Watoto wa kike miaka hii mnaishi kwa hisia sana..... Yaani mnaishi maisha ya kutumia hisia badala uhalisia.
Ndio maana leo unaweza kwenda kuazima gari ya mtu, ukatafuta hela kidogo na ukamuomba rafiki yako nyumba yake na ukatumia hivi vitu kumpata mwanamke unaemtaka sababu wanaishi kwa hisia na kutaka vitu vya kusadikika.
Sikatai kuna vijana wa kiume ni wavivu sana na si watu wa kuchakalika. Ila sasa msigeuze hii kitu kuwa ni kila mtu yupo hivyo. Mpambanaji ni Mpambanaji tu kukosa au kupata ni matokeo. Sasa kwann mnalazimisha wanaume wote wafanane matokeo yaani wapate as if walichagua kukosa.
Kitendo cha mwanaume kukuchagua tu tayari ni ishara ya kuwa na interest na wewe, na ulipomkubalia ni ishara ya kukubali proposal yake ya kuwa nae.
Watoto wa kike wa siku hizi you lack proper training ya maisha na kuelewa ni wapi msaada wako unahitajika kwa huyu mwanaume anapohitaji. Wengi maisha hamyajui.
Unahisi wewe unapopigia simu michepuko yako unayoigawia mgegedo ikutumie hela basi na mwanaume anafanya hivyo hivyo?!
Huu ugumu wa sasa ni man made na sio natural. Ingekuwa tunaishi nyumba za tembe na kulima mahindi ndio maisha yameisha am sure 80% ya population ya vijana wa kibongo wangekuwa wameshaanza maisha ya familia. Ila balaa ni kwamba anatakiwa atafute hela ya kodi, umeme, mavazi, bili ya maji, usafiri, mawasiliano, michango ya ulinzi, harusi, na mambo mengine. Hivi vyote anatakiwa atafute mwenyewe na bado wewe hajakulipia bili zako za kipuuzi kama vikoba ambavyo huwa havimsaidii lolote mwisho wa siku.
Kimsingi mnataka watu waigizie maisha na wasiwe natural ili kuwafurahisha ninyi.
Kama ukitafiti vijana wa kiume wanaoamua kukaa mbali maswala ya ninyi wadangaji huwa wanafika mbali kimaisha kabla ya kuanza familia sababu pesa nyingi huwa wanawekeza katika kuwafurahisha na isiwe na faida mwisho wa siku.
Hebu rejeeni misingi ya kuwa mwanamke na vigezo vyake vya ukweli na muache usanii.