Mwanamke ilikuwaje hadi ukapigwa mmeo/bwana wako?Wewe mwanaume kwanini ulimpiga mama watoto/mchepuko wako?

Mwanamke ilikuwaje hadi ukapigwa mmeo/bwana wako?Wewe mwanaume kwanini ulimpiga mama watoto/mchepuko wako?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Sijawahi kupiga mtu anayeitwa mwanamke ila nimewahi kupigana,kupigwa na kupiga na wanaume wenzangu hii ni torati pale ninapoona nataka kufanyiwa uhuni na uwezo wa kupambana ninao huwa nakubali lolote lile litokee nipigwe,nipige au tupigane yote ni matokeo.

Nimeshuhudia mara kadhaa vidume vikishusha vipigo kwa wake zao bila huruma.

Nikiwa katika upangaji nimekaa nje kwenye mlango wa geto langu mida ya jioni basi kulikuwa na wapangaji wengine mme na mke.Jamaa yule aliwekewa maji ya kuoga bafuni na mke wake basi ile dume ikaenda kuoga na taulo huku kifua kiko wazi ilikuwa ni kawaida yake haijarishi hapo nje wapo watu wengi kiasi gani.

Basi siku hiyo baada ya kumaliza kuoga mke wake akiwa amekaa nje na mdada mwingine (mpangaji )jamaa yule aliteleza na kuanguka limbolo likawa nje tu acha mke wake acheke kwa sauti hata sisi tukawa tunacheka huku tukitoa pole huku tukicheka kwa sababu mke wake alicheka huku akikimbilia ndani kwa aibu ile njemba baada ya kuingia ndani dk1 nyingi tukasikia kilio na kipigo huku mlango umefungwa.

Mimi kama ilivyo torati huwa siingilii ugomvi wa wanandoa nikasepa nikaenda mtaani.Sikujua nini kiliendelea zaidi.

Jana usiku kwa jirani nimesikia kipigo na mwanamke analia kilugha kwa kichapo anachopokea bado sijajua sababu maana nimeamka mapema sana kuja kazini.Nina imani nikirudi wife ni sawa na cctiv camera yenye antena ya kunasa kila mawimbi lazima nitapewa tu huu ubuyu .


Kwako wewe mwanamke ulifanyaje hadi ukapigwa na mmeo na kipi kilisababisha wewe mwanaume ukampiga wife au mchepuko wako?



MJADALA HURU
 
Baada ya kusema mwanaume suruali. huku me ndo namkojoza mix matumizi na watoto sita juu
 
Back
Top Bottom