Bi zandile
JF-Expert Member
- Sep 12, 2024
- 459
- 1,155
Nimeona mjadala mkubwa wa Gen Z huko Tiktok kuhusu hii picha ya mtu aliyekuwa akiwananga huku akiwa amewashikia kiuno.
Vijana wanaulizana, kwani anatuchukuliaje?
Ilikuwa ni lazima aongee akitutaja sisi huku akiwa ametushikia kiuno?
Vijana wa kiume walienda mbali zaidi( ila mimi huko sitafika kwa ajili ya kulinda heshima ya jinsi yangu), lakini jambo hili limewashangaza sana.
Lakini mimi nimeng'amua mambo machache kwenye hii picha. Kwanza hii ni michezo ya kike tulikuwa tukiifanya utotoni kuringishia watoto wenzetu pale tulipokuwa tumenunuliwa nguo ama viatu vipya na wazazi wetu, nadhani na yeye amekumbushia utotoni kuturingishia kile anachodhani ni Madaraka makubwa ambayo wengine hawana.USHAMBA
Pili ni ishara tuliitumia zaidi sisi watoto wa kike kujihami hasa pale tulipokuwa tukihisi hatuko salama, tulikuwa tunashika kiuno huku tukijitikisa tikisa, lakini kiukweli ni kwamba ikitokea yule tuliyemuhofia anatusogolea tulikuwa tunatimua mbio.
Huyu mwanamke aliyeshika kiuno hapa anajaribu kujitikisa tikisa ili watu wasimsogee, anajua wakisogea zitamuokoa mbio. Yuko katika hatua ya mwisho kabisa ya anguko lake( The last kick of a dying horse.)...
Tukipuuze kiburi chake, ni kiburi cha kitoto ambacho hakitamsaidia kuvuka salama katika kipindi hiki.
Tumebakiza hatua moja mbele kuuangusha.
utawala haramu wa huyu kiumbe.Tusife moyo, TUMESHASHINDA HII VITA.