NADHARIA Mwanamke kuwa katika Hedhi inasababisha kunyauka kwa mboga na matunda

NADHARIA Mwanamke kuwa katika Hedhi inasababisha kunyauka kwa mboga na matunda

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Kuna madai mengi mtaani yanayosema kuwa mwanamke akiwa kwenye hedhi husababisha kunyauka kwa mboga na matunda ikitokea amechuma. Mdau mmoja wa JamiiForums amendika pia kuhusu suala hili.

Menstruation.jpg

Baadhi ya tamaduni huwazuia kabisa wanawake wasichume vitu hivyo. Kisayansi, madai haya yana ukweli?
 
Tunachokijua
Hedhi ni tendo la kiasili na kibaiolojia linalotokea kwa mwanamke baada ya kufikia umri wa kuvunja ungo. Tendo hili huwa na umuhimu mkubwa katika kupima uimara wa afya ya uzazi ya mwanamke. Huundwa kwa damu, ute wa mlango wa kizazi, majimaji ya uke, tishu za mji wa uzazi, madini ya chuma, sodium, calcium, phosphate na chloride

Kwa mujibu wa UNICEF, 26% ya wanawake wote duniani wapo kwenye umri unaoruhusu tendo hili litokee maishani mwao.

Tamaduni za nchi nyingi duniani huchukulia hedhi kama jambo lisilofaa kutokana na uwepo wa nadharia nyingi zisizo na uthibitisho wa kisanyansi. Utafiti uliofanywa na UNICEF kwenye nchi za Afghanistan, Bangadesh, Ethiopia, Ghana na Indonesia unathibitisha ukubwa wa tatizo hili. Mfano nchini Afghanistan, wasichana hukatazwa kula nyama, mboga za majani pamoja na kunywa maji ya baridi. Aidha, hukatazwa pia kuosha vyombo na nguo.

Kwa Tanzania, tamaduni za jamii nyingi hukataza wasichana kuchuma mboga wala pilipili, baadhi hukatazwa kubeba mtoto mchanga kwa madai ya kumdhuru au hata kumsababishia homa na maambukizi na wengine huambiwa kukaa mbali na Wanyama kwa kuwa wanaweza kushambuliwa nao. Hii ni mifano michache tu kati ya mingi.

Ukweli wake kisayansi
Kisayansi, tendo la hedhi haliwezi kwa namna yoyote ile kukausha mboga, kupukutisha pilipili, kuchafua maji pamoja na kusababisha maambukizi ya aina yoyote kwa mtoto mchanga. Hizi ni nadharia zisizo na mashiko kisayansi.

UNICEF na WHO wanataja ukosefu wa elimu ya kutosha kwenye jamii zetu kama chanzo namba moja kinachofanya mitazamo na nadharia hizi ziendelee kushika kasi kwenye jamii zetu.

Kisayansi, madai haya sio sahihi. Hedhi ni kitu kinachopaswa kuchukuliwa kama jambo la kawaida kwenye maisha ya binadamu na baadhi ya wanyama kwani ndiyo msingi wa muendelezo wa kuuleta uhai mpya duniani.

Kwa msingi wa hoja hizi umejijenga kiimani, JamiiForums inachukulia suala hili kama nadharia inayopaswa kuchunguzwa zaidi ili kupata uthibitisho unaoweza kupimwa kwa njia zilizo wazi.
Kuna madai mengi mtaani yanayosema kuwa mwanamke akiwa kwenye hedhi husababisha kunyauka kwa mboga na matunda ikitokea amechuma. Mdau mmoja wa JamiiForums amendika pia kuhusu suala hili.

View attachment 2623539

Baadhi ya tamaduni huwazuia kabisa wanawake wasichume vitu hivyo. Kisayansi, madai haya yana ukweli?

Hili ni jambo la kweli kabisa ila sababu ya wengi kutotaka kulielewa hawataelewa.
Kwa wale waumini wa dini kubwa duniani tumefundishwa mengi kuhusu hedhi

Kwa wakristo ni sehemu moja tuu kwenye bible Yesu alitamka kuwa nguvu zimemtoka - Pale alipoguswa vazi lake na mwanamke aliyekuwa kwenye hedhi

Luke 8: 43-46​

Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote, alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.​

Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga.​

Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka."​

Sare ndio TUJUE sio kuchuma mboga tuu, hata ukimwingilia mwanamke akiwa kwenye hedhi unanyauka

Hata kuhudumiwa kama kupikiwa na mwanamke aliye kwenye hedhi sio salama

Wake zenu, dada zenu na watoto zenu wakiwa kwenye hedhi wapumzisheni tena nyie ndio muwahudumie
🤓🤓🤓🤓
 
Naomba kuuliza juu ya hili suala la je Kuna uhusiano gani kati ya mimea na hedhi nimepanda mchai chai wakati nauchukua nilipewa maelekezo kua mwanamke asichume akiwa na hedhi endapo ata chuma basi mmea huo utauka baada kufatilia nikagundua kua hata wamiliki wa bustani za mboga wanafuata maelekezo hayo. Inaoenaka kuna nguvu za giza kwenye hiyo damu
ni mboga tu au
 
Hili ni jambo la kweli kabisa ila sababu ya wengi kutotaka kulielewa hawataelewa.
Kwa wale waumini wa dini kubwa duniani tumefundishwa mengi kuhusu hedhi

Kwa wakristo ni sehemu moja tuu kwenye bible Yesu alitamka kuwa nguvu zimemtoka - Pale alipoguswa vazi lake na mwanamke aliyekuwa kwenye hedhi

Luke 8: 43-46​

Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote, alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.​

Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga.​

Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka."​

Sare ndio TUJUE sio kuchuma mboga tuu, hata ukimwingilia mwanamke akiwa kwenye hedhi unanyauka

Hata kuhudumiwa kama kupikiwa na mwanamke aliye kwenye hedhi sio salama

Wake zenu, dada zenu na watoto zenu wakiwa kwenye hedhi wapumzisheni tena nyie ndio muwahudumie
🤓🤓🤓🤓
Asante mkuu kwa hili neno.
Ubarikiwe 🙏🙏
 
Kisayansi, madai haya siyo sahihi. Hedhi ni kitu kinachopaswa kuchukuliwa kama jambo la kawaida kwenye maisha ya binadamu na baadhi ya wanyama kwani ndiyo msingi wa muendelezo wa kuuleta uhai mpya duniani.[emoji1545][emoji1752]
Hawaonewi Kaka. Tusibishe kla ktu. Mke wng yupo kwny siku zake leo nimeongea nae khs hil kasema n kwel anajua kuwa akiwa hvyo kuna mboga za majan akchuma znakauka

So n kwel mzee. Let the nature take place tuheshimu uumbaj w Mungu. Kuna ktu kwny damu ya Hedhim damu ya uzazi n.k
 
Semeni hivii sayansi haijapata ufumbuzi wa hiyo nadharia kwamba bado inaendlea kufanyiwa uchunguzi sio kukanusha kwamba sayansi inalikataa hlo jambo, labda miaka ijayo ltapata uthibitisho kupitia sayansi hyohyo utajuaje
Kuna connection gani kati ya hedhi na pilipili kunyauka? Tusaidie kwa faida ya wengi.
 
Hawaonewi Kaka. Tusibishe kla ktu. Mke wng yupo kwny siku zake leo nimeongea nae khs hil kasema n kwel anajua kuwa akiwa hvyo kuna mboga za majan akchuma znakauka

So n kwel mzee. Let the nature take place tuheshimu uumbaj w Mungu. Kuna ktu kwny damu ya Hedhim damu ya uzazi n.k
Kuna connection gani mkuu kati ya hedhi na mboga? Ndio tunataka kufahamu wengi.
 
Mbona ni kweli shida hawa wanasayansi wanapingana na asili ko nilazima wakanushe tu wakikubali tayari inakuwa siyo sayansi tena m nmeshashuhudia mara kibao tu mbona
 
imani potofu, hedhi ni dalili ya uhai - hedhi ni baraka !! kumbuka lile ni yai ambalo limekosa rutubisho hivyo linajitoa kuweka mazingira saafi ili yai jingine lisongee ...
Mkeo au mpenzi wako akiwa kwa hedhi ndiyo wakati mzuri wa kumkubatia - mpe penzi loote mahaba ya kumwaga - ile ni suna.
Nyie ndio mnaoishiaga kujinyonga tu maana mnaamini upande mmoja tu hili jambo lishafanyiwa tafit na lina ukweli hadi wao wanawake wanakili ni kweli wewe ni nani kuna mambo mengne hayana majibu ya kisayansi kama ng'ombe tu kula majani harafu akatoa maziwa....
 
kuna vitu vingine sayansi haifui dafu hata uchawi sayansi haiutambui kabisa na uchawi upo.

kwa hio watu wanaoamini katika sayansi peke yake wanapitwa na mengi sana
 
Wanasema kuna baadhi ya mimea, siyo yote!! Mie nilifanya jaribu kwenye mbaazi!!

Alichuma jani akiwa kwenye siku zake na nikauweka alama!! Haukuzaa ule mbaadhi na afya yake ilikiwa dhoofu sana mpaka ukafa mapema sana kabla ya mingine!!
 
Kuna madai mengi mtaani yanayosema kuwa mwanamke akiwa kwenye hedhi husababisha kunyauka kwa mboga na matunda ikitokea amechuma. Mdau mmoja wa JamiiForums amendika pia kuhusu suala hili.

View attachment 2623539

Baadhi ya tamaduni huwazuia kabisa wanawake wasichume vitu hivyo. Kisayansi, madai haya yana ukweli?
Kuwahi shuhudia sijawahi ingawa nimesikia mara kadhaa kwa majirani kuwa hali hiyo hutokea
 
Back
Top Bottom