Tabia ya kubambikizia akina baba watoto wasio wao imeendelea kushamiri miongoni mwa akina mama. Swali langu kwenu, mnakuwaje na amani katika maisha yenu kwa kukaa na siri kuu namna hiyo? Unakuta wengine wamekuwa walokole au wanaenda kuungama, je dhambi hii mnaiungama pia? Na kama mnaiungama, je mnawaomba msamaha wenzi wenu? Kama sivyo, mnadhani mnaweza kupata msamaha muutakao bila kuwashirikisha waathirika? Hapa namaanisha akina baba wanaobeba mzigo usio wao kwa maisha yao yote bila kujua.