Mwanamke kuolewa ni muhimu na ni mafanikio makubwa au mtindo wa maisha mtu anaouchagua tu?

Naunga mkono hoja, [emoji106]
 
Kati ya kitu kikubwa kinacho drive maisha ya mwanadamu ni "a sense of belonging". Ile hali ya kujua here is a place i belong. Na ndoa ni sehemu mojawapo ambayo inatupa a sense of belonging. Ndio maana linakuwa ni hitaji la muhimu. Sasa ndoa katika maana yake halisi ni makubaliano kati ya wapenzi wawili kuishi pamoja mpaka kifo kiwatenganishe, On why do women crave on papers ni sababu ya maamuzi hasa ya kiuchumi ambayo "dunia imemmilikisha mwanaume" Suala la papers ni refu na lina mizizi yake kuliko ambapo linavyoonekana, Wakuu walikaa wakawaza na kuwazua.

Okay, hitaji la kupata a place where you belong linaenda mbali na kuhusisha mambo mengi kama Familia, Sehemu ya kuabudu, kijiwe cha kupiga stori, social clubs (kwa watu wa special groups), timu za michezo, etc.

Muulize mtoto aliyekulia mtaani juu ya anajisikiaje kutokuwa na familia, hakika majibu yake yatakuwa yakuhuzunisha sana. Na familia nyingi stage ya kwanza ni ndoa.
Ndoa ni muhimu lakini iwe ya watu wawili wenye malengo mamoja kitu ambacho ndicho chanzo cha furaha. Malengo hayo si lazima yawe malengo mazuri, hata yakiwa malengo mabaya ilimradi wote kwa pamoja ndicho kitu mlichokiazimia basi mtakuwa na furaha katika "umoja wenu huo". Mfano kuna ndoa za vibaka wawili, majambazi wawili, walevi wawili, wauaji wawili, ndoa ya wanasiasa wawili, wana harakati wawili etc. Ukiwachunguza sana utagundua ni watu wenye furaha sababu wamekubaliana katika hilo. (Compatibility)

Nataka kusema nini? Ndoa ni kitu kimoja kinachotakiwa kuwa na malengo mamoja, Ndoa moja yenye watu wawili wenye malengo tofauti kimbembe huwa kinaanzia hapo. A very simple mathematics.
 
Nukuu
Wanawake wanaanza maisha baada ya kuolewa full stop
 
Ndoa ni maelekezo ya Mwenye aliunda hiyo taasisi.

Wanadamu ni watekelezaji tu!
 
Super 👍🏽
 
Binafsi kuolewa sijakupa kipaumbele sana kwenye maisha yangu.
Watu wametoa makasiriko yao kwenye hii post sijui comment.
Wapenzi tulieni kidogo hii ni jf na sio maisha halisi naweza andika chochote najisikia, na sio kila kinacho andikwa humu ni kweli.
 
Ndoa ni kwajili ya familia, familia ni kwajili ya mwanamke.... jifunzeni hata kwa wanyama wasiooshwa ubongo.
 
Jibu liko kwa wanyama. Hii ndiyo tofauti baina ya wanyama na watu
 
wengine huwa wanaenda mpaka kwa waganga ngoja tusubiri maoni yao
 
katika siku sita Za Uumbaji
Mungu aliumba mbingu na dunia.(akatenganisha)
Mungu aliumba nuru na giza.(akatenganisha)
Mungu aliumba nchi kavu na bahari.(akatenganisha)
Mungu alimuumba;mwanaume na mwanamke (aliwaweka pamoja)

Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.”
KWAMBA NDOA/ KUISHI PAMOJA NI SHERIA YA ASILI, SIO SUALA LA KUTAFUTA HESHIMA. NI KAKAMILI MPANGO WA MUNGU (KWAMBA BILA NDOA HUJAKAMILIKA).NI HITAJI LA LAZIMA

SASA ENDELEA KUBISHANA NA ASILI
 
Ngoja nizungumze na kiongozi ili hii comment iwe pinned.
Binafsi nimeielewa na nimeipenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…