Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Anaandika, Robert Heriel
Mambo ya kubembelezana hakuna hapa. Kwanza muda mchache na maisha mafupi huo muda wa kubembelezana tutautoa wapi. Kama hawezi kukugharamia piga chini. Usiwe na jicho la huruma hata siku moja. Mimi kaka yenu, naam ndiye baba yenu ninaelewa ninachokisema. Hutaki acha wala sikubembelezi. Najua wakaidi wapo, na siku zote mkaidi hufaidi ukaidi wake.
Sifa moja ya mwanaume ni kula kwa jasho. Lazima ahenyeke iwe atumie nguvu nyingi au akili nyingi au atumie vyote. Mwanaume lazima alipie gharama huo ndio uanaume. Sio kupenda vya burebure kama demu.
Wanawake karibu wote moja ya swali atakalokuuliza katika yale maswali yao matatu ya awali ni hili, unajishughulisha na nini? Swali hilo ni muhimu na linalenga kuangalia namna utakavyoweza kugharamika.
Wanawake wa siku hizi wengi wenu mmezubaa zubaa kama uji wa mgonjwa, mnashindwa hata na kuku. Hamuoni mitetea inavyowasumbua majogoo, mnashindwa hata kuangalia viumbe wengine wanaishije. Jamani, nature inamtaka mwanaume asulubike, ahenyeke, avuje jasho ndio apata.
Tusulibisheni!
Tuhenyesheni!
Tutaabisheni!
Tukaangeni!
Jasho litutoke!
Nini mnaogopa, mnatuonea huruma sio? Mwanaume haonewi huruma. Unapomuonea huruma unampunguza uanaume wake. KAZI! KAZI!
Unatongoza demu leo, linakubali leo. Pumbavu kabisa! Kama jingajinga! Mpaka unajiuliza huyu ni mwanamke kweli au jitu gani!
Uanaume ni challenge.
Na wanawake wote wenye akili wanalijua hilo. Mwanamke mwenye akili na anayejitambua lazima ampe mwanaume challenge. Yaani amfanye mumewe aishi naye kwa akili.
Mwanaume hakuhudumii unachekacheka tuu kama boya! Asipokuhudumia wewe jua wewe hakupendi, tuseme hivi mpaka lini. Kama hakuhudumii wewe jua kuna mtu anamhudumia au kuna kitu anakipenda zaidi yako. Labda ni pombe, kuvaa au kula.
Nawafahamu wanaume wanaopenda pombe kuliko wake zao. Nawafahamu wanaume wanaopenda kula kuliko wake zao, yaani wanakula nyama choma huko mitaani halafu familia inahenyeka nyumbani. Taikon anawatambua kama wanaume wachoyo au walafi.
Wanawake pendeni vijana wachapakazi, wachakarikaji, na wanaobeba wajibu na majukumu yao. Mwanamke usikubali kusikia visingizio vya kijingajinga. Ni bora uwe na mwanaume muuza genge au bodaboda anayekuhudumia kuliko kuwa na mwanaume msomi mwenye visingizio.
Hata hivyo wanawake pia gharamikiweni kulingana na hadhi na madaraja yenu. Sio mtake gharama za juu wakati hadhi yako ya chini.
Ni bora usiolewe kabisa. Nasisitiza ni bora usiolewe kabisa kuliko kuishi na mwanaume asiyetaka kukugharamia.
Kuishi na mwanaume asiyetaka kulipa gharama nakuhakikishia utateseka tuu. Watoto wako watahenyeka tuu. Yaani utakuwa na familia masikini isiyotaka kugharamika.
Kumbuka upendo wa mwanaume ndio unatangulia kwako ndipo umtii na kumsikiliza. Kama hakupendi hakuna haja ya kumsikiliza na kumtii. Dunia ni hisabati. Yaani kila kitu kinaenda kwa mahesabu. Upendo huleta utiifu.
Na mtu hawezi kusema anakupenda kama hakuhudumii, never! Hakuna kitu kama hicho. Upendo ni gharama ya kumhudumia mtu. Upendo sio maneno.
Mwanaume lazima awajibike, anakutaka mwambie afuate protocol za kimapenzi. Aonyeshe kuwa anakupenda.
Zingatia upendo sio wingi wa mali au wapesa atakazokupa Ila thamani ya kile atakachokupa.
Mfano, Mwanaume uchumi wake ni let's say Kwa siku ni Tsh 5,000/= Kwa siku.
Alafu bado akawa anajitoa kwako Kwa hali na Mali licha ya kuwa pesa yake ni ndogo. Au anaelfu 30,000/= alafu akakupa elfu 20,000/= au yote kabisa. Huyo mkubalie muishi wote. Pesa yake ni ndogo lakini inathamani Kwa sababu kakupa bila hata kubakiza. Huyo anaweza kukugharamia.
Kuliko mtu mwenye milioni 5 alafu akupe laki 5, Huyo amekupa pesa nyingi lakini hazina thamani kama yule aliyekupa Tsh 30,000/=. Kugharamika ni kutoa Ile pesa inayouma, kuthamini mtu kuliko vitu. Yaani mtu anakuthamini wewe kuliko pesa zake. Huyo ndiye anayeweza kukugharamia na sio yule mwenye pesa au mali nyingi.
Upendo ni Kutoa/Utoaji. Na utoaji unapimwa kwa thamani ya kile kilichotolewa. Kinaweza kuwa kidogo lakini kikawa na thamani kubwa kuliko kile kikubwa. Sio ajabu wanawake wengi unaweza kumuona anapenda pesa lakini akaja kuolewa na mtu wa kawaida tuu tena asiye na lolote.
Pesa nyingi kwa mwanamke hazimfanyi akupende hata siku moja. Yaani umpe milioni 10 alafu ajue unabilioni moja😀😀 ataona humpendi.
Wanawake wengi hupenda kuchunguza mishahara ya waume zao, au vipato vya waume zao. Moja ya sababu ni kutaka kujua namna atakavyohudumiwa, lakini pia kuzuia wezi wa mali za mumewe lakini mwisho kupima kiwango cha mapenzi ya mumewe.
Mwanamke akijua mshahara wako labda ni laki tano, atalinganisha na huduma za pale nyumbani na vile unavyomhudumia alafu atatoa hesabu kuwa unampenda au humpendi.
Mke anaweza kukutetea kuwa Kwa kweli mumewe unajitahidi sana, unampenda, na unahangaika kwa ajili ya familia yenu, kama akijua kipato chenu na vile unavyowatunza. Mwanamke atajua unagharamia.
Lakini Mkeo anajua unalipwa milioni 5 lakini anazoziona ndani kwa Hesabu zake ni milioni moja ni rahisi kumsikia akilalamika kuwa hutunzi familia, hupendi familia yako. Na unashindwa kugharamikia familia yako.
Vijana wa siku hizi wanapenda vya bure bure jambo ambalo linaondoa uanaume wao. Mwanaume kamwe hawezi kukubali vitu vya burebure. Lazima ulipe Mahari, lazima umtunze mkeo, lazima uhakikishe mkeo ni kama mtoto wako. Akikosea muadhibu kwa upendo mama unavyoadhibu watoto wako wa kuwazaa. Sio unaadhibu kwa kumkomoa.
Raha ya mwanamke aringe, aombe pesa Kwa madeko na aibuaibu, kujishaua, asuse ili abembelezwe, ajifanye hataki kungonoka ili pawe na purukushani au atongozwe, apekue simu yako Kwa kujiiba akutane na meseji isiyoeleweka aanze kupata presha, akuite kesi ianze ujieleze hapo kwa kumsifu na kumpamba alivyomzuri na hakuna wakumfikia, pia eleza vile unavyopenda alivyomakini kulinda mali yake(wewe), mtoe out. Hivyo yaani.
Siku nyingine unamuwashia moto kelele mwanzo mwisho, anajiliza wewe hujali yaani motomoto! Kisha jioni unamwambia akusamehe kichwa yako haikuwa sawa😊😊, mwambie jinsi ulivyojisikia vibaya kwa ulivyomfokea, eleza jinsi biashara zinavyokuchanganya, mueleze jinsi alivyo na mchango mkubwa katika maisha yako hata kama haoni mchango huo, eleza umuhimu wake kwako.
Wanawake wanapenda sana kusikia hivyo. Huko pia ni kulipa gharama. Usifikiri unavyomgharamikia tuu kwa vitu na muda wako ndio iwe sababu ya kutoona umuhimu wake. Wanawake wanajiamini na kujiona safe Kwa wanaume wanaowahitaji, kwa wanaume wanaoona umuhimu wao katika maisha yao. Wanawake hawajiamini na hawajivunii mwanaume asiyeona umuhimu wao, asiye wahitaji.
Zingatia, kama mwanaume halipi gharama Kwa mtazamo wako ni bora umuache kuliko uwe malaya/yaani uwe na madanga alafu upo ni mshikaji. Sisi wanaume tunatabia zinazofanana. Unachomfamnyia mumeo tunakiona na mara nyingi tunatabia ya kumlipia mshikaji kisasi. Sio ajabu wanawake wengi huvunja ndoa kisa mshikaji wa pembeni atamuoa alafu ndoa ikishavunjika mshikaji naye anakimbia.
Mshikaji hawezi kukuheshimisha na kukugharamia alafu umdharau kisa mimi mchepuko wa nje tunayefanya dhambi alafu ati nije nikuoe, never ever. Hakuna mwanaume mwenye akili atakayekubali kukuchukua.
Nipumzike sasa!
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa Sasa Dar Es Salaam.