Mwanamke msomi ni faida kwa ndugu zake na sio mume

Kama anasaidia ndugu si ndo vizuri ili asikuombe vihela vyako. Hamtaki kusaidia ndugu zao na hamtaki wao wawasaidie, mnataka nini nyie lia lia?
 
Kama hajawa faida kwa ndugu zake awe na faida kwa nani? Awe na faida kwako kwani ulimsomesha!!
 
Kitu pekee utachovuna kwa mwanamke ni watoto, uzao wako ndio Mali yako.
Subiri mpaka wababa wa watoto wako waje wakulipe hela ya matunzo kwa watoto wako, kisha wawabebe kwa kuwa wewe ni mlezi tu....
 
Papuchi na yas au Jadda
Kama hamvioni vingine wanavyoofa au labda mnajua ila mnajitoa tu ufahamu basi sawa lakini pia kusema kwamba mwanamke hana cha kuofa zaidi ya papuchi ni sawa na kusema mawingu hayana kingine cha kuofa zaidi ya mvua, huwa mnakiri wenyewe kwamba kitu cha muhimu zaidi mnachohitaji toka kwa wanawake ni hicho na hata kuhangaika kwenu kutafuta pesa asilimia kubwa ni kwa ajili ya kutumia na wanawake, sasa kwanini mnaongea kama vile hicho wanachoofa is nothing to you na kina mbadala na kwamba hata mkikikosa in your entire life hakuna impact yoyote
Sio kweli wanawake wa siku hizi hawana cha ku offer,mfano ndani usafi wa nyumba,kupika na kufua anafanya dada wa kazi-ingawa Mke yupo.
Ni kwa sababu mnataka wawasaidie majukumu haiwezekani mwanamke atoke kutafuta pesa na achangie uchumi wa familia halafu bado unataka kazi za nyumbani nazo afanye na bado akutii na akuheshimu, kama mke ni mama wa nyumbani hana shughuli yoyote ya kumuingizia kipato na unamhudumia kwa kila kitu halafu hataki kufanya kazi za nyumbani basi huyo hata mimi nakushauri fukuza, lakini kama mke anajitoa walau kiuchumi basi haina shida housegirl akifanya hizo kazi vinginevyo ni kutaka kumtwisha mwanamke mzigo wa majukumu na mwisho wa siku kumfanya asione umuhimu wa mwanaume
Wewe naye usipende kukurupuka kama hujaelewa hoja uliza siyo kurukia kwenye hitimisho na kujikuta unamlisha mtu maneno, kama huyo mwanamke wako unamhudumia basi hana budi kujitoa kwako ila mimi nazungumzia hawa wanawake ambao mnataka wawasaidie majukumu, halafu tunapozungumzia wanawake tunazungumzia wote kwa ujumla hata housegirl naye ni mwanamke kwahiyo kama unaona housegirl ana vingi zaidi vya kuofa kuliko mpenzi wako basi muache oa housegirl tatizo liko wapi
Yani huwa mnanifurahisha sana mnavyojikuta wanasaikolojia uchwara na kujifanya mnanijua kwa kuongelea sifa zangu na maisha yangu eti kisa mitazamo yangu ninayoiwasilisha humu, halafu mbaya zaidi mnapishana kauli kuna mwingine nimetoka kubishana naye huko kuhusu mada kama hii yeye anasema mimi naonekana nimetoka kwenye familia masikini na yenye migogoro mara sijui nimeumizwa na wanaume ndio maana nimekuwa feminist, mara sijui nitakuwa na sura ya baba na umbo la mwanaume maana mwanamke mrembo hawezi kuwa na mitazamo kama yangu sasa sijui nishike lipi ila nikishaonaga mtu anatoka kwenye mada anaanza kuleta ad hominem attacks kama hizo huwa najua tu ni defensive mechanism baada ya kuishiwa hoja
Hivi huu unafiki wako utaacha lini kwani ninyi si ndio wale mnaosema kuwa wanawake waache kuwategemea wanaume waanze kujitegemea wenyewe na wajifunze kuwasaidia wanaume zao pale wanapokwama, sasa mnataka kuwapa wanawake majukumu sawa wakati hiyo haki sawa tu hamjamaliza kuwapa na hamko tayari kuwapa, mfano mpaka leo pamoja na kwamba wanawake wengi wameshaanza kutafuta pesa zao wenyewe na wengine wakiwasaidia wanaume zao lakini bado mnataka waendelee kuwatii na kuwaheshimu kwa kila kitu sasa mnataka hilo kwa misingi ipi, ofcourse hamuwezi kuyatamani majukumu ya wanawake sababu mnajua ni magumu ingawaje mnayadharau ilihali wanawake wanaweza kufanya majukumu yenu vizuri tu, kwahiyo kwa hapa tulipofikia tunaona ni nani mwenye shida maana wanawake wameshaonesha wako tayari kwa majukumu sawa ila wanaume ndio hamko tayari kwa haki sawa ndio maana baadhi ya wanawake bado wanasita kukubali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…