Mwanamke mmoja aligundua mama yake mzazi anatoka kimapenzi na aliyekuwa mme wake

Mwanamke mmoja aligundua mama yake mzazi anatoka kimapenzi na aliyekuwa mme wake

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
1646040919715.jpeg

Mwanamke mmoja nchini Kenya aitwaye Martha Wanjiku, ameeleza kisa chake, baada ya kubaini mama yake mzazi amekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na aliyekuwa mume wake kwa zaidi ya miaka 25.

Martha ameeleza kwamba aliolewa na mwanaume huyo na ndoa yao ilidumu kwa miaka miwili pekee na ilipofika mwaka 2020, alibaini mama yake ana mahusiano na aliyekuwa mume wake huyo, alipoenda kuamulia ugomvi baada ya kupigiwa simu na kuambia mama yake anapigwa.

"Nilishtuliwa na simu siku moja asubuhi, nikaambiwa nikaokoe mama yangu anapigwa na mume wangu wa zamani, na nilipomuuliza kwanini anafanya hivyo, aliniambia mtu anaulizwanga akipiga bibi yake?," alieleza Martha.

Aidha, Martha ameongeza kuwa mama yake alikuwa kwenye mahusiano na mwanaume huyo hata kabla ya wao kuoana na kudai kwamba alishamsamehe lakini hawezi tena kupata ujasiri wa kumtambulisha mama yake hata atakapopata mwanaume mwingine.

Chanzo: Emotional woman says ex-hubby and her mom had an affair for 25 years
 
Duh pole yake.

Nimeupenda msuko wake,yeboyebo safi kabisa
 
Back
Top Bottom