My dear kuna mtu alishawahi kukufundisha kuwapenda wazazi, watoto wako au ndugu zako? Tulijikuta tu tunawapenda since we found them there for us. Muda tunaoutumia pamoja, vitu tunavyofanya pamoja, wanavyotujali automatically tunajikuta na sisi tunawapenda na kuwajali na tunatengeneza bond ambayo si rahisi kuvunjika. Ndiyo maana utagombana nao weee, mtanuniana but still mtamend your broken relationship. Anza kumjali mumeo, mchukulie kama ndo nusu yako, furaha yako; fanya vitu vitakavyompa furaha. Yani anza kuona kuwa huyo ndo mumeo, na hiyo ndo ndoa yako na hutokuwa na ndoa nyingine, na huna option nyingine ila kuona ndoa yako (including wewe mwenyewe), mna furaha.
Ungekuwa kwenye dating maybe tungekushauri muachane, ila ndo mmeshakuwa familia tayari. You were very selfish kuingia ndoani na huyo mwanaume now clear your conscious, mfanye mumeo kama ndo "project" yako mpya unayoianzisha ukiwa na "goal" ya kutengeneza ndoa imara yenye furaha. Put in your all; sacrifice everything you can to make your marriage enjoyable.
Ndugu, sijui kama unajua how blessed you are to have such kind of a man; He is such a rare gem (inawezekana unajua ila kwa sababu upo naye, unaona kama kitu cha kawaida tu). Ukikutana na "waathirika wa ndoa", utalia na kujuta kwa nini unamfanyia hivyo mumeo. Afu wanaume wa hivyo siku akigundua jinsi unavyomuwazia ndugu you will surely regret. Atakavyokubadilikia, hutoamini kamwe na inawezekana isiwe rahisi sana kuja kurudisha mambo kama yalivyokuwa before . You have bagged yourself a good man; usiwe mwanamke mpumbavu; keep him oooh keep him.
Amua kwamba unataka kuwa na ndoa ya furaha. Muaccept/embrace mumeo. I know kuna wishes/matarajio fulani kwenye maisha lakini hadi leo hujayapata, je umeacha kuenjoy maisha au umesema haya ndo maisha yangu na nitayaishi to the fullest? Amua kuenjoy your marriage mama. Ukija makanisani wenzio wanavyoomba hata waume zao waugue angalau tu waweze kupata muda wa kukaa nao......! Amua tu mama.
Btw, huko moyoni mwako hamna mtu/ex ambaye umembeba and possibly ndo anakufanya unashindwa kureciprocate upendo wa mumeo? Leave everything behind for the sake of your marriage.