Mwanamke ukimtukuza na kumnyenyekea sana uwe na uhakika atakunyea kichwani! Inabidi tukae nao kijasusi!

Mwanamke ukimtukuza na kumnyenyekea sana uwe na uhakika atakunyea kichwani! Inabidi tukae nao kijasusi!

Tunakumbushana tu..... Ni marufuku mwanaume kulia lia na mapenzi. Mwanaume hautakiwi

:kukonda kisa mapenzi
:kufirisika kisa mapenzi
:kupoteza nguvu kisa mapenzi
:kupoteza Muda kisa mapenzi
:kuhangaika na mwanamke asie na manufaa
:kuendelea kuwekwa kwenye urafiki (friend zone)
:kutongoza mwisho ni siku Tatu kwa mwanamke mmoja akizingua piga chini angalia mwingine kuokoa Muda.

Na kama tulivyo kubaliana kwenye kikao kilicho pita kuwa tunataka Taifa lenye uume na imara sio la wanaume wanao lia lia na mapenzi.

Mwanaume ni marufuku kuendelea kuteseka na huyo mwanamke eti kisa anakulelea wanao.... Mwanaume hauna haja ya kuogopa piga chini ingia chimbo tafuta pesa leta dada wa kazi akusaidie kutunza na kama kuna uwezekano peleka kwa bibi yao ila hakikisha pesa za matumizi zinaenda ikiwezekana zaidi na mfanya kazi nae aende kwa bibi huko huko kwa uangalizi zaidi.

Wanaume ni kwamba tumelegeza sana hadi wanawake wanatuendesha hili halitakiwi na tukizembea zaidi mbinguni hatuta ingia kwa sababu power tulio pewa na mwenyezi Mungu tumeshindwa kuitumia.

Pia mwanaume hautakiwi kuogopa kumuacha mwanamke asie fit ndoto zako.... Wanawake ni wengi wee tu katika picha hao wote ni wajane wa dar tu bado masingo maza nk... Unaogopa nn kufanya maamuzi ili kuokoa Muda na afya yako kwa kimtu kisicho fit ndoto zako.... Piga chini ukajenge Taifa.

Nk ni marufuku kwa mwanaume kumnyanyasa mwanamke alie tulia na msikivu na ukibainika unamfanyia ukatili mwanamke wa sampuli hiii adhabu yake tusilaumiane.

Kwa leo inatosha

(WANAUME TUREJESHE UUME WETU)
HILI ANDIKO LA MTU FLANI, SIMKUMBUKI JINA
 
MKE WANGU ANANISUMBUA
BABU: Denis! Denis! Mbona umejiinamia mjukuu wangu, kulikoni?

DENIS: ...Oooh! Acha tu Babu...Mke wangu ananisumbua sana...kwanza shikamoo Babu...

BABU: Marhaba mjukuu wangu Denis....Tazama ulivyotingwa na mawazo mengi kichwani. Pole sana Denis... Tatizo ni nini?

DENIS: Sijui nikuelezee nini Babu?, nampenda sana mke wangu...nimefanya kila kitu ili awe na furaha lakini bado ananisumbua. Nimekuwa mkamilifu kwake...sijui anataka nini nimfanyie?

BABU: Aaaaah! Umenifurahisha sana leo mjukuu wangu. Najua unampenda sana mkeo. Bahati mbaya huwajui wanawake. Kwa miaka 79 ya maisha yangu hapa Duniani....Nimejifunza haya kwa wanawake. Sikiliza!!!

BABU:Japo watu wengi wanasema...mwanamke hajui anachotaka lakini ukweli ni kuwa, mwanamke anapenda vitu vigumu.

Wao (Wanawake) wanasema wanapenda mwanaume aliye "romantic" ukweli ni kwamba; wanawake wengi wanawaumiza wanaume walio romantic. Kwahiyo, wanachokisema sicho wanachokitaka.

Kadiri unamvyompenda sana mwanamke ,ndivyo unavyokaribia kumpoteza.

Wanawake kiujumla wanavutiwa na wanaume walio wababe, wenye misimamo na wasiojali sana. Wanawake hawapendi wanaume wapole sana.

Ukimsikiliza sana anachokitaka....Mwanamke anakudharau. Wanasema wanapenda maneno matamu kutoka kinywani mwa mwanaume lakini ukweli sio wanavyomaanisha.


Kiujumla...wanawake wanapenda vitu ambavyo wao hawana.


Denis! Denis! nisikilize hapa kwa umakini......

"Maji tumekuwa tukiyatumia nyumbani na yana thamani kubwa sana katika uhai wa mwanadamu, lakini hakuna hata siku moja ambayo umewahi kuwazia juu ya uthamani wake.


Kwa kuwa upatikanaji wake ni rahisi pamoja na umuhimu wake maji ,hayana thamani sokoni.


Madini mfano dhahabu, Tanzanite, Almasi hayana mchango wowote katika uhai wa mwanadamu lakini ndio kitu chenye thamani kubwa sokoni kwa sababu upatikanaji wake ni mdogo"


Je umenielewa ?

DENIS: Nimekuelewa kiasi Babu...Nakusikiliza....

BABU: Kupatikana kwako muda wote kwa mkeo ,kunasababisha thamani yako kupotea. Upendo wa mkeo kwako unapotea. Kuwa karibu na mkeo kila mara ni makosa.



Kumbuka Denis...Mwanadamu ukiheshimu na kukithamini kitu anachokipata kwa tabu na kukihangaikia kuliko kitu anachokipata kwa urahisi. Nenda kafikirie...Haya ninayokueleza.


DENIS: Asante sana Babu...nimejifunza mengi....nataka kuwa wa thamani sasa.

BABU: Nataka kukuaga....naomba nikupe wosia kuhusu wanawake....mwanamke anapenda shuruba kiasi, kunyanyaswa kidogo katika mapenzi. Sisemi usiwe romantic...bali kuwa kwa kiasi. Usipende kusikiliza kila kitu akisemacho kwa kukubali tu...atakudharau. Asante kwa kunisikiliza. KWAHERI


DENIS: Ooooh! Asante sana kwa elimu yako Babu..Nimejifunza na nina hakika naenda kuwa mtu mpya.



Hii nimeikwapua kwa mkuu Prosper Kimboka
 
dawa ni kujizima data tuh na kujiambiza kichwani yaleyale kisha unapotezea
 
Duuh karibia watu watavaa boxer kichwani kila siku nyuzi za mikakati ya jinsi ya kuwadhibiti wanawake 🤣
 
Back
Top Bottom