NADHARIA Mwanamke kuwa katika Hedhi inasababisha kunyauka kwa mboga na matunda

NADHARIA Mwanamke kuwa katika Hedhi inasababisha kunyauka kwa mboga na matunda

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Kuna madai mengi mtaani yanayosema kuwa mwanamke akiwa kwenye hedhi husababisha kunyauka kwa mboga na matunda ikitokea amechuma. Mdau mmoja wa JamiiForums amendika pia kuhusu suala hili.

Menstruation.jpg


Baadhi ya tamaduni huwazuia kabisa wanawake wasichume vitu hivyo. Kisayansi, madai haya yana ukweli?
 
Tunachokijua
Hedhi ni tendo la kiasili na kibaiolojia linalotokea kwa mwanamke baada ya kufikia umri wa kuvunja ungo. Tendo hili huwa na umuhimu mkubwa katika kupima uimara wa afya ya uzazi ya mwanamke. Huundwa kwa damu, ute wa mlango wa kizazi, majimaji ya uke, tishu za mji wa uzazi, madini ya chuma, sodium, calcium, phosphate na chloride

Kwa mujibu wa UNICEF, 26% ya wanawake wote duniani wapo kwenye umri unaoruhusu tendo hili litokee maishani mwao.

Tamaduni za nchi nyingi duniani huchukulia hedhi kama jambo lisilofaa kutokana na uwepo wa nadharia nyingi zisizo na uthibitisho wa kisanyansi. Utafiti uliofanywa na UNICEF kwenye nchi za Afghanistan, Bangadesh, Ethiopia, Ghana na Indonesia unathibitisha ukubwa wa tatizo hili. Mfano nchini Afghanistan, wasichana hukatazwa kula nyama, mboga za majani pamoja na kunywa maji ya baridi. Aidha, hukatazwa pia kuosha vyombo na nguo.

Kwa Tanzania, tamaduni za jamii nyingi hukataza wasichana kuchuma mboga wala pilipili, baadhi hukatazwa kubeba mtoto mchanga kwa madai ya kumdhuru au hata kumsababishia homa na maambukizi na wengine huambiwa kukaa mbali na Wanyama kwa kuwa wanaweza kushambuliwa nao. Hii ni mifano michache tu kati ya mingi.

Ukweli wake kisayansi
Kisayansi, tendo la hedhi haliwezi kwa namna yoyote ile kukausha mboga, kupukutisha pilipili, kuchafua maji pamoja na kusababisha maambukizi ya aina yoyote kwa mtoto mchanga. Hizi ni nadharia zisizo na mashiko kisayansi.

UNICEF na WHO wanataja ukosefu wa elimu ya kutosha kwenye jamii zetu kama chanzo namba moja kinachofanya mitazamo na nadharia hizi ziendelee kushika kasi kwenye jamii zetu.

Kisayansi, madai haya sio sahihi. Hedhi ni kitu kinachopaswa kuchukuliwa kama jambo la kawaida kwenye maisha ya binadamu na baadhi ya wanyama kwani ndiyo msingi wa muendelezo wa kuuleta uhai mpya duniani.

Kwa msingi wa hoja hizi umejijenga kiimani, JamiiForums inachukulia suala hili kama nadharia inayopaswa kuchunguzwa zaidi ili kupata uthibitisho unaoweza kupimwa kwa njia zilizo wazi.
Hatuwaonei ni nature Yao, kasome maandko ww, mchaichai uko sensitive na mambo ya hovyo hata mtu mzinifu akiupanda hauoti
😂😂😂😂😂 Daaah yaani kuna rafiki ni mzinzi huyoo kila siku ni kubadilisha wanawake anafuga kuku na kutotolesha vifaranga na hapo kwake kapanda michai chai kibao na inakuwa kila siku kama unaamini hivyo kwako ni sawa
 
😂😂😂😂😂 Daaah yaani kuna rafiki ni mzinzi huyoo kila siku ni kubadilisha wanawake anafuga kuku na kutotolesha vifaranga na hapo kwake kapanda michai chai kibao na inakuwa kila siku kama unaamini hivyo kwako ni sawa
Labda anaingia kwenye bustani yake baada ya kuoga!!
 
Labda anaingia kwenye bustani yake baada ya kuoga!!
Sasa ueleweki umesema mtu mzinifu kwani ukioga uzinzi unakuwa umetoka au? Au unazungumzia mtu aliyetoka kufanya mapenzi akaenda kupanda mchai chai ndo hauoti mkuu haieleweki😂😂
 
Hedhi ni tendo la kiasili na kibaiolojia linalotokea kwa mwanamke baada ya kufikia umri wa kuvunja ungo. Tendo hili huwa na umuhimu mkubwa katika kupima uimara wa afya ya uzazi ya mwanamke.

Kwa mujibu wa UNICEF, asilimia 26 ya wanawake wote duniani wapo kwenye umri unaoruhusu tendo hili litokee maishani mwao.

Tamaduni za nchi nyingi duniani huchukulia hedhi kama jambo lisilofaa kutokana na uwepo wa nadharia nyingi zisizo na uthibitisho wa kisanyansi. Utafiti uliofanywa na UNICEF kwenye nchi za Afghanistan, Bangadesh, Ethiopia, Ghana na Indonesia unathibitisha ukubwa wa tatizo hili.Mfano nchini Afghanistani, wasichana hukatazwa kula nyama, mboga za majani pamoja na kunywa maji ya baridi.

Aidha, hukatazwa pia kuosha vyombo na nguo.

Kwa Tanzania, tamaduni za jamii nyingi hukataza wasichana kuchuma mboga wala pilipili, baadhi hukatazwa kubeba mtoto mchanga kwa madai ya kumdhuru au hata kumsababishia homa na maambukizi pa wengine huambiwa kukaa mbali na Wanyama kwa kuwa wanaweza kushambuliwa nao. Hii ni mifano michache tu kati ya mingi.

Huuu uzi wakitambo lkn una mantiki sana, hiyo ishu imekaa kiimani sana,,ipo nadharia kwamba ukifanya jambo lakumchukiza mwanamke ambaye yupo kwenye hedhi ,basi siku nzima inaweza kuwa na mikosi,, inaenda sambamba na mwanamke anaye nyonyesha na mjamzito kuishinao Kwa machukizo lazima kuandamwa na mikosi,, Mimi nadhan ni Imani zaidi
 
Ingawa naiamini sana sayansi lakini hili jambo nimelishuhudia ni kweli kabisa.
Kule kijijini achana na na watu wakio hedhini lakini kuna wale wanajijua kabisa akichuma mboga, imekwenda na maji. Hata akija kwako akiipenda mboga ataomba umchumie mwenyewe.
 
Naomba kuuliza juu ya hili suala la je Kuna uhusiano gani kati ya mimea na hedhi nimepanda mchai chai wakati nauchukua nilipewa maelekezo kua mwanamke asichume akiwa na hedhi endapo ata chuma basi mmea huo utauka baada kufatilia nikagundua kua hata wamiliki wa bustani za mboga wanafuata maelekezo hayo. Inaoenaka kuna nguvu za giza kwenye hiyo damu
 
Duniani Kuna mambo hata macho nayo yanamadhara sio hedhi , wengine wakiangalia mazao , mboga , hata kusifia baada ya siku unakuta kitu kimeanza kuharibika kama ni mboga imeanza kukauka.
Kingine kwenye bible wanasema mwanamke akiwa hedhi anakuwa ni najisi , hata yule ambaye atamshika nae pia anakuwa najisi, , inawezekana akishika mboga anainajisi mpaka inakauka.
 
Naomba kuuliza juu ya hili suala la je Kuna uhusiano gani kati ya mimea na hedhi nimepanda mchai chai wakati nauchukua nilipewa maelekezo kua mwanamke asichume akiwa na hedhi endapo ata chuma basi mmea huo utauka baada kufatilia nikagundua kua hata wamiliki wa bustani za mboga wanafuata maelekezo hayo. Inaoenaka kuna nguvu za giza kwenye hiyo damu
Nguvu ya Imani ni ya ajabu, once you belive it happens... 😁 😁
 
Uislam hautaki aingie msikitini au afanye ibada . Huwa anasamehewa akiwa katika hali hiyo.Pia hauruhusiwi kumuingilia mkeo kwenye hali hiyo.So mimi binafsi sihitaji kujua sana kwanini mboga zinaungua ila Mungu mwenyewe aliyewaumba kawapa udhuru inatosha kuwa kuna siri kubwa na damu ya nifas au hedhi.
 
Hiyo sayansi yenu isiwafanye kuwa vipofu wa kifikra!... Na kuacha kuamini nature...

Hii hapa chini nimeambatanisha picha... Ni michaichai mitatu niliyoipanda siku 1 niliyoipanda Mimi mwenyewe!

Nikawa naimwagilia na kuipa mbolea ya samadi...

Mchaichai wa kwanza sikutaka mtu auguse!...niliufunika na neti...

Ili nije kujithibitishia mwenyewe huo uhalisia sayansi inaouita nadharia!

Msipende kuamini sayansi... Kuna nguvu isiyoonekana kuizidi hiyo sayansi!

Angalia tofauti sasa ya hiyo michaichai hapa chini! 👇 Mmoja umedumaa, mmoja niliouwekea uangalizi... Uko sawa kabisa!

Vitu vingine havihitaji ubishi! Wala kumsubiri Yesu ndio aje athibitishe!!!
 

Attachments

  • 20240105_185304-1.jpg
    20240105_185304-1.jpg
    1.9 MB · Views: 19
Utafiti wa kisayansi hauna mwisho, naamini miaka ijayo watapata jibu juu ya hili.

Mi binafsi sikuwahi kuiamini nadharia hii, lakini nimeshuhudia kwenye bustani yangu.

Pilipili kichaa, pilipili mbuzi na mwendo kasi zimekauka kwa nyakati tofauti baada jirani kuruhusiwa kuchuma akiwa kwenye hedhi.
Mchaichai umenyauka baada ndugu wa familia kukata majani yake akiwa kwenye hali hiyo.

Hata hivyo hili halitokei kwa kila mwanamke.
Ni baadhi tu ya wanawake.
 
Back
Top Bottom