Mwanamke niliyezaa nae ananipa majukumu yasiyonihusu

Hii comment ndio niliyoielewa vzuri, naahidi kumhudumia kadri ninavyoweza. Ahsantee Mkuu kwa Muda wako wa kunisaidia mawazo.
Pamoja sana mkuu. Nimekujibu from experience nimewahi pitia same situation unayopitia!
 
ana mtoto mwingine ukitoa huyo wa kwako?
 
Mkuu kuna wanawake wengine si wa kuzaa nao, ndiyo maana yabidi kutumia condom kama hauko tayari kuzaa ama kuoa.....unajiletea mateso ya moyo bure na kujipunguzia siku za kuishi duniani. Si unafahamu hapa duniani tunaishi na majini pia, tena wako wengi tu hapa Dar. Mwingine yule namuona anapita hapa barabarani, ngoja nikamsalimie.
 
Kama mama mtoto hauna mahusiano naye tena basi wewe unahusika na vitu 2 tuu:

1. Chakula cha mama(food)
2. Mahitaji ya mtoto.

Ni hayo tuu, narudia tena ni hayo tuu kulingana na sheria za ustawi wa jamii.

Mambo ya nyumba,biashara/kazi HAYAKUHUSU KISHERIA ila kama uko vizuri ukaamua kumsaidia kibinaadamu hapo sawa ila sio yeye aanze kukuforce.
Unforgetable
 
Kama hata mtoto hajamuona usikute hata mtoto hayupo ni siasa tu za ulimwengu😂.

hii kazi ngumu
 
Ila hujainisha tatizo lililokufanya usitake kuishi nae. ..ninachoona baby mama anachokitaka kutoka kwako ni attention yako tu and she's scared atakupoteza. Unless awe na issue ambayo alishawahi kukufanyia rather than that she's desparate for your attention.

NB: Sijui ataolewa na nani kama mzazi mwenzie hamtaki.
 
Chukua mtoto peleka kwa mama yako, kama huwezi lipia bills za matumizi ya mtoto usimpe hela. Kumbuka pia mama aliyejifungua huwa wana ukichaa fulani (kichaa cha mimba).
 
Chukua mtoto peleka kwa mama yako, kama huwezi lipia bills za matumizi ya mtoto usimpe hela. Kumbuka pia mama aliyejifungua huwa wana ukichaa fulani (kichaa cha mimba).

Shida sina mama, alishatangulia mbele za Haki. Kuna wadau wamenishauri nijaribu kuhudumia kadri ninavyoweza na pia nijaribu kucheza na akili za huyu mama mtoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…