unaongea Pumba muda wote. Kwa nini akusikilize.
Embu fikiria mkeo anamsikiliza Mchunga au Sheikhe au mganga kuliko wewe. Alafu huko kwa wachungaji wala hakuna vitu vya maana. Hujiulizi? Ni kwamba mwanamke amekuona hamnazo.
Niliwahi kupata kesi moja. Mwanamke anasema, mumewe akiongea anasikia aibu yeye. Yaani mwanaume huwezi kuwaza kwa Logic, unakurupuka, vitu vya kawaida hujui.
Kazi umbea umbea.
Vitu vya Simba na Yanga unavijua.
Vitu vya kina Diamond unavijua na unabishana.
Matatizo ya familia yako huyajui. Mambo ya Afya Basics tuu huyajui.
Mambo ya imani basics hujui.
Mambo ya Saikolojia ya wanawake na watoto basics hujui.
Mambo ya wanyama unaowafuga basics hujui.
Lakini upo busy kwenye vijiwe vya kahawa unapiga umbea mara Morison, sijui Chelsea, sijui Yanga imefanya nini. Miaka nenda rudi.
Mwanamke gani atamtii na kumsikiliza mwanaume Mjinga?
Wanawake ni kama Watoto. Mwanzoni mwa mahusiano saikolojia yao wanaamini kuwa Mwanaume wake(mumewe) anajua kila kitu. Yaani chochote unajua. Hiyo inawafanya wajihisi salama. Watakuuliza maswali mengi sana Mwanzoni.
Ni kosa la kiufundi kuwa mwanaume usiyejua Mambo hasa kwa level ya basic knowledge.
Wanawake wanapenda Wanaume Much Knows. Yaani kwenye maswali anayokuuliza mwanamke, asilimi zaidi ya sabini unatakiwa uwe na majibu yake.
Unaposema hujui zikawa nyingi. Mara usiniulize hayo maswali. Mara mimi sio Daktari au mwanasheria. Wakati swali dogo linahitaji tuu mantiki, akili ya kuzaliwa. Wanaanza kukudharau.
Alafu akukute unajadili vitu vya kijinga anaona hapa hamna Kitu.
Wanawake wana ile tabia, akiwa na wenzake utasikia akiwaambia, subiri nitamuuliza mume wangu(baba fulani au shemeji yenu). Na wako proud na hiyo hali au wanakupigia simu.
Unapokuwa hujui. Unaanza kutengeneza bomu. Imani yake kwako inapungua. Haoni umuhimu wa kukuuliza na kukushirikisha kwa sababu hauna msaada wowote.
Unapoambiwa uishi na mwanamke kwa Akili ni somo pana sana.
Wanawake hawahitaji utumie nguvu. Hata siku moja.
Ni ngumu sana kuishi na mwanamke ukiwa na akili ndogo. Kwa sababu wanawake hawapatani na ni wepesi kunusa hatari kama hiyo. Na wakishaona hatari hiyo wataanzisha vitimbi.
Ukiona mwanaume anasema mwanamke sijui mtawala sijui mwenye elimu kubwa, sijui mwenye pesa hawezi kuwa mke. Ujue huyo akili ni ndogo sana.
Kwa wanaume wenye Akili. Mwanamke ni mwanamke. Iwe anaelimu au hana, iwe tajiri au maskini. Iwe mtawala au asiyemtawala.
Mwanamke hata awe maskini kiasi gani atakuendesha tuu kama unatabia na akili za kibwege.
Na kama ni Mwanaume Timamu, unaakili zilizotimia. Mwanamke hata awe Rais wa nchi hawezi kukuendesha na wao wanajua hilo.
Atakunyenyekea, atakupenda, atakuwa mtiifu kwa sababu hayo ni mambo ambayo wanawake wote kiasili wameumbiwa hivyo.
Wanapenda kunyenyekea, kutii, kujidekezesha, kujishusha kwa wanaume halisi, wanaume wanaowapenda.
Yaani vile mwanamke anavyonyenyekea ndio anapenda. Ule ndio uanamke. Kujiliza, kujidekeza, kujiinamisha, kukutumikia, hayo wanayapenda sana lakini kamwe hawapendi kama sio kwa mtu sahihi.
Yaani mwanamke akuone hamnazo alafu ajishushe, hilo sahau. Atakudharau automatically.
Vijana, ni muhimu kuifanya Akili zenu ziwe Active. Jifunze Mambo mengi ya muhimu.
Kuwa mwanaume.
Uanaume ni chanzo.
Uanaume ni utatuzi wa changamoto.
Unapatwa na jambo. Usionyeshe panic. Mwambie unafuatilia. Kama jambo lipo nje ya ufahamu wako. Kajifunze. Uliza kwa wanaojua. Usitake mkeo ndio akaanze kutatuliwa matatizo yake na yenu na wanaume wengine kwa majina ya uchungaji, sijui usheikhe, sijui uganga, sijui mshauri gani huko.
Mwanaume ndiye mwenye jukumu la kutatua matatizo ya hapo nyumbani kwako.
Matatizo ya kisaikolojia. Mtibie mkeo.
Mjali, mpende, mpe moyo, mdekeze, mshirikishe, msikilize hata kama hutatekeleza kama unahoja zaidi, onyesha kwamba wewe ni Mume wake, wewe ni kichwa.
Wewe ni kichwa.
Haiwezekani mwili unawasha sehemu fulani. Alafu kichwa cha mtu mwingine ndio kinatambua hilo. Kwamba mguu wako unawasha, jikune.
Malalamiko mengi ya Wanawake kwenye ndoa hayahusiani na pesa hata kidogo.
Wanalalamikia
a) Wanaume uwezo mdogo kiakili.
Hili ndio kubwa zaidi kwani hilo linazaa haya mengine.
b) Wanaume kutowashirikisha Wake zao.
c) Wanaume kupenda ndugu na wazazi wao kuliko Wake zao.
Hizi zote ni tabia za wanaume mabwege.
Mtu asiyejua kwa nini ni Baba na Mume hawezi kuleta kizazi cha maana.
Mtu ambaye muda wote anawaza kwa nafasi ya mtoto badala ya kuwaza kama Mume au Baba.
d) ukosefu wa uaminifu.
Usaliti, meseji za mapenzi, na dharau. Hili ni tatizo jingine kubwa.
Ukiwa na tamaa basi uwe hata na Akili ya kuficha Mambo yako.
Upeo mdogo alafu unakimbizana na michepuko. Unaharibu maisha yako na familia yako kijinga.
Elewa, Ndoa ni muhimu kwa Mwanamke. Lakini Familia ni nguzo muhimu kwa Mwanaume. Kwani hiyo ndio himaya yake.
Vijana, msikubali kuwa MABWEGE.
Tumia Akili ili uishi maisha rahisi.
Nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa, Moshi Kilimanjaro