Mwanamke niliyezaa nae ananipa majukumu yasiyonihusu

Mwanamke niliyezaa nae ananipa majukumu yasiyonihusu

Usikubali kupelekeshwa kizembe.
Kwanza je, una uhakika huyo mtoto ni wako?
Kama mtoto ni wako lazima mgawane majukumu, sio mzigo wote wa kulea anakuletea wewe. Yaani mama anataka pesa za kununua na kutengeneza simu, vocha, nguo za mama, saloon, mtaji wa biashara nk kisa nimezaa naye! Huo ndio ujinga wa single mothers wengi, wanatumia mtoto kama mtaji wa kuishi mjini.

Ningekuwa ni mimi ningeweka msimamo mmoja tu, mama alee mimba yake na mtoto mchanga kwa gharama zake mpaka mtoto akue na kujitambua (labda miaka saba), baada ya hapo anipe mtoto wangu nimlee mimi mwenyewe mpaka atakapokuwa mtu mzima. Anayekaa na mtoto, ndiye anayelea na ndiye analipa matumizi. Tofauti na hapo, toka mtoto anazaliwa mpaka anakuwa mtu mzima tunagawana gharama za kumtunza kwa 50% kwa 50%. Hiyo ndio maana ya haki sawa.
 
Habari za wakati huu wapendwa na wanajamvi wenzangu wa MMU. Poleni kwa kazi na kwa wale walioenda kusali hongereni kwa ibada.
Nianze mkasa wangu juu ya huyu Baby mama wangu, Hapa juzi kati (wiki iliyopita) mwanadada aliyedai kuwa anaujauzito wangu na kunikabidhi kulea, alijifungua salama na Mtoto wa Kiume Mungu akajalia.

Anaishi kwao na mimi naishi kwangu, mwanzo alitaka aje akae nami tulee mimba pamoja nilikataa kwa sababu zangu binafsi. So ikabidi akae kwao tu, sasa tangu amejifungua nimekuwa nikituma pesa kwa ajili ya mahitaji ya msingi kwaajili ya mtoto na mama mtoto ukizingatia mtoto bado anategemea kila kitu kutoka kwa mama yake.

Kuna baadhi ya mahitaji ananitajia kimsingi mimi nayaona kama sio sahihi mimi kuhudumia kwa maana mahusiano mimi na yeye yaliisha na mimi nikawa nime move on na yeye akawa ame move mwanzoni kabisa mwa ujauzito. Sasa wakati kuna majukumu mengine naona kama napewa mzigo usio wangu, kwa mfano ananiambia nimlipie kodi ya nyumba akaishi kwake, ikiharibika simu hela ya matengenezo anapiga simu kwangu na niliwahi mpatia mara moja akatengeneza ila naona kama anazidi kuleta mazoea anataka nimpatie mtaji au nimfungulie biashara ili asinisumbue ishu ya matumizi ya mtoto [emoji3064], nilikataa nikamwambia nitatoa hela ya matumizi kila mwisho wa mwezi ila sio kukufungulia biashara.

Tokea hapo, ikitokea amepiga simu na nikawa sijapokea labda ikawa iko mbali au sikusikia anatuma mimeseji ya ajabu... Mara naona unakatika mauno juu ya huyo malaya wako ila simu ya mwanamke anayekulelea mwanao hupokei” sikujibu lolote ni nyingi tu mara unatumia pesa na malaya wako ila hela ya mtoto hutoi.! Pesa natoa ila yeye anaiingiza kwenye matumizi yake binafsi so namimi nakaza.

Sasa nimekuja kwenu, wanaume wenzangu ambao tunaohudumia hawa akina mama mnafanyaje ili kufanya hili suala la malezi kuwa rahisi na kupunguza mivutano na huyu mwana mama (Baby mama)

Naomba kuwasilisha, naombeni michango yenu wakuu

Mkuu lipa kodi ya nyumba ni sehemu ya majukumu yako kwake.
Unategemea mtoto aishi nae wapo

Kama mtu amekuzalia mtoto kwanini hata husitoe ka shukrani kwa kumfungulia biashara.

Acha hzo bro.
Kulea si mchezo, wewe huwez
 
Naona unapigilia msumari..! Ila kusema ukweli nahudumia ila biashara na Kumangishia itafanyika kama kuna huo ulazima. Anakaa kwao alfu yeye anajipiga kifua kwenda kupanga so mie nifanye nini.! Mmh

Matusi ya kuishi na mtoto nyumbani kutoka kwa wazaz sio poa

Mpe heka akapange
 
Mkuu lipa kodi ya nyumba ni sehemu ya majukumu yako kwake.
Unategemea mtoto aishi nae wapo

Kama mtu amekuzalia mtoto kwanini hata husitoe ka shukrani kwa kumfungulia biashara.

Acha hzo bro.
Kulea si mchezo, wewe huwez

Biashara ?? You can’t be serious asee. Nimfungulie biashara ni mke wangu au ?? Hapo na mwanaume wake alfu mimi hela yangu ndio iwe inamlisha huyo jamaa ...! Never
 
Back
Top Bottom