Mwanamke ukiishi naye kinyumba (bila ndoa) hata kwa miaka kadhaa, kisheria hastahili kupata chochote endapo mtaachana

Mwanamke ukiishi naye kinyumba (bila ndoa) hata kwa miaka kadhaa, kisheria hastahili kupata chochote endapo mtaachana

Mwanamume

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
271
Reaction score
216
Huu ni ushuhuda wa kweli. Kuna mwanaume amepata ushindi mahakamani dhidi ya gumegume, ambao inabidi tushirikishane hapa ili wanaume msiogope kuwafukuza wajasiriaNDOA a.k.a "makupe"au magumegume.

Kuna wanasheria uchwara huku kitaa, wanatutisha kuwa ukikaa na mwanamke kwa zaidi ya miezi 6 basi huyo ni mkeo (yaani umeoa tayari ) na ana haki zote. Nadharia hii si ya kweli, na hata kama ni ya kweli basi haifanyi kazi mahakamani.

Mahakama inatambua uwepo wa ndoa kwa kutumia nyaraka (cheti cha ndoa), siyo kwa ngonjera na hadithi.

Kuna mjuba alijitwisha gumegume miaka 6 iliyopita huku akiwa kajipanga vema kimaisha. Kumbe gumegume halikuwa na mapenzi ya dhati bali lilitaka kufyomonta (syphoning) ukwasi wa mjuba. Baada ya miaka 3 likaanza kutikisa kiberiti. Mwaka wa 6 gumegume likakata kamba (likavunja mahusiano) na likafungua kesi mahakamani kudai mgawo wa mali.

Mjuba aliliruka gumegume mita 100 na kudai kuwa hakuwa mke bali alikuwa hawara tu. Mjuba huyu ameshinda kesi hiyo kwasbb gumegume lilkosa nyaraka (cheti cha ndoa) kuthibitisha uwepo wa ndoa hiyo.

Gumegume limeaibika na kukosa hata senti kutoka kwa mjuba.

Asanteni
 
Safi sana
1683544135698.jpg
 
Mwanamke ukiishi naye kinyumba (bila ndoa) hata kwa miaka kadhaa, kisheria hastahili kupata chochote endapo mtaachana
Siyo kweli, kuna jambo hujaelewa hapo..

Kilichomuokoa huyo "mjuba" ni kuwa alichuma hizo mali zake zote kabla hajaanza kuishi na huyo mdada.

Kama angechuma hizo mali wakiwa wanaishi pamoja hata bila ndoa rasmi, wangegawana kama kawaida
 
Sheria zingine za ndoa ni za kipuuzi sana. Yaani uishi na mwanamke mzae watoto na mpate maaendeleo halafu mwanamke asitambulike katika mgao wa mali? Kwani ndoa ni lazima iandikishwe huko kwenye usajili? Ndoa inaanza pale ushirikiano ndani ya nyumba unapoanza, hiyo ndio ndoa. Kama mwanamke ataasi basi aondoke tu aache mali aende akaanze kutafuta upya kwingine
 
Basi ndiyo sababu mjuba kapata ushndi wa kishindo kwenye kesi hii
Nadhan akipata ushindi wa kuwa mlalamikaji alishindwa thibitisha vigezo vilivyo ainishwa kwenye Sheria kama vilivyo ainishwa na kifungu Cha 160 Cha Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971
 
Back
Top Bottom