Mwanamke Masikini, Mama Pendo (Single Mother wa Watoto Wawili) wa Tageta Machinjioni anavunjiwa Banda lake Saa Hii: Tumsaidie Mamlaka kuingilia kati

Mwanamke Masikini, Mama Pendo (Single Mother wa Watoto Wawili) wa Tageta Machinjioni anavunjiwa Banda lake Saa Hii: Tumsaidie Mamlaka kuingilia kati

Wanabodi
Nimepigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Mama Pendo akiomba msaada wa haraka,anavunjiwa kibanda chake cha kuishi eneo la Tageta Machinjioni。

Anaomba media tupaze sauti wenye mamlaka wasikie wamsaidie kumnusuru。

Please tumsaidie huyu Mtanzania mwenzetu ambaye ni masikini wa kutupwa ambaye pia ni single mother wa watoto wawili。

Saa hii, anavunjiwa banda lake hapo Tageta Machinjioni na mtu anayedai ndie mmiliki wa banda hilo。

Number yake ni 0656104986,kama kuna mtu anaweza。kusaidia lolote please do。

Paskali
CC Waziri Dkt. Gwajima D
Dah, sadness
 
Hii nchi haiishi vituko..., Sasa wewe mdau wa Media unless umekuwa ukiishi under the rock somewhere na leo ndio umetoka utakuwa unajua kwamba kina mama Pendo wapo wengi... Sasa tuendelee kupaza sauti kila Mama Pendo au Sikudhani akivunjiwa au tuhakikisha kina Mama Pendo, Khadija na Sikudhani wanakuwa sio wabangaizaji na mara nyingine wavamizi wa maeneo ?!!!!

Tunahitaji kuja na Sera za watu kupata Ujira wa kujitosheleza bila kuvunja Sheria au kuwa wachuuzi ambao they are one sickness away from loosing everything.....

By the way... Wakati tunamvunjia mama Pendo na kutokumpa alternative ya kipato bado tunamkamua kila kona...



👆 Hilo ndio la kupazia sauti na si vinginevyo...
 
Hii ndio fisiem y CHURA matajiri wenzake wanakula mema ya nchi.walala hoi KAZI tunayo.
All the best
 
Kulikuwa kuna haja gani ya kusema ni SINGO MAZA,,,Unajua ifike wakati tuwe tunafanya mambo kiasi kwamba watu wasikushushie heshima.

We mzee na degree zako zote kwanini unaact kama sio msomi. Yamkini unataka hili jambo lako lishughulikiwe kwa hisani na sio weledi na haki😄😄😄

Na huko law school ulienda kuchukua cheti, wewe ni mwanasheria kweli au ni wale wanaojiendeleza kukusanya vyeti.

Hata kama huyo mama ameonewa wewe kama mwanasheria ulikuwa ndo wakati wako sasa wa kuonyesha ubora wa elimu yako kwa kumtaarifa huyo mama kufika sehemu husika za kimamlaka ili aweze kupata haki yake.

Au kama ni haki hicho kibanda kuvunjwa hapo lazima tuseme wazi SHERIA IFATE MKONDO WAKE,,,,PERIOD!!! Uwe kiwete, uwe singo maza wa taifa, uwe mjane sheria haiangalii hali yako ila usawa ili kusiwe na upendeleo kesho mwingine akibomolewa watu waanze kunyoosheana vidole, mbona flani hakubomolewa.
 
Ingekuwa siku takazi najua nigekimbilia mahakamani fasta kuweka stop order,pole yake mama,hata kama ni chumba kimoja ungeandika kuwa ni nyumba,ile kuita kwamba ni kibanda imefanya nipoteze mzuka wa kumsaidia
 
Ni Tegeta kwa Ndevu au ni wapi tena. Naona Tegeta kwa ndevu pamekuwa wa moto pana trend balaa
 
Ngoja niwahi chaap badala ya kuchati operation okoa mama. Nitawapa mrejesho
 
Back
Top Bottom