Mwanamke kutojua kupika inaweza kuwa sababu ya kupewa talaka?

usija

usijali olewa na mimi tutakua tunakula hotelini hata watoto wakizaliwa tutakua tunakula nao hotelini
Kwa kipato gani mkuu. Mtakuwa hamfanyi vya maana nyie hela zenu zote mtakuwa mnazielekeza hotelini pekee.
 
Wapo sana, nawaonaga mim. Mdada mrembo akitoka umo ndani alivotupia mbona had raha.... Sasa aje akupikie wali tu na nyama, lol aibu, ubwabwa umekumbatiana hatari, uo mchuzi mwekunduuuuuu. Khaa jamani!!!!
Hahahaaa! Yashanikuta sehemu hayo Halafu chuzi lenyewe unakuta zito halichoteki unashindwa kujua kiazi kiko wapi na nyama yenyewe iko wapi yani vurugu tupu.
 
Kwa kipato gani mkuu. Mtakuwa hamfanyi vya maana nyie hela zenu zote mtakuwa mnazielekeza hotelini pekee.
😀😀 ni dhihaka tu hiyo mkuu kiukweli mwanamke wa hivyo hapaswi kabisa kuolewa😡
 
Mume wako atakuwa na raha sana. Hongera zako, ukibahatika kupata mke kama wewe basi ndoa utaiona bomba sana vinginevyo unaweza ukaichukia na kushangaa inakuwaje wengine wanakata miaka 20/30/40 na kuendelea ndani ya ndoa.

Kwi kwi kwi kwi lol! sasa huo wekundu wa mchuzi unasababishwa na nini? lol!...

Wapo sana, nawaonaga mim. Mdada mrembo akitoka umo ndani alivotupia mbona had raha.... Sasa aje akupikie wali tu na nyama, lol aibu, ubwabwa umekumbatiana hatari, uo mchuzi mwekunduuuuuu. Khaa jamani!!!!
 
Wengi wa hivyo wanakosa umakini , kushindwa kujiongeza na kutokujali pia. Na kama huyo utakuta kwa kujipara tu hajambo.
 
Ni aibu kwa binti wa Kitanzania kutojua kupika, na idadi ya wasiojua kupika siku hizi inazidi kuongezeka na chanzo ni life style.

Wengi wa hivyo wanakosa umakini , kushindwa kujiongeza na kutokujali pia. Na kama huyo utakuta kwa kujipara tu hajambo.
 
Cha usiku kitamu
Muhimu kujua

Alafu sio kama sijui kupika chakula kabisa ila nahisi sipo qualified enough
Kumbe ndio wewe hujui kupika jitahidi tu utajua maadamu unania utajua tu pia huenda sio kosa lako ni kosa la mama yako
 
Alikuwa busy sana na shule
Kasoma boarding schools. . .kamaliza chuo ndoa ikafuata ,hakuwa na muda wa kujifunza kazi za nyumbani
Hajataka tu kujifunza kupika mana sio kwamba miaka yote hapati hata likizo akarudi nyumbani.

Mi nakumbuka kipindi niko nyumbani ule muda wa likizo mama alikuwa anaweka zamu ya kupika kuanzia vitafunwa vya asubuhi mpaka jioni ambapo kila mtu lazima ataingia jikoni utake usitake na hiyo ilikuwa dawa japo kwa muda mfupi lakini kwa upande fulani ilitusaidia sana.
 
Mume wako atakuwa na raha sana. Hongera zako, ukibahatika kupata mke kama wewe basi ndoa utaiona bomba sana vinginevyo unaweza ukaichukia na kushangaa inakuwaje wengine wanakata miaka 20/30/40 na kuendelea ndani ya ndoa.
Shukrani
 
Reactions: BAK
Ni aibu kwa binti wa Kitanzania kutojua kupika, na idadi ya wasiojua kupika siku hizi inazidi kuongezeka na chanzo ni life style.
Wengi wanajikweza na kusahau kuwa hawataweza kuja kuwa na maisha yao hapo baadae pia wakijijenga kichwani kwamba hata ikitokea akiolewa ataajiri housegirl ambaye atakuwa anampikia kumbe sivyo.
 
Kabisa.... Ni malezi
 
....More details needed. Did he know, wali date na hawakuwahi kutembeleana na kupikiana ?
Chakula gani basic, chai, uji au biriani ?. Hata kutumia rice cooker ??

In general kwangu sio big deal kabisa ingawa inashangaza dunia hii ya kibantu km mwanamke hajui kupika hata basic meal, wali, mboga ect. Hata chai mmnunue hotelini ??
 
Kujua kupika ni muhimu sana na inapendeza. Si lazima iwe kwa ajili ya mume, hata kwa ajili yako pia. Kwani wewe hupendi kujipikia vyakula tofauti tofauti, vyakula vizuri na vitamu?
 
Mwanamke kutojua kupika ni aibu, mi mwny dem wang alkuw hajui kupika ila kwa vle nampenda then najua kupika nlianza kumfundsha taratb mpk akajua had xaiv huwa namfundisha. Yeye chakula alichokuw anajua kupika ni pilau tu, vngne vyote hajui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…