Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Maafisa wa forodha nchini India wamemkamata mwanamke mmoja raia wa Kenya mwenye umri wa miaka 43 kwa kosa la kusafirisha kilo 1.7 za kokeini zenye thamani ya kati ya Ksh225 milioni na Ksh300 milioni.
Kwa mujibu wa The Indian Express, mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Emily Rodha alikamatwa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chhatrapati Shivaji Maharaj mjini Mumbai Jumanne.
Taarifa zinaonyesha alikuwa akisafirisha dawa hizo haramu kutoka Nairobi hadi Delhi kupitia Doha. Wakati wa kuhojiwa na maafisa wa forodha Emily alikiri kukabidhiwa shehena hiyo na mwanamke mwingine jijini Nairobi na kuahidiwa kiasi cha Ksh100,000, iwapo ataufikisha mzigo huo Delhi.
Haya yakijiri, wakati Mkenya mwengine Margaret Nduta, amehukumiwa adhabu ya kifo baada ya kupatikana na kosa la kusafirisha madawa ya kulevya huko Vietnam.
Chanzo.Trt Swahili