Wakuu habari za muda huu tena.. nashukuru kwa michango yenu, japo wapo watu wamedhihaki na wengine wamechangia positive.
Nimeumizwa sana na suala hili kiukweli, pale nilipowekeza nikitegemea neema nakutana na maumivu.. msichana mzuri kiasi kile kaingia kwenye kasumba kama hii, sikia kwa mwenzako tu
kiufupi ilibidi nimtafute mwanadada kwa njia ya simu, tumeongea takribani masaa mawili na dakika 23, maongezi ambayo nimepata kujua upumbavu mwingi zaidi wa huyu mwanadada baada ya mazungumzo na maswali magumu niliyohoji
nimepata kujua rasmi kuwa mwanamke hata kwenye unafiki atamwaga machozi tu na ndio defensive mechanism Yao.. nimemwambia kuna upuuzi kumbe huwa unafanya, unajiuza mitandaoni halafu una-act unanipenda, eti analia nimemuita malaya namdhalilisha.. nimemwambia Dunia Haina siri, hakuna nisichojua zaidi tena.. eti anasema tatzo langu naamini maneno ya watu.. nimemwambia sio maneno, hadi ushahidi upo.. Bado anagoma tu na anaapia kabisa hajawahi kutumia telegram.. ikabidi nimtukane sasa maana hasira zilinipanda kuona unafiki ule ikabidi nimwambie mzigo huo angalia Whatsapp kwako, nikamtumia picha, aisee
Amepiga simu baada ya kuona picha zile, ni KULIA tu anaomba nimsamehe sana kwamba sio michezo yake amefanya tu kwa mara ya kwanza aone reaction kama watu watamsumbua 😡😡😡 ila hakudhamiria kutoka na yeyote ambae angemwendea direct..
hasira niliyopata angekuwa karibu Leo ndio ingekuwa mara yangu ya mwisho kuwa uraiani.. nimemuuliza maswali yote ambayo ni dukuduku zangu baada ya kukutana na upumbavu wake nikamwambia asinifiche kitu.. aisee ni Bora nisingeuliza tu.. Nimeconnect na dots baadhi ambazo zilijitokeza before ambapo baada ya kujibiwa zimenipa patterns kibao juu ya huyu mrembo niliemwamini kupindukia. Wazee wa KATAA NDOA huwa wapo sahihi tu. Nimemwambia aniache kwanza kwakuwa anarudi jumanne ntampa majibu yake kama tutaendelea au la.
Amepiga simu hadi Kero, nimeblock namba zake Kila Kona. Mdogo wake kapiga sjapokea, rafiki yake pia kapiga zaidi ya mara tano na sms juu ila nimepiga kimya maana namuona ni walewale, wanajua upumbavu unaoendelea halafu yanakomaa kuniita shemeji.. 😡😡😡
Ngoja aje