Mwanamke mpole na mtulivu sana

Mwanamke mpole na mtulivu sana

Babu shikamoo
Niunganishe na huyo mjukuu wako tuanze maisha. Mwambie kuna mkarismatiki huku namhitaji sana awe mke wangu....

Unajua kuna kitu anakipitia huyo mjukuu na nakielewa kwa undani sana.
Harafu pia anahitaji watu tusio na mambo mengi na tunasali sana.

Akikubali niunganishe naye
 
Niliwahi kufundisha chuo kikuu kimoja hapa Tanzania,nilikuwa na mwanafunzi mmoja,ni mpole,mkimya,hana makuu,hanywi pombe,haendi out,ni mtulivu sijapata kuona.Ni mkristo lakini huvaa,ushungi kila siku na darasani alikuwa wastani tu.Akamaliza na alipata kazi mji huohuo aliposomea,baada ya miaka 2 nilienda kumtembelea,alipopanga,nilimkuta na sifa zake zilezile,niliongea nae sana na akaniambia kuwa mpaka sasa hajapata mchumba japo anatafuta sana mwenza na anasali kila siku.Nilishangaa mdada mzuri kama huyo kukosa mume,kweli hata mie roho inaniuma sana
Wewe kumtembelea tu ghetto inamuondolea credit za kuolewa, kwanza wewe ni mwl wake, alafu ukute unapenda kuanzisha urafiki na wanafunzi wa kike,hata kama huwagusi, Sasa vaa uhusika,jifanye wewe ni mwanafunzi wa kiume ambaye ndiye alitakiwa awe mchumba Sasa, akikuona uko karibu na chombo, kichwani watawaza Nini!? Just as "demu mkalii ,mpole kumbe ni chombo ya teacher!! Teacher mwenyewe kiwembe,
Binafsi ni mtu mzima, Kuna baadhi ya Engle katika maisha yangu nilijua kabisa naweza haribu future ya wanawake Fulani,hasa kimahusiano ,nilijitahidi kukaa mbali, kama wewe ni mwl wa chuo jua heshima Yako ni kubwa, na uko so superior kwa wanafunzi wako wa kiume,wao ni rahisi kuaga mashindano Kila sehemu wanapokukuta umejiandikisha pia, wanajua una elimu,una pesa,una weza wapa sup za makusudi, so badala ya kudeal na wewe wanasepa Kisha wanamdharau Binti, na hawaishii hapo kwa hasira za kumkosa watamchafua Hadi basi, utasikia degree yake ya chupi, Hana jipya, hizi story zikisambaa Huwa zinaishi, tutazikuta Hadi job,



Hivo acha tabia ya kuwaweka mabinti karibu kwa status Yako, unawaharibia afu unakuja kushangaa, Kaa mbali watoto waoane
 
Upole si sababu ya Mtu kuwa Binadamu, kinyume chake ni sawa na Mtu aliyezaliwa na ukarimu ila kihulka ni Mkali au Mkorofi.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Kweli mkuu. Ukorofi ni matokeo ya kukosa amani moyoni hivyo kila binadamu ni mkorofi inategemea umemkuta wakati gani ila utu/ukarimu ni sifa anayozaliwa nayo ama kujifunza kupitia mapito yake, hivyo mwenye utu anaweza kuwa mkorofi pia.

Note: Kila binadamu ni mkorofi lakini si kila binadamu ana utu/ukarimu.
 
Sasa anajifungiaje ndani na anafanya kazi!!.🤔 Au kazi anafanyia nyumbani. Mara nyingi watu wapole hawanaga bahati, sijui kwanini🤔🤔🤔
sawa babu mkufunzi wa tuition,

mueleze mjukuu asijifungie chumbani tu, atoke nje ili hatimae akutane na mwenza wake anaemtafuta kwa muda mrefu sasa 🐒
 
Sasa anajifungiaje ndani na anafanya kazi!!.🤔 Au kazi anafanyia nyumbani. Mara nyingi watu wapole hawanaga bahati, sijui kwanini🤔🤔🤔
akitoka nyumbani tu pwwwiiiffuuu ofisini ndani. Akitoka ofisini pwwwiiiffuuu break ni ndani chumbani kwake, kwa style hiyo atapata wapi wakumchumbia na ikiwa tena kanisani haendi, msikitini haendi, kwenye seminar, warsha na makongamano ya vijana wenzie haendi n.k🐒
 
Niliwahi kufundisha chuo kikuu kimoja hapa Tanzania. Nilikuwa na mwanafunzi mmoja—mpole, mkimya, hana makuu, hanywi pombe, haendi out, ni mtulivu sijapata kuona.

Ni Mkristo, lakini huvaa ushungi kila siku, na darasani alikuwa wastani tu. Alimaliza na alipata kazi mji huohuo aliposomea. Baada ya miaka miwili, nilienda kumtembelea alipopanga. Nilimkuta na sifa zake zilezile.

Niliongea naye sana, na akaniambia kuwa mpaka sasa hajapata mchumba japo anatafuta sana mwenza na anasali kila siku. Nilishangaa, mdada mzuri kama huyo kukosa mume. Kweli, hata mimi roho inaniuma sana.
Mbona wapo wengi na hao kupata wachumba shida sana
 
Umetaja sifa za nje, Huenda sifa zake za ndani ni mbaya sana ...
 
Back
Top Bottom