NADHARIA Mwanamke kuwa katika Hedhi inasababisha kunyauka kwa mboga na matunda

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Hatuwaonei ni nature Yao, kasome maandko ww, mchaichai uko sensitive na mambo ya hovyo hata mtu mzinifu akiupanda hauoti
😂😂😂😂😂 Daaah yaani kuna rafiki ni mzinzi huyoo kila siku ni kubadilisha wanawake anafuga kuku na kutotolesha vifaranga na hapo kwake kapanda michai chai kibao na inakuwa kila siku kama unaamini hivyo kwako ni sawa
 
😂😂😂😂😂 Daaah yaani kuna rafiki ni mzinzi huyoo kila siku ni kubadilisha wanawake anafuga kuku na kutotolesha vifaranga na hapo kwake kapanda michai chai kibao na inakuwa kila siku kama unaamini hivyo kwako ni sawa
Labda anaingia kwenye bustani yake baada ya kuoga!!
 
Labda anaingia kwenye bustani yake baada ya kuoga!!
Sasa ueleweki umesema mtu mzinifu kwani ukioga uzinzi unakuwa umetoka au? Au unazungumzia mtu aliyetoka kufanya mapenzi akaenda kupanda mchai chai ndo hauoti mkuu haieleweki😂😂
 
Huuu uzi wakitambo lkn una mantiki sana, hiyo ishu imekaa kiimani sana,,ipo nadharia kwamba ukifanya jambo lakumchukiza mwanamke ambaye yupo kwenye hedhi ,basi siku nzima inaweza kuwa na mikosi,, inaenda sambamba na mwanamke anaye nyonyesha na mjamzito kuishinao Kwa machukizo lazima kuandamwa na mikosi,, Mimi nadhan ni Imani zaidi
 
Semeni hivii sayansi haijapata ufumbuzi wa hiyo nadharia kwamba bado inaendlea kufanyiwa uchunguzi sio kukanusha kwamba sayansi inalikataa hlo jambo, labda miaka ijayo ltapata uthibitisho kupitia sayansi hyohyo utajuaje
Apo sawa
 
Ingawa naiamini sana sayansi lakini hili jambo nimelishuhudia ni kweli kabisa.
Kule kijijini achana na na watu wakio hedhini lakini kuna wale wanajijua kabisa akichuma mboga, imekwenda na maji. Hata akija kwako akiipenda mboga ataomba umchumie mwenyewe.
 
Naomba kuuliza juu ya hili suala la je Kuna uhusiano gani kati ya mimea na hedhi nimepanda mchai chai wakati nauchukua nilipewa maelekezo kua mwanamke asichume akiwa na hedhi endapo ata chuma basi mmea huo utauka baada kufatilia nikagundua kua hata wamiliki wa bustani za mboga wanafuata maelekezo hayo. Inaoenaka kuna nguvu za giza kwenye hiyo damu
 
Duniani Kuna mambo hata macho nayo yanamadhara sio hedhi , wengine wakiangalia mazao , mboga , hata kusifia baada ya siku unakuta kitu kimeanza kuharibika kama ni mboga imeanza kukauka.
Kingine kwenye bible wanasema mwanamke akiwa hedhi anakuwa ni najisi , hata yule ambaye atamshika nae pia anakuwa najisi, , inawezekana akishika mboga anainajisi mpaka inakauka.
 
Nguvu ya Imani ni ya ajabu, once you belive it happens... 😁 😁
 
Uislam hautaki aingie msikitini au afanye ibada . Huwa anasamehewa akiwa katika hali hiyo.Pia hauruhusiwi kumuingilia mkeo kwenye hali hiyo.So mimi binafsi sihitaji kujua sana kwanini mboga zinaungua ila Mungu mwenyewe aliyewaumba kawapa udhuru inatosha kuwa kuna siri kubwa na damu ya nifas au hedhi.
 
Hiyo sayansi yenu isiwafanye kuwa vipofu wa kifikra!... Na kuacha kuamini nature...

Hii hapa chini nimeambatanisha picha... Ni michaichai mitatu niliyoipanda siku 1 niliyoipanda Mimi mwenyewe!

Nikawa naimwagilia na kuipa mbolea ya samadi...

Mchaichai wa kwanza sikutaka mtu auguse!...niliufunika na neti...

Ili nije kujithibitishia mwenyewe huo uhalisia sayansi inaouita nadharia!

Msipende kuamini sayansi... Kuna nguvu isiyoonekana kuizidi hiyo sayansi!

Angalia tofauti sasa ya hiyo michaichai hapa chini! 👇 Mmoja umedumaa, mmoja niliouwekea uangalizi... Uko sawa kabisa!

Vitu vingine havihitaji ubishi! Wala kumsubiri Yesu ndio aje athibitishe!!!
 

Attachments

  • 20240105_185304-1.jpg
    1.9 MB · Views: 19
Utafiti wa kisayansi hauna mwisho, naamini miaka ijayo watapata jibu juu ya hili.

Mi binafsi sikuwahi kuiamini nadharia hii, lakini nimeshuhudia kwenye bustani yangu.

Pilipili kichaa, pilipili mbuzi na mwendo kasi zimekauka kwa nyakati tofauti baada jirani kuruhusiwa kuchuma akiwa kwenye hedhi.
Mchaichai umenyauka baada ndugu wa familia kukata majani yake akiwa kwenye hali hiyo.

Hata hivyo hili halitokei kwa kila mwanamke.
Ni baadhi tu ya wanawake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…