Ukitazama kwenye mahusiano ya watu wengi utagundua kuwa wanawake hudhania kumtii mwanaume,kusikiliza maagizo yake na kuyafanyia utekelezaji bila kuhoji maswali yasiyo ya lazima,kuwa msikilizaji mzuri na sio mzinguaji au mpinzani, kuwa mshirika na sio hasimu, hivi vyote kwao hudhania ni option kuvifanya kwa mwanaume.
Wao kuvifanya hivi ni hadi pale ambapo wanataka kupata kitu kwa mwanaume na ndipo huvaa usanii kama vile Kajala, Wema sepetu au irene Uwoya anavyoigiza kwenye bongo movie kuwa ni mke mwema asiyejua mwanaume mwingine nje ya mume wake.
Kwao kumtii mwanaume na kumpa heshima kama kiumbe waliyezidiwa nae hufanyika katika mazingira ya mali,wadhifa/cheo, na fedha kumzidi nje ya hapo watatumia nguvu nyingi kuonyesha mwanaume kuwa wao ni sawa au zaidi yake.
Kuwa fukara na mkeo miaka 5 utaona rangi zake zote. Ghafla pata contract ya milioni 300 na nyingine tofauti zikianza kuingia juu ya hiyo ya milioni 300 uone namna ghafla huyu mwanamke atakuwa mnyenyekevu,atakuwa na hofu ya kukukwaza, atatetemeka akisikia sauti yako na atakuwa analazimisha ukaribu na wewe kitandani.
Hii ikupe picha kuwa mwanamke kwake kuheshimu mwanaume huona ni option ambayo anaweza kuamua kuifanya pale atakapoona inafaa au anataka kufanya ili kupata kitu fulani.
Upande wa pili wanawake huamini mwanaume kuwapa matunzo,mali,fedha na hadhi ya mke ni jambo la lazima na bila hivyo ni bora uhusiano uvunjwe.
Leo hii mahusiano mengi yamevunjika kwasababu wanawake hawakupewa pesa wanazotaka, hawakupewa mali walizogombania. Kwao hivi vitu huamini wanaume hawana option ila kuwapa. Yaani mwanamke anaweza yeye akawa na milioni 5 wewe una milioni moja,akaona yeye ni lazima wewe umpatie sehemu ya pesa yako ambayo ni aslimia ndogo sana ya pesa aliyonayo ambayo ni nyingi kukuzidi na akaamini kuwa hauna option zlnyingine nje ya kumpatia alichotaka (ujinga wa karne).
Yeye ataona pesa zake ana option ya kukupa kama utampa zaidi au asikupe ila wewe hata kama hatakupa zaidi wala hatakupa chochote hauna option ila kumpatia ndio maana anataka ni lazima umpatie sababu haamini kuwa una option nyingine nje ya kumpa hiyo hela anayotaka.
Hii glorification ya tabia mbaya ya ubinafsi ifikie hatua ikemewe. Tukemee tabia mbaya zinazopewa jina la "ndivyo tulivyo".