Maisha yana "fakes" nyingi sana kama pesa, mali, majumba, starehe.
Lakini kiuhalisia utakuja kugundua maisha yanahitaji LOVE ( UPENDO ), AMANI na FURAHA.
Ukiwa na mtu anayeweza:
- Kusimama na wewe katika nyakati ngumu,
- Kukutia moyo
- Kukupenda
Nakuhakikishia utahisi you have the world hata kama hujala siku 2
Ukitaka kujua hili, siku ukiwa very stressed au deppressed, hebu chukua simu yako mpigie mtu unayempenda, eithet awe:
- Mama
- Baba
- Mwanao
- Mpenzi
- Mjomba
- Rafiki
Utajihisi moyo unapoa tuliiii
Ndio maana hata wagonjwa, huko hospitalini akioneshwa upendo anakuwa poa mnooo.
Hii siri ya upendo, hamasa na matumaini inatumiwa sana na:
- Viongozi wa dini
- Motivational speakers
Hakuna jambo zuri kama kuambiwa Nakupenda, kutoka kwa mtu umpendae.
Ukiwa bado kijana, una nguvu mbwembwe zinakuwa nyingi. Ila itafikia stage hata kukaa mjini utaona kelele, hata ukiwa na majumba 600 utalala kwenye chumba kimoja. Na wakati huo utahitaji kuwa na mtu wa karibu siyo tena kampani za Bar na Night clubs.
Family! family! family! Is irreplaceable.
Vitu vingine kama midegree, sijui vyeo ni vitu artificial vya kutengeneza tu.