MKE WANGU ANANISUMBUA
BABU: Denis! Denis! Mbona umejiinamia mjukuu wangu, kulikoni?
DENIS: ...Oooh! Acha tu Babu...Mke wangu ananisumbua sana...kwanza shikamoo Babu...
BABU: Marhaba mjukuu wangu Denis....Tazama ulivyotingwa na mawazo mengi kichwani. Pole sana Denis... Tatizo ni nini?
DENIS: Sijui nikuelezee nini Babu?, nampenda sana mke wangu...nimefanya kila kitu ili awe na furaha lakini bado ananisumbua. Nimekuwa mkamilifu kwake...sijui anataka nini nimfanyie?
BABU: Aaaaah! Umenifurahisha sana leo mjukuu wangu. Najua unampenda sana mkeo. Bahati mbaya huwajui wanawake. Kwa miaka 79 ya maisha yangu hapa Duniani....Nimejifunza haya kwa wanawake. Sikiliza!!!
BABU:Japo watu wengi wanasema...mwanamke hajui anachotaka lakini ukweli ni kuwa, mwanamke anapenda vitu vigumu.
Wao (Wanawake) wanasema wanapenda mwanaume aliye "romantic" ukweli ni kwamba; wanawake wengi wanawaumiza wanaume walio romantic. Kwahiyo, wanachokisema sicho wanachokitaka.
Kadiri unamvyompenda sana mwanamke ,ndivyo unavyokaribia kumpoteza.
Wanawake kiujumla wanavutiwa na wanaume walio wababe, wenye misimamo na wasiojali sana. Wanawake hawapendi wanaume wapole sana.
Ukimsikiliza sana anachokitaka....Mwanamke anakudharau. Wanasema wanapenda maneno matamu kutoka kinywani mwa mwanaume lakini ukweli sio wanavyomaanisha.
Kiujumla...wanawake wanapenda vitu ambavyo wao hawana.
Denis! Denis! nisikilize hapa kwa umakini......
"Maji tumekuwa tukiyatumia nyumbani na yana thamani kubwa sana katika uhai wa mwanadamu, lakini hakuna hata siku moja ambayo umewahi kuwazia juu ya uthamani wake.
Kwa kuwa upatikanaji wake ni rahisi pamoja na umuhimu wake maji ,hayana thamani sokoni.
Madini mfano dhahabu, Tanzanite, Almasi hayana mchango wowote katika uhai wa mwanadamu lakini ndio kitu chenye thamani kubwa sokoni kwa sababu upatikanaji wake ni mdogo"
Je umenielewa ?
DENIS: Nimekuelewa kiasi Babu...Nakusikiliza....
BABU: Kupatikana kwako muda wote kwa mkeo ,kunasababisha thamani yako kupotea. Upendo wa mkeo kwako unapotea. Kuwa karibu na mkeo kila mara ni makosa.
Kumbuka Denis...Mwanadamu ukiheshimu na kukithamini kitu anachokipata kwa tabu na kukihangaikia kuliko kitu anachokipata kwa urahisi. Nenda kafikirie...Haya ninayokueleza.
DENIS: Asante sana Babu...nimejifunza mengi....nataka kuwa wa thamani sasa.
BABU: Nataka kukuaga....naomba nikupe wosia kuhusu wanawake....mwanamke anapenda shuruba kiasi, kunyanyaswa kidogo katika mapenzi. Sisemi usiwe romantic...bali kuwa kwa kiasi. Usipende kusikiliza kila kitu akisemacho kwa kukubali tu...atakudharau. Asante kwa kunisikiliza. KWAHERI
DENIS: Ooooh! Asante sana kwa elimu yako Babu..Nimejifunza na nina hakika naenda kuwa mtu mpya.
Hii nimeikwapua kwa mkuu Prosper Kimboka