Mwanamke mwenye miaka 30+ hujaolewa unasubiri nini?

TatIzo lingine ni wanaume kufikiri miili yetu ni kwaajili ya wao kujifurahishia wakati miili yetu ni ya Bwana, tena imenunuliwa kwa Bei. Kwa damu.

Wewe mwanaume Uko tayari kumwaga damu kwa ajili yangu?

"Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, ambaye mlimpokea kutoka kwa Mungu? Nyinyi basi, si mali yenu wenyewe.

Mlinunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo, itumieni miili yenu kwa ajili ya kumtukuza Mungu."

1Wakorintho.6.19-20.BHN
 
Hii hoja yako ndio niliyoitumia kumwambia dada mmoja mwenye masters na yupo 34 yrs na hajapata mchumba,pamoja na tabia zake njema kabisa,hanywi pombe,haendi vijiwe,havai hivyohovyo,ni mkatoliki mwenye kusali na ni mtu wa low profile.Pamoja na sifa zote hizo hajawahi kupata mwanaume aliyemwambia amuoe.Hatimae ameamua kufunga ndoa ya serikali na mwanaume wa kiislamu ambaendie alimtamkia kuwa yu tayari kumuoa na wamefunga ndoa ambayo haina sherehe yoyote ile na sasa bibie ni mja mzito.Mungu amsaidie ndoa yake idumu
 
You snapped with this one!😅

I second you gurl🫰🏾
 
Labda kama mtoa mada ungesema kama umri huo bado mwanamke hana mtoto hata bila ndoa. Mpaka kufikia umri huo halafu mwanamke hana mtoto wakati amebakisha miaka michache afikie menopouse basi huo ni uzembe wake, hakutumia vema talanta yake aliyepewa na Mungu
 
Wao wenyewe hawana ajira za kueleweka wamepagawa, sasa hivi wenzao tumejipata tunawaza kuwekeza pesa sio poumbou basi yana makasiriko kila nyuzi kutusema..!! 😹😹😹
Inasemekana mwanamke ndiye anayehitaji ndoa, lakini mwanaume ndiye anayemsimanga mwanamke kwa kutokuolewa na hukuti mwanamke anamsimanga mwanaume kwa kutokuoa. Ukichunguza hili vizuri utagundua anayehitaji ndoa kuliko mwenzake ni nani 😅

Mada ingeletwa na mtu anayejielewa tungejadili serious, shida huyu mleta mada huwa ni dishi fulani so wala tusihangaike kumuelewesha chochote.

Mate, ngoja mi nimalizie chai, Mfungo mwema.
 
Kuna binti mmoja nilimhoji aniambie alipo baba wa watoto wake, alinijibu kuwa alipoona umri unapanda huku hajapata wa kumuoa akaamu kujiachia kwa waume za watu, akapata hao watoto. Yuko vizuri kiuchumi anaendesha maisha yake vema akiwa single mother
 
Wasikuseme sana wewe njoo nikuoe mimi halafu basi hizi lawama ziishe maana hakuna namna tena
 
Olewa wewe muda una kimbia sana 45 mpaka 50 sio mbali mwanaume hata miaka 100 anatungisha mimba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…